Rostam auza hisa zake Mwananchi

Hakuna kanuni iliyovunjwa sema huyo anayetaka majina ya watu yaondolewe ndio sio mtu huru
 
Kama kuna mada halafu watu hawataki kujadili nimelazimika kutoa maoni ya sehemu zingine nayo muone kama mlikuwa hamjui nini kinaendelea muweze kuwa na picha kidogo

ni kwa faida ya jukwaa zima

pole sana wewe usiependa dunia mduara
 
Hakika hata mimi naungana na WAJINGA hayo magazeti yanayomilikiwa na RA ni lazima yasusiwe kununuliwa,najua RA kwa wakati huu anahitaji mno Media kuweka sawa mabo yake nakubaliana pia na Mheshimiwa MPITA NJIA hawezi kuuza hizo hisa sana sana anatka kujitanua zaidi.MUNGU TUONYESHE NJIA YA KWELI NA WACHUKUE MMOJA MMOJA HAO MAFISADI.
 
Heshima kwenu Wanazuoni, Bila shaka Erick Kajitahidi sana kueleza kuhusus suala la hisa na nafasi za wanahisa katika kutoa maamuzi ndani ya kampuni, kuna tofauti kati ya namna Mwananchi communication inavyoendeshwa na IPP media na mara nyingi maamuzi ya kulindana hutegemea pia nani ana hisa nyingi zaidi! rejea Habari corporation kabla haijawa New Habari, namna gazeti kama Rai lilivyokuwa na lilivyo sasa. Naona kuna mawazo ambayo hayajitokezi vyema hapa lakini nadhani wachangiaji wengi wanamwelekeo huo, nalo ni wazo zima la kuwa na mabepari wazalendo, national bourgeoisie as opposed to petty bourgeoisie wanaoishia kuwa vibaraka wa wenye mali, sasa ni kosa la nani? tulipokubali kuwa mabepari bila kujiandaa na kuingia kwenye mchezo ambao hatujui hata taratibu zake tulitegemea nini? kuwa kichwa cha mwendawazimu bila shaka! tukawatafute akina Maksimo, Mkapa aliwahi kumleta mmoja majuzi enzi zake! lakini naona somo lake la kuifufua mitaji mfu bado halijaeleweka, na Mzee wa tabasamu hata wakati wa masikitiko naye aliwahi mleta Maksimo wa kuwafanya masikini wakopesheke! lakini hatujui iliishia wapi? nchi ya majaribio na mikakati! nadhani hiyo ina refrect wananchi wake walivyo pia! bila shaka tunafanya majaribio kibao hata kwenye maisha binafsi! Tuache kuwa watu wa hisia hisia, emotions zitatumaliza! Haya sasa mumeambiwa na Erick hata hao Wakenya ni washika dau tu mwenyewe haswa ni Aga khani foundation! who is Aga khan? haya hata hapa kwetu Aga khan ana interest nyingi tu! tatizo letu hata utafiti kidogo wa kujisomea hatufanyi matokeo yake kila kitu kwetu ni kipya! kuna namna ambayo uwekezaji unaweza fanyika ukawa ni faida kwetu binafsi sina tatizo na uwekezaji wa Aga Khan kwani tofauti na wengineo walau Aga khan foundation unaweza sema wanachokifanya kina onekana, nchi kujengwa na wawekezaji nina tatizo na hii dhana pia, sidhani kama style inayofanyika hapa Marekani wanaweza kuruhusu ifanyike kwao na ndio maana makampuni mengi ya Kimarekani yamekimbilia Mexico! ama yanaelekea katika maeneo nje ya marekani kama China na nchi za dunia ya tatu kama Tanzania ambako unaingia na begi lako na vijisenti vya kudanganyia then ukirudi Eapoti ni mmoja wapo katika kundi la akina Bill Gate! Kuna haja ya kubadilika na kubadili mtizamo katika masuala mengi ikiwemo namna ya kujipanga! vinginevyo tutaendelea kushuhudia rasilimali zetu zikihamishwa huku wenyewe tukiangalia na kulipuka kwa hisia tu! moja ya maeneo ndiyo haya ya sheria zetu! maana twaweza sema kuna sheria lakini kama sheria zenyewe ni kama hii ya madini tuliyokuwa nayo Mungu aepushie mbali! Sheria ya uwekezaji nk ni maeneo nyeti tunayopaswa kuyatazama kwa makini ilikuepuka kuzidiwa kete na wajanja wachache, mabepari sio wajomba zetu, hawa ni wafanyabiashara haswa na msukumo wao mkubwa ni faida! wao hawaui Ma Albino kama wenzetu wengine wafanyavyo! wao hucheza na sheria na mikataba ukisinzia umekwisha! Chonde chonde Amkeni! Baha.
 
