Rostam auza hisa zake Mwananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam auza hisa zake Mwananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yona F. Maro, Aug 26, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 26, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kampuni ya Mwananchi communication iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya watanzania na wakenya sasa inamilikiwa kwa asilimia 100 na wakenya .

  Habari za kuaminika toka kwa watu mbali mbali waliomo ndani ya kampuni hiyo zinasema umiliki ulikamilika wiki iliyopita , umiliki huo kwa sasa uko chini ya National Media Group baada ya kukamilisha malipo ya hisa kutoka kwa wamiliki wazalendo .

  Mmiliki mzalendo ambaye pia ni mbunge wa igunga mhe rostam aziz alilipwa kiasi cha shilingi mil 750 wiki iliyopita kuiwezesha national media group inayomilikiwa kwa kiasi Fulani na agha khan foundation kumiliki kampuni hiyo

  Mwananchi communication pia imepata piga baada ya kuondokewa na baadhi ya waandishi wake 15 katika kipindi hicho cha wiki moja kutokana na sababu za kimasilahi , waandishi hao wamejiunga na vyombo mbali mbali vya habari jijini dare s salaam .

  Baadhi ya maofisa wa serikali wanasema hawakubaliani na uamuzi wa kuwepo umiliki huu lakini haijulikani walikuwa wapi wakati rostam anakabidhi hizo hisa kwa kampuni ya national media au kama kweli wako makini katika kufuatilia umiliki wa kampuni za kigeni hapa nchini , inatia mashaka kuhusu kuwajibika kwao huku .

  Kulingana na sheria ya vyombo vya habari , hairuhusiwi chombo chochote kumilikiwa kwa asilimia 100 na kampuni au muwekezaji wowote kutoka nje , umiliki au ubia unatakiwa usizidi asilimia 49 wachambuzi mbali mbali wa mambo wanasema sasa mwananchi imerudi kule kule ilipotoka nyumbani kwao

  Na sasa wale wakenya waliofukuzwa kazi wakati ile kwa kufanya kazi na chombo hicho bila vibali vya uhakika wataweza kurudi tena na kuongezwa wengine zaidi

  Gazeti la mwananchi ndio gazeti linaloongoza kwa mauzo kwa sasa nchini Tanzania kwa mwagazeti ya Kiswahili na kwa habari za michezo gazeti la mwanaspoti ndio linaongoza kwa mauzo .
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huenda hao wakurugenzi wa Mwananchi wameshakamilisha taratibu za kuomba uraia na sasa ni Raia kamili wa Tanzania.

  Rupert Murdoch alifanya hivyo ili amiliki media USA.
   
 3. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #3
  Aug 26, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Nadhani wameona RA anakuwa na conflict of interest kwenye story nyingi za maana, hasa scandals. Inawezekana hata fununu kuwa sakina aliondoka ni kwa sababu hizo hizo (kubanwa kati ya kumlinda RA au kutekeleza wajibu kwa kusema ukweli).
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Inaniwea vigumu sana kuamini kuwa watu makini kama Nation Media wanaweza kukubali kununua asilimia 100 ya hiza za media house Tanzania wakati wanajua kuwa sheria inakata hivyo
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Wanajuaa sana kuchez a na doc na kupindisha ukweli..maana wana washauri wazoefu na wanasheria piaa...wameenea kila idara ujue...so kuuza hisa zote inawezekana ...tutafute ukweli tujue how........
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Taarifa nilizonazo mimi ni kuwa Rostam amenunua hisa 20 za mzee Ruhinda. Kwa hiyo, Rostam anamiliki asilimia 40 ya hisa za Mwananchi kwa sababu awali alikuwa na asilimia 20. NMG wanamiliki asilimia 60.
  Anachokifanya RA ni kushinikiza ili baadhi ya matakwa yaliyomo kwenye sera ya habari ya habari yaingizwe kwenye sheria mpya ya habari itakayopelekwa Bungeni. Kikubwa anachokitaka katika hilo ni ile kipengelea kinachotaka wageni wasilimiki zaidi ya asilimia 49 ya hisa kwenye makampuni ya habari. Anaamini kuwa akifanya hivyo, itawalazimu NMG kuuza asilimia 11 ya hisa zao, na si ajabu akawa anazivizia na hizo au auamtumia mtu mwingine kuzinunua ili awe na majority stake kwenye kampuni hiyo
   
 7. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #7
  Aug 26, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nakuomba uverify kwa sources wako validity ya hii info...kwa kuwa hata mimi info niliyonayo inafanana sana na ya Shy, na imetoka kwa jamaa wa NMG kwenyewe japo siyo official. Sure Badala ya kuuza hisa awe amenunua?
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa mtu anayefahamu ambitions za RA, huwezi kuamini kuwa katika wakati huu anaweza kuuza hisa zake kwenye strong media company kama Mwananchi
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama anaweza kuuza hisa kwenye gazeti ambalo linapata faida kubwa kama zilivyo hapa chini kwani unaweza kujionea mwenyewe.

  Source;NMG.


  Advertising Revenues 75%
  Circulation revenues 21%
  Operating Profits 72%
  Mwananchi Communications
  Highlights
  �� Management restructure
  has yielded significant
  improvements in the
  year
  �� Mwananchi relaunch in
  July
  �� Prospects looking good
   
 10. w

  wajinga Senior Member

  #10
  Aug 26, 2008
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania acheni kununua magazeti hayo.
   
 11. King Zenji

  King Zenji Senior Member

  #11
  Aug 26, 2008
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ahh kwa nn sasa tuache kununua wakati jamaa wanaweza ANGALAU,Manake hizo media nyengine ndo KIMEO kwelikweli.
   
 12. L

  LazaroSMtindi Senior Member

  #12
  Aug 27, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unachosema ni sahihi. Azma kuu ya RA ni kutawala public opinion Tanzania kupitia vyombo vyake vya habari. Anahaha kupata Wabunge mamluki wa kutosha, Serukamba type, kusimama bungeni kidete kutaka "wazalendo" wawe na hisa zaidi kwenye kila chombo cha habari. RA naye anajiona "mzalendo" maana mliisha mbatiza kwa kumpa nafasi nyeti katika chama tawala ya "Mweka Hazina wa Taifa"! Ama kweli Nyerere angefufuka leo, angetamani kurejea ardhini haraka sana!

  Himaya ya RA sasa ni magazeti yafuatayo: RAI, MTANZANIA, DIMBA, THE AFRICAN, TAZAMA na sasa ameongeza mengine kutokana na Karamagi na Lowassa ku-chip in pesa: AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA na UMMA. Nimeona maombi yao ya kundi hili kuanzisha Radio na TV Station mapema mwaka kesho. Yote haya ni kwa ajili ya kumsafisha Lowassa na Rostam kuwa watu wasafi na kumfungulia njia Lowassa ya kugombea Urais mwaka 2010 na RA kuwa Waziri wake wa Fedha! Msalie Mtume!
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ina maana hawatampa muungwana awamu ya pili?
   
 14. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Swali la msingi. Hako pamoja?
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Hello Makamaradi,Duuh..hi habari ni ya kweli? kama ni kweli basi Tanzania kweli kuna mengi yanaendelea chini ya kapeti ambayo ni kasheshe kubwa sana kwa jamii. 1. kweli Rostam alikuwa anamiliki shares pale mwananchi communications?2.Kweli shares zote jamaa wakenya wamebeba?

  MICHAEL DALALI
   
 16. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #16
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ndugu wazalendo, Ningependa kufahamu zaidi kuhusu swala la Rostam kuwa na share ndani ya kampuni ya Communication. Nina maswali kidogo juu yan hilo 1. Je ni kweli ameambiwa arudishe hisa au yeye mwenyewe ameamua kurudisha baada ya kuona kazi yake imemalizika has baada ya Richmondi kuanza kusahaulika? 2. Rostam ni mbunge na sina wasiwasi juu ya uewlewa wake kuhusu sheria na kanuni za usajiri wa makampuni ukizingatia CASPIAN, RICHMOND,DOWANS, HABARI Corporation ni makampuni ambayop aidha anayamiliki au anahusiana nayo kwa karibu. 3. Ukizingatia maswali haya unafikiri ni kwli kwamba atakuwa amenyang'anywa hisa au wmerudisha mwenyewe kwa sababu zake binafs na ndiyo maana amaeamua kuwa kimya? Naomba kuwasilisha na siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli. Regards, Vincent
   
 17. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #17
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ndugu Wanazuoni,


  Mimi si msemaji wa kampuni ya mwananchi ila kama mfanyakazi wa mwananchi nimeona ni vema nikitoa maoni yangu kuhusu mjadala huu. Maoni haya ni ya kwangu binafsi,hayana uhusiano wowote uongozi na kampuni ya Mwananchi. Article ya kuhusu Mwananchi inasikitisha maana mwandishi wake hakufanya utafiti wa kutosha, na huyo mtu angeachiwa gazeti aliongoze kwa article za staili hiyo, angefungwa kutokana na wingi wa kesi. Sheria ya vyombo vya habari sivyo inavyosema ila serikali iko mbioni kuibalisha ili wazawa wamili hisa zaidi. NAFIKIRI KAMA WANAZUONI WOTE TUNAVYOJUA"NO RESEARCH, NO RIGHT TO SPEAK". Kama leo tungepiga kura kutafuta gazeti huru nchi hii, nafikiri matokeo yangetupa ukweli.

  Nafikiri kuna tatizo moja kuwa baadhi ya mambo yaliyosemwa na baadhi ya wachangiaji kaktika mjadala hayakufanyiwa utafiti wa kutosha pia ndo maana nikafikiri naweza kutoa maoni yangu juu ya hili. Kwanza kabisa Mwananchi Communications si ya wakenya, ni sehemu ya Nation Media Group ya Kenya ambayo Aga Khan ambaye ni principal shareholder lakini pia kuna wakenya ambao in washika dau. Kwa Tanzania, kuna washika wengine ni wazawa kama kama sheria za uwekezaji zinavyosema. Rostam Aziz ni mshika dau kama washika dau wengine katika kampuni ya Mwananchi.

  Ila kwasababu Nation (Aga khan) anamiliki shares nyingi, maana yake ni kwamba management iko mikononi mwake. Na machapisho yote yanakuwa na editorial huru.

  Haina maana eti kwasababu Rostam ni shareholder basi eti lazima magazeti 'yamwandike vizuri' ata kama amefanya makosa. Sifikiri kama ni kweli kwasababu ni kinyume na maadili ya vyombo vya habari na uhandishi wa habari. Pia, si kwamba watu wanaamka asubuhi na kuamua mambo kiholela. Hapana! Kuna policy Inayotoa mwongozo juu ya namna ya kufanya mambo mbalimbali kila siku.

  Mimi binafsi mwisho, sina matatizo na Wakenya kuwekeza hapa nchini. Nafikiri sisi watanzania tumekuwa ambazo nafikiri ni za kihistoria zaidi kuwa wakenya si watu wazuri, na nafikiri ndo maana tunaogopa ata kuingia kwenye East Africa Common market, juzi tumekataa kusaini Free Movement of Labour Protocal n.k Tunafikiria kuwa tunaweza kufanya mambo yetu kama kisiwa na hatuwaitaji watu wengine, jambo ambalo si kweli. Kama alivyosema mjasirialimali maarufu nchini, Ali Mufuruki, tatizo letu kubwa ni mindset na tuna sababu za kutufanya tubadilike. Bwana Mfuruki alitoa mfano wa nchi kama Marekani na Dubai, ambazo Watanzania walio wengi wanaota kwenda kuishi na kufanya kazi, kuwa hazikujengwa na wazawa peke yao bali walishirikiana na wageni. Zaidi ya asilimia 60 ya labour Labour force ya Dubai ni kutoka nchi za kigeni.

  Kama alivyosema mwandishi maarufu wa Marekani, Thomas Fredman, katika kitabu cha THE WORLD IS FLAT, hivi sasa kuna wachina zaidi ya milioni wanaofikiria kuja hapa nchi kufanya kazi kama ya Yona Maro, Bwana Mbogela na wengine. Mfano mwengine ni Rwanda amabayo juzi watu walikuwa wanachinjana lakini leo ni hub ya ICT na economic advisors na watendaji wakubwa waliobadilisha nchi hiyo ni wageni wakishirikia na wazawa. Tuongelee mtu kama Steve Jobs, wa Apple computers, kiwanda chake cha kutengeza computers kipo Asia (out sourcing) na mifano mingine mingi.

  Kuhusu wawekezaji kwenye vyombo vya habari, kama mwandishi wa habari, sioni tatizo wawekezaji wa kigeni kuwekeza kwenye media, kama vyombo hivyo vitakuwa objective na kufanya kazi zao vuzuri. Leo Rupert Mudoch ambaye ni mmarekani anamiliki vyombo vyenye nguvu marekani na nchi nyingine na juzi tumeona amemu-endorse Obama. Hivi sasa anakamilisha utaratibu wa kuwekeza nchini China. Kwahiyo, mimi sina matatizo na Wakenya wala Rostam kuwekeza au kufanya kazi Mwananchi kama wanafanya hivyo kihalali na wanafuata sheria na taratibu za nchi. Kama kutakuwepo na vielelezo kuwa mshika dau yoyote kwenye kampuni ya Mwananchi ni fisadi, tutamwanika. Ndo maana Magazeti ya Mwananchi comm. Yalikuwa mstari wa mbele ku-report kasheshe ya Rostam bungeni. Wote tunajua!!!!

  Naomba kuwakilisha.

  ERICK KABENDERA
   
 18. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ok goood ndiyo maana nilikuwa najiuliza what hapen to sis askina kabakia na cheo moja tu pale kwennye talk show ya mzee simbeye.
   
 19. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu, kama kweli wewe ni mtu makini basi ujadili kwa uangalifu hilo tatizo, usifuate maneno ya Mufuruki na wengine kuwa tatizo la Watanzania ni mindset...haya mambo ya Free Movement of Labour yamewekwa wazi kwenye thread yake, na kila inachohitaji Tanzania kiko wazi na kinaeleweka nenda usome kisha useme kipi kibaya.

  Wakenya wanapiga ngoma, watanzania mcheze...mkitaka kupiga yenu wao wacheze, wanalalamika kuwa Tanzanians are antifederation...hii inachosha! Acheni bongo zifanye kazi, badala ya kuacha tu mambo yafanyike kwa kufuata upepo.

  Haiingii akilini kusema Tanzania haitaki Common market wakati ilisaini EAC Treaty. bali inataka kila hatua inayopigwa basi iwe na manufaa kwa pande zote. Unagalifu huu ndiyo mnaoita mind set? After all, kuna ubaya gani kujadili mambo kwa kina badala ya kufuata popular noise?
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii imekaje mods? naona Shy kaanzisha thread, halafu anachukua maoni ya watu wengine anayapost kwa jila lake kwa majina halisi ya watu hao. Je, kuna concert ya hao watu maoni yao kuwa posted hapa kwa majina yao halisi?
   
Loading...