Elections 2010 Rostam au Mramba au Lowassa au Chenge wakiomba kujiunga na CHADEMA

Uswe

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,204
626
wana JF,

nimejiuliza hili swali nimekosa jibu, nikaona si mbaya wacha nilisogeze sebuleni, kama inatokea mmoja kati ya watu waliothibitika kwa ufisadi akaomba uanachama wa chama chetu (CHADEMA) nini cha kufanya? kuna vetting yeyote kabla ya mwanachama kukubaliwa? wakati nachukua kadi yangu nimepewa straight, nikajiuliza hivi mafisadi si wanaweza kuja huku kutafuta hifadhi kama walivofanya kwa ccm, kwa sababu mwanzoni CCM kilikuwa chama wakulima na wafanyakazi lakini badae kikapokea mafisadi na ndo walokiharibu, sasa sisi firewalls zetu ziko imara kiasi gani?
 
Kuwa mwanachama na kuongoza ni vitu viwili tofauti, kwanza mtu kama Mramba au Rosta au Chenge akiisoma vizuri ile kadi dhamira yake itamshtaki kujiunga nayo. Vinginevyo kama mtanzania yeyote anayohaki ya kujiunga chama chochote cha siasa ambacho kimesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya jamhuri ya muungano wa kinafiki wa Tanzania.
 
Mimi nadhani kama Chadema watakuwa kind enough wataruhusiwa kuingilia mlango wa kutokea gerezani!!!!!!! baada ya kumaliza kifungo kwa makosa ya ufisadi!!
 
Mimi nadhani kama Chadema watakuwa kind enough wataruhusiwa kuingilia mlango wa kutokea gerezani!!!!!!! baada ya kumaliza kifungo kwa makosa ya ufisadi!!

Wanaweza kujiunga na Chadema kwa kufuata utaratibu ufuatao
1) Kutubu ufisadi wao wote
2) Kurudisha mali zote walizoiba serikalini
3) Kuahidi kuwa hawatarudia ufisadi wao

Wakishapokelewa hatua zifuatazo zitachukuliwa:
1) Watawekwa chini ya makamanda wa Chadema kwa Miaka mitatu mfululizo
2) Hawataruhusiwa kugombea madaraka kwa miaka 6

Baaday ya hapo watakuwa wanachama huru
 
mi jamani mnanichosha na hizi assumptions zenu nyie acheni tu ..khaaaa yaani mramba ajiunge CHADEMA???mwee
 
Wanaweza kujiunga na Chadema kwa kufuata utaratibu ufuatao
1) Kutubu ufisadi wao wote
2) Kurudisha mali zote walizoiba serikalini
3) Kuahidi kuwa hawatarudia ufisadi wao

Wakishapokelewa hatua zifuatazo zitachukuliwa:
1) Watawekwa chini ya makamanda wa Chadema kwa Miaka mitatu mfululizo
2) Hawataruhusiwa kugombea madaraka kwa miaka 6

Baaday ya hapo watakuwa wanachama huru

Kosa kubwa ni kwamba Chadema hawana Makamanda au tuseme wamefurahi kuongeza wabunge na sasa wanakwenda likizo kulala mpaka 2015, ukweli