Kama kuna mada halafu watu hawataki kujadili nimelazimika kutoa maoni ya sehemu zingine nayo muone kama mlikuwa hamjui nini kinaendelea muweze kuwa na picha kidogo

ni kwa faida ya jukwaa zima

pole sana wewe usiependa dunia mduara

JF ni jukwaa huru na huwezi kuwalazimisha watu wachangie. Ukiona watu hawachangii, ujuwe hawana cha kuchangia. katika kuchangia, watu wanaofikiri kwa kina wananyamaza kimya wanapoona hawana cha maana cha kuchangia. katika hali kama hiyo, huwezi kutulazimisha hapa JF, ambako ni huru, kutuhamishia mawazo ya watu wengine kwenye forum nyingine. Kwa nini usituache tuchangie mawazo ya hapa hapa JF? Kama unadhani huko unakopata maoni haya unakufahamu wewe tu, nakupa pole sana, wenzako walishafika huko kabla wewe hujakujua.
Kuhamisha maoni ya watu kama ulivyofganya, na kuyabandika kwa jina lako, inaitwa plagiarism kwa kimombo na ni kosa kisheria. usitake kuiingiza JF kwenye matatizo. hao waliochangia huko kwingine wanaifahamu JF na kama wangetaka kuchangia hapa wala wasingesitaa kufanya hivyo kwa sababu hakuna anayezuiliwa hapa
 
Angalia chini utaona kuna majina ya wenyewe sio jina langu kuna baha angalia usiwe mzushi
 
Kama mali za mafisadi wa EPA zilikamatwa na kama RA alitajwa tajwa katika EPA, na kama aliona asije kujikuta anakamatiwa mali zake hata kama anaamini hahusiki, kwa hiyo basi nataka kuamini ama napenda kusahihishwa kama uuzaji, uhamishaji au ubadilishaji wa hiza za Mwananchi unaweza kuwa na uhusiano na uhamishaji/uuzaji wa hisa za RA katika Vodacom zilizohamishiwa Afrika Kusini
 
Shy ni mimic na ambaye taarifa zake ni za kutokuaminika.

jadilini kwa umakini wa hali ya juu
 
Bwana Rostam Aziz, ambaye amejikita kuiimarisha kampuni ya News Habari Corp, ameuza hisa alizokuwa anazishikilia katika kampuni ya Mwananchi Communication Limited. Pia rafiki yak wa karibu, Mzee Ferdinand Ruhinda, naye amuza hisa zake kwenye kampuni hiyo.
 
hizo aliuza toka mwezi wa 7 mwaka huu mkuu mpita njia ila sasa hivi nimeona watu wengi sana wanauza hisa zao katika kampuni kumbwa

nasikia mosha yule wa akiba bank nae ameuza hisa zake katika kampuni ya interconsult pamoja na akiba bank yaani hizi epa hizi kiboko
 
Hili Taifa letu bwana! Rostam Aziz akikimbia nchi taifa hili halitatawalika.

Na hiyo kampuni ya Mwananchi ina maana wakenya wanamiliki asilimia ngapi ya hisa zote?

Sisi tunachotaka ni chenji yetu tu,auze arudishe hela yetu tena na interest
 
lets find out nani wamenunua?. Kuna wakati shares za Afrcan Media Group ziliuzwa kwa Multi Choice. Mengi akapinga deal ikagomba. Kunawakati the Nations Group walitaka kununua Channel Ten na Mwananchi 100%. Msajili wa makampuni akagoma. Hii take over isije ikawa ndiyo ya 100% stake halafu game likawa kama Kibo Breweries.
 
Hapa kuna haja ya kufuatilia,maanke tunajikuta tunasalimisha uhuru wetu hata kwa mabepari uchwara
 
Labda anatafuta cash ya kujiwekea dhamana pale kisutu ili asilale keko kama wenzake. Just kidding!!
 
Na Mwandishi Wetu

BODI ya wakurugenzi ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), ambaoni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen, imetangaza uteuzi wa wakurugenzi huru wanne.

Wakurugenzi hao ni Profesa Palamagamba Kabudi, Zuhura Sinare Muro, Mohammed Rweyemamu na Abdulsultan Jamal. Wote wamejiunga na bodi ya MCL kuanzia jana na wote kwa ujumla historia yao kielimu inahusisha uandishi wa habari, uhandisi, rasilimali watu na masuala ya biashara.

Kuteuliwa kwao ni kutengeneza mfumo mpya wa kampuni baada kujiuzulu kwa Rostam Aziz na Balozi Ferdinand Ruhinda, ambao wameuza hisa zao kwa kampuni ya Nation Media Group.

Wengine ambao wamejiuzulu kwenye bodi ya MCL ni Wangethi Mwangi na James C. Kinyua wote wakitokea kampuni ya Nation Media Group.

Kampuni mama ya MCL ambayo ni kampuni tanzu ya Nation Media Group, inao wakurugenzi wawili katika bodi hiyo ambao ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), Linus Gitahi na Mkurugenzi wa Fedha, Stephen Gitagama, kati ya wakurugenzi saba wa bodi ya MCL.

Akitangaza uteuzi huo jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa bodi ya MCL, Ali Mufuruki alisema: “Tunafurahi kuwapata Watanzania waliojitolea kujiunga na bodi ya Mwananchi Communications. Limekuwa lengo letu kuunda bodi ya wakurugenzi ambayo ni yenye, uhuru, heshima na uwezo wa kimawazo, jinsia na historia yenye utaalamu.”

Aliongeza kusema: “Kuwa na Watanzania watano ambao ni wakurugenzi huru, ikiwa ni pamoja na mwenyekiti na wakurugenzi wawili kutoka Kenya, Mwananchi ina mrengo wa juu katika katika taaluma na biashara ya habari, kitu ambacho ni habari nzuri kwetu.”

Prof. Kabudi, 51, ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mwandishi wa habari wa zamani ambaye pia ni mmoja wa wakurugenzi wa Bodi ya Baraza la Mazingira Tanzania (NEMC) na pia mjumbe wa bodi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC). Ameandika zaidi ya vitabu 50 na taarifa za utafiti mbalimbali na ni mwenye ujuzi mkubwa katika ushauri.

Muro, 47, ana utaalamu wa uongozi wa rasilimali watu, na ni mwenye ujuzi mkubwa katika biashara za ndani, siasa ya jamii na uchumi wa mazingira kwa Tanzania na nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alikuwa mkuu wa kitengo cha uajiri cha kampuni ya simu ya Celtel, ambayo imebadilishwa jina na kuwa Zain, na pia ni mkurugenzi na katibu wa mfuko wa uongozi wa Afrika katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rweyemamu, 50, ni mshauri wa masuala ya uhandisi wa kujitegemea na ana shahada ya uzamili ya sayansi ya uhandisi wa mitambo. Hivi sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni za MEX ambazo zinashughulika na kukodisha vifaa vya ujenzi.

Mkurugenzi mpya wa nne ni Jamal, ambaye ni mfanyabiashara wa siku nyingi ambaye amehusika katika makampuni mbalimbali. Anahusika na biashara za samani, ujenzi wa nyumba na anahusika sana katika masuala ya jamii.

MCL ni kampuni dada ya Nation Media Group, ambayo makao makuu yake yako jijini Nairobi nchini Kenya.
 
Rostam Aziz ajiuzulu, Mwananchi yatangazawa bodi mpya

Rostam Aziz, ambaye amejitoa katika bodi ya wakurugenzi wa Mwananchi Communication Ltd (MCL) baada ya kuuza hisa zake zote

source :Mwananchi Tanzania News Paper
 
Back
Top Bottom