Rostam azidi kuanikwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam azidi kuanikwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 12, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Rostam azidi kuanikwa

  [​IMG]
  Na Alfred Lucas - Imechapwa 12 February 2011

  [​IMG][​IMG] [​IMG]

  SIRI imefichuka. Kampuni ya Dowans Holdings SA inayodaiwa kusajiliwa nchini Costa Rica, haikuwa na “biashara nyingine yeyote duniani” wakati ikimpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (Power of Attorney) ya kuiwakilisha nchini Tanzania.

  Hii ndiyo kampuni inayodai TANESCO Sh. 94 bilioni kwa kukatisha mkataba wake wa kufua umeme ilioupata kutoka kampuni hewa ya Richmond Development (LLC).

  Taarifa hizi zimepatikana katika hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara (ICC) ambayo MwanaHALISI ina nakala yake.
  Imefahamika kuwa hata wakati wa kumpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (28 Novemba 2005) ya kusimamia biashara zake, kuingia ubia na kufanya shughuli zake nyingine, Dowans haikuwa na biashara yoyote Costa Rica au kokote duniani.

  ICC inasema katika hukumu yake kuwa wakati Rostam anapewa madaraka, Dowans inayodaiwa kuwa ya Costa Rica haikuwa na shughuli zozote wala ofisi isipokuwa Ubungo, jijini Dar es Salaam.

  Kampuni inayotaka kulipwa mabilioni ya shilingi na serikali ya Tanzania, “…haina mali yoyote isiyohamishika, magari wala haikuwa imesajiliwa kama mlipa kodi” nchini Costa Rica imeeleza hukumu hiyo.
  Aidha, Dowans hiyo haikuwa imewahi kufanya kazi nyingine yeyote, Costa Rica na, au duniani kwa jumla.

  Taarifa hii inayotokana na hukumu ya ICC, inasaidia kujenga shaka juu ya uhalali wa Dowans ya Costa Rica, mamlaka ya Rostam ya kuwakilisha kampuni hiyo na uhalali wa TANESCO/serikali kulipa kiasi chote inachodaiwa.
  Wakati huohuo ICC imebainisha kuwa wakati wa kusikiliza madai ya Dowans, mashahidi tisa na nyaraka karibu 3,000, zilionyesha kuwa Rostam alikuwa “mtu muhimu” katika suala lililopelekwa mahakamani.

  Mashahidi waliofika mahakamani hapo, ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Dowans Tanzania Ltd., Guy Picard na Henry Surtees, mhandisi wa ujenzi wa kampuni ya Caspian ambaye pia ni mfanyakazi wa Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd (DTL) kwa karibu mwaka mmoja. Kampuni Caspian inamilikiwa na Rostam.

  Wengine ni Stanley Munai, mhasibu aliyeajiriwa na DTL kama mdhibiti wa fedha na Johannes Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa kampuni ya Net Group Solution ya Afrika Kusini.

  Lottering, mkuu wa idara ya usambazaji umeme wa Net group Solution ndiye aliyetajwa na kampuni ya mawakili iliyotetea TANESCO – Rex Attorney – kwamba mahakama iliridhika kuwa alilazimishwa kuweka saini uhamishaji mkataba kutoka Richmond hadi Dowans.

  Kwa mujibu wa hukumu hiyo (uk. 8), ICC inaeleza ilivyokubaliana na kila ushahidi, isipokuwa ushahidi wa Henry Surtees ambaye ni mfanyakazi katika kampuni ya Rostam, Caspian Limited.

  Siku tatu zilizopita Rais Jakaya Kikwete alikana kufahamu wamiliki wa Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Limited. Kauli yake imekuja miaka mitano baada ya kukiri hadharani kuwa rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.

  Mashahidi wengine katika shauri hilo la madai Na. 15947/VRO kati ya TANESCO na makampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd., ni Subira Wandimba, mwanasheria wa TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura, mwenyekiti wa bodi ya TANESCO na Dk. Idris Rashid, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO.

  Mashahidi wengine ni Jamhuri Ngelime, mkurugenzi wa fedha wa TANESCO na Boniface Njombe, mhandisi mkuu wa miradi wa shirika hilo.
  “Jopo la majaji liliridhika kuwa mashahidi wote waliotoa ushahidi, walifanya hivyo kwa uaminifu na kwa kadri ya kile walichoweza kukikumbuka na ushahidi wao ni wa kuaminika,” inasema hukumu ya ICC.

  Tofauti pekee ilionekana katika ushahidi wa Bw. Surtees ambaye jopo linasema alionekana wazi kukwepa kujibu maswali kuhusiana na maslahi na umiliki wa kampuni ya Caspian Ltd., na Dowans Tanzania Limited (DHL) na pia kuhusiana na utata wa nafasi ya ushirika wa Bw. Rostam Aziz katika historia ya mgogoro huu.

  Mahakama inasema imeuchukua “ushahidi wake kwa tahadhari, kwa kuwa Bw. Surtees alikuwa pia anakwepa kueleza uhusiano wake na Dowans.”
  Katika toleo lililopita la gazeti hili, tulichapisha taarifa mbalimbali zinazomhusisha Rostam na Dowans/Richmond – kampuni iliyopewa mkataba kwa upendeleo, huku ikiwa haina fedha, utaalam wala historia ya kufua umeme. Makampuni hayo yalibadilishana mkataba tarehe 23 Desemba 2006 kinyume cha sheria za nchi.

  Hata hivyo, habari zinasema toleo la MwanaHALISI lililokuwa na taarifa hizo, lilihujumiwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa baadhi ya watu ambao hawajafahamika, kununua nakala nyingi na mara nyingi ili kuziondoa sokoni.
  Maeneo ambayo gazeti lilipatikana kwa shida kutokana na watu wachache kununua nakala nyingi, ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Iringa na Mbeya.

  Toleo hilo lilikuwa na taarifa juu ya mamlaka ambayo Rostam alipewa na Dowans. Hiyo ni pamoja na kuajiri mawakili, kudai, kushitaki na kupokea malipo yoyote ya fedha kwa niaba ya kampuni.

  Kazi nyingine ambazo Dowans ilimpa Rostam, ingawa yenyewe haikuwa na shughuli zozote, ni kufunga na kufungua akaunti za benki za kampuni hiyo na kununua au kuuza hisa za kampuni pale atakapoona inafaa.

  Nafasi ya Rostam katika “biashara” hii inamwezesha kudai, kufungua madai, kukazia hukumu, kutumia fedha kwa biashara, kuajiri washauri na maajenti kwa shughuli za kampuni.
  Mamlaka ya Rostam yanahusu pia kutetea kampuni, kujibu au kupinga hoja au hatua zozote kisheria zinazogusa kampuni katika biashara zake za sasa na hata za baadaye.

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, iwapo mahakama itaamua TANESCO ilipe Sh. 94 bilioni, ni Rostam atakayechukua malipo hayo na kupanga jinsi ya kuyatumia.
  Maelezo kwenye hati ya mamlaka yanasema Rostam ataendelea kuwa na mamlaka hayo hadi atakapopewa taarifa ya kuyasitisha.

  Pamoja na mamlaka ya Rostam kushitaki na kukazia hukumu ili kupata akitafutacho, wasuluhishi wa ICC wamekiri kuona kuwa alifanya ushawishi mkubwa katika kuhakikisha kampuni yake hiyo inapata zabuni ya kufua umeme nchini, nje ya utaratibu wa kisheria.

  Kwa mfano, wakati wa kesi hiyo, ilielezwa jinsi Rostam alivyotumia mamlaka yake ndani ya serikali kushawishi TANESCO kutoa zabuni ya kufua umeme kwa kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

  Rostam alijua, kwa sifa za kawaida za uchambuzi wa zabuni, Richmond isingeweza kupata zabuni hiyo ya kufua umeme mwaka 2006, imeeleza taarifa ya kampuni ya uwakili ya Rex Attorney iliyoitetea TANESCO.

  Bali, mahakama ya ICC inasema, “Bw. Rostam Aziz alikuwa kwenye nafasi ya ushawishi mkubwa juu ya kampuni ya Dowans, hata kama haijulikani alikuwa na maslahi yanayoeleweka katika makampuni hayo.”

  Hata hivyo, ICC imesema katika mazingira ya Dowans/Richmond na jinsi Rostam alivyonufaika binafsi, “…mahakama haiwezi kuchunguza.”

  Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliripoti mwanasheria maarufu, mbunge na naibu waziri wa Miundombinu, Dk. Harisson Mwakyembe akisema aliyeleta balaa la Dowans ni Rostam Aziz.
   
 2. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watanganyika wamepigwa na butwaa ha wasijue wapi pa kuanzia. Tumebaki kusononeka kwenye vijiwe vya kahawa, na kwenye meza za wauza magazeti na wapigarangi viatu. Watawala wamekuwa watwana dhidi ya watanzania masikini ambao kila kukicha wao wanatafuta mlo wa siku. Poleni sana.
   
 3. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Natamani tungefanya mabadiliko ya nguvu kama ya Egypt halafu tukatunga sheria maalum ya kumhukumu huyu mburushi na kumyongelea mbali. Balaa mkubwa huyu.
   
 4. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wamefanya na wanafanya makusudi kuhakikisha kuwa tunabaki hapo kwenye RED.
  It's very sad.
   
 5. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Tehetehetehe! Kwikwikwi! "MBURUSHI" it must be a complex means of describing "JANGILI". Umenikumbusha kipindi kidogo cha nyuma tulipotumia majina haya ikiwa ni pamoja na "mwarabu koko".
  Huyu jamaa ni "mercenary" kama tulivyowahi kusoma katika taarifa kadhaa, I've no doubt about this. Nyimbo zake ziko nyingi na wasaidizi wake wapo wengi. Mungu atatujalia tu tutaendelea kuwajua kama huyu bwana mdogo wa juzi anayemdai mzee Mengi fidia ya shilingi moja na hatima yao itafika. Kwani wamekomaa kama Hosni Mubarack wa Egypt? Hawawezi
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Wakati wa Komandoo(Salmin) kule zenji alikuwepo jamaa anaitwa Mohamed Raza, huyu naye alikuwa km rostam, kuna kipindi mpaka alikuwa anaisemea serikali, mfanyabiashara huyo sasa na sisi tuna Rostam sasa, lkn Raza sasa hivi hana mbele wala nyuma, hata huyu mwizi ikiisha miaka ya JK atafulia km Raza always lkn anatunyonya saaaana huyu KUPE mweupe, wananchi kwa nini tusiende kwenye biashara zake ttukachukua MALI ZETU? maana anatuibia kweupeeee na Mkwere anamchekea tuuuuuu
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  MI naona hizi Habari ni za marudio tu, hi habari inajulikana kwa muda mrefu sasa kuwa RA na kundi lake ndio wamiliki wa hiyo kitu Dowans
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ipo siku yake tu!
   
 9. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  SIRI imefichuka. Kampuni ya Dowans Holdings SA inayodaiwa kusajiliwa nchini Costa Rica, haikuwa na “biashara nyingine yeyote duniani” wakati ikimpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (Power of Attorney) ya kuiwakilisha nchini Tanzania.

  Hii ndiyo kampuni inayodai TANESCO Sh. 94 bilioni kwa kukatisha mkataba wake wa kufua umeme ilioupata kutoka kampuni hewa ya Richmond Development (LLC).

  Taarifa hizi zimepatikana katika hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Biashara (ICC) ambayo MwanaHALISI ina nakala yake.

  Imefahamika kuwa hata wakati wa kumpa Rostam Aziz mamlaka ya kisheria (28 Novemba 2005) ya kusimamia biashara zake, kuingia ubia na kufanya shughuli zake nyingine, Dowans haikuwa na biashara yoyote Costa Rica au kokote duniani.

  ICC inasema katika hukumu yake kuwa wakati Rostam anapewa madaraka, Dowans inayodaiwa kuwa ya Costa Rica haikuwa na shughuli zozote wala ofisi isipokuwa Ubungo, jijini Dar es Salaam.

  Kampuni inayotaka kulipwa mabilioni ya shilingi na serikali ya Tanzania, “…haina mali yoyote isiyohamishika, magari wala haikuwa imesajiliwa kama mlipa kodi” nchini Costa Rica imeeleza hukumu hiyo.

  Aidha, Dowans hiyo haikuwa imewahi kufanya kazi nyingine yeyote, Costa Rica na, au duniani kwa jumla.

  Taarifa hii inayotokana na hukumu ya ICC, inasaidia kujenga shaka juu ya uhalali wa Dowans ya Costa Rica, mamlaka ya Rostam ya kuwakilisha kampuni hiyo na uhalali wa TANESCO/serikali kulipa kiasi chote inachodaiwa.

  Wakati huohuo ICC imebainisha kuwa wakati wa kusikiliza madai ya Dowans, mashahidi tisa na nyaraka karibu 3,000, zilionyesha kuwa Rostam alikuwa “mtu muhimu” katika suala lililopelekwa mahakamani.

  Mashahidi waliofika mahakamani hapo, ni pamoja na mkurugenzi mtendaji wa Dowans Tanzania Ltd., Guy Picard na Henry Surtees, mhandisi wa ujenzi wa kampuni ya Caspian ambaye pia ni mfanyakazi wa Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd (DTL) kwa karibu mwaka mmoja. Kampuni Caspian inamilikiwa na Rostam.

  Wengine ni Stanley Munai, mhasibu aliyeajiriwa na DTL kama mdhibiti wa fedha na Johannes Lottering aliyekuwa mwajiriwa wa kampuni ya Net Group Solution ya Afrika Kusini.

  Lottering, mkuu wa idara ya usambazaji umeme wa Net group Solution ndiye aliyetajwa na kampuni ya mawakili iliyotetea TANESCO – Rex Attorney – kwamba mahakama iliridhika kuwa alilazimishwa kuweka saini uhamishaji mkataba kutoka Richmond hadi Dowans.

  Kwa mujibu wa hukumu hiyo (uk. 8), ICC inaeleza ilivyokubaliana na kila ushahidi, isipokuwa ushahidi wa Henry Surtees ambaye ni mfanyakazi katika kampuni ya Rostam, Caspian Limited.

  Siku tatu zilizopita Rais Jakaya Kikwete alikana kufahamu wamiliki wa Dowans Holding SA na Dowans Tanzania Limited. Kauli yake imekuja miaka mitano baada ya kukiri hadharani kuwa rafiki wa karibu wa Rostam Aziz.

  Mashahidi wengine katika shauri hilo la madai Na. 15947/VRO kati ya TANESCO na makampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd., ni Subira Wandimba, mwanasheria wa TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura, mwenyekiti wa bodi ya TANESCO na Dk. Idris Rashid, aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO.

  Mashahidi wengine ni Jamhuri Ngelime, mkurugenzi wa fedha wa TANESCO na Boniface Njombe, mhandisi mkuu wa miradi wa shirika hilo.

  “Jopo la majaji liliridhika kuwa mashahidi wote waliotoa ushahidi, walifanya hivyo kwa uaminifu na kwa kadri ya kile walichoweza kukikumbuka na ushahidi wao ni wa kuaminika,” inasema hukumu ya ICC.

  Tofauti pekee ilionekana katika ushahidi wa Bw. Surtees ambaye jopo linasema alionekana wazi kukwepa kujibu maswali kuhusiana na maslahi na umiliki wa kampuni ya Caspian Ltd., na Dowans Tanzania Limited (DHL) na pia kuhusiana na utata wa nafasi ya ushirika wa Bw. Rostam Aziz katika historia ya mgogoro huu.

  Mahakama inasema imeuchukua “ushahidi wake kwa tahadhari, kwa kuwa Bw. Surtees alikuwa pia anakwepa kueleza uhusiano wake na Dowans.”

  Katika toleo lililopita la gazeti hili, tulichapisha taarifa mbalimbali zinazomhusisha Rostam na Dowans/Richmond – kampuni iliyopewa mkataba kwa upendeleo, huku ikiwa haina fedha, utaalam wala historia ya kufua umeme. Makampuni hayo yalibadilishana mkataba tarehe 23 Desemba 2006 kinyume cha sheria za nchi.

  Hata hivyo, habari zinasema toleo la MwanaHALISI lililokuwa na taarifa hizo, lilihujumiwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa baadhi ya watu ambao hawajafahamika, kununua nakala nyingi na mara nyingi ili kuziondoa sokoni.

  Maeneo ambayo gazeti lilipatikana kwa shida kutokana na watu wachache kununua nakala nyingi, ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Iringa na Mbeya.

  Toleo hilo lilikuwa na taarifa juu ya mamlaka ambayo Rostam alipewa na Dowans. Hiyo ni pamoja na kuajiri mawakili, kudai, kushitaki na kupokea malipo yoyote ya fedha kwa niaba ya kampuni.

  Kazi nyingine ambazo Dowans ilimpa Rostam, ingawa yenyewe haikuwa na shughuli zozote, ni kufunga na kufungua akaunti za benki za kampuni hiyo na kununua au kuuza hisa za kampuni pale atakapoona inafaa.

  Nafasi ya Rostam katika “biashara” hii inamwezesha kudai, kufungua madai, kukazia hukumu, kutumia fedha kwa biashara, kuajiri washauri na maajenti kwa shughuli za kampuni.

  Mamlaka ya Rostam yanahusu pia kutetea kampuni, kujibu au kupinga hoja au hatua zozote kisheria zinazogusa kampuni katika biashara zake za sasa na hata za baadaye.

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, iwapo mahakama itaamua TANESCO ilipe Sh. 94 bilioni, ni Rostam atakayechukua malipo hayo na kupanga jinsi ya kuyatumia.

  Maelezo kwenye hati ya mamlaka yanasema Rostam ataendelea kuwa na mamlaka hayo hadi atakapopewa taarifa ya kuyasitisha.

  Pamoja na mamlaka ya Rostam kushitaki na kukazia hukumu ili kupata akitafutacho, wasuluhishi wa ICC wamekiri kuona kuwa alifanya ushawishi mkubwa katika kuhakikisha kampuni yake hiyo inapata zabuni ya kufua umeme nchini, nje ya utaratibu wa kisheria.

  Kwa mfano, wakati wa kesi hiyo, ilielezwa jinsi Rostam alivyotumia mamlaka yake ndani ya serikali kushawishi TANESCO kutoa zabuni ya kufua umeme kwa kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na sifa ya kufanya kazi hiyo.

  Rostam alijua, kwa sifa za kawaida za uchambuzi wa zabuni, Richmond isingeweza kupata zabuni hiyo ya kufua umeme mwaka 2006, imeeleza taarifa ya kampuni ya uwakili ya Rex Attorney iliyoitetea TANESCO.

  Bali, mahakama ya ICC inasema, “Bw. Rostam Aziz alikuwa kwenye nafasi ya ushawishi mkubwa juu ya kampuni ya Dowans, hata kama haijulikani alikuwa na maslahi yanayoeleweka katika makampuni hayo.”

  Hata hivyo, ICC imesema katika mazingira ya Dowans/Richmond na jinsi Rostam alivyonufaika binafsi, “…mahakama haiwezi kuchunguza.”

  Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliripoti mwanasheria maarufu, mbunge na naibu waziri wa Miundombinu, Dk. Harisson Mwakyembe akisema aliyeleta balaa la Dowans ni Rostam Aziz.

  Mwakyembe alinukuliwa akisema ndani ya mkutano wa wabunge wa CCM jijini Dar es Salaam, “…mnahangaika nini? Aliyetufikisha hapa ni mtu mmoja tu; anaitwa Rostam Aziz. Serikali ifanye kila linalowezekana kuhakikisha fedha hizi hazilipwi.”
   
 10. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duuh aisee sijui sasa Rostam atajifichia wapi...! Hivi bado yupo Tanzania?
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sasa hawa ICC mbona hawaeleweki? Ukisoma taarifa hii inaonyesha wazi kabisa jamaa walishagundua kuwa Dowans ni matapeli mbona wameshinda kesi? Au majaji nao walihongwa? Maana kesi yenyewe imefanyikia hapahapa Dar. Halafu mara ya kwanza walisema hukumu niTANESCO kulipa bilioni 185, ghafla ikawa bilioni 94. Naona kuna utapeli mwingi sana hapa, huenda hata hiyo ICC inayotajwa ikawa ya mfukoni.
   
 12. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna watu wanasema Tanzania kuna serikali! Tanzania kuna mafioso wananchi tuamke na kuwafukuza kama Misri.
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Very sad indeed

 14. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Hivi hizo Bil 94 tunalipa kwa kosa la kuvunja mkataba au tunadaiwa kwa kuwa tulitumia umeme wao bila kulipa? Maana mheshimiwa JK alieleza kuwa tumetumia umeme wao kwa miezi 9.

  Ningependa kwenda mbali zaidi, hivi wakati umeme unazalishwa nani anayenunua mafuta au gas ? maana nimesikia kule bungeni waziri akisema Serikali imenunua mafuta mazito kwa ajili ya kuwasha mitambo ya IPTL
   
 15. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Muda wote huu....tangia aanzwe kuhusishwa na haya madudu amejificha wapi !!!
   
 16. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakuu hebu tusibiri mahakama na wanaharakati wanaoisaidia nchi kukwapuliwa na mafioso watafanya nini na hao au ndio watapewa mgao kama wale walioenda kusikiliza na kutoa ushaidi ICC? ukiangalia ni wazi wamenusa arufu ya hela za mafioso ili kupindisha sheria.
   
 17. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  yupo kaka
   
 18. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bongolala kweli. Sijui lini tutaamka. Jamaa kama vile wametupulizia kaputi wala siyo nusu kaputi.
   
 19. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inawezekana Isee! Ktk kanuni za kesi za ICC huwa kunatakiwa kuwe na idha mediators mmoja (aliyechaguliwa na ICC wenyewe) au watatu (Aliyechaguliwa na ICC, aliyependekezwa na mlalamikaji na aliyependekezwa na mlalamikiwa) sasa hii yetu naona mediators wametajwa wawili tuu - kanuni imechakachuliwa/ au ndo wamechemsha!
   
 20. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yupo na hata kwenye sherehe za CCM wiki zilizopita aliudhuria na kwenye kikao cha wana CCM na mwakyembe mwishoni akamlipua kua anayetuletea matatizo yote CCM ni mtu mmoja anayeitwa Rostam
   
Loading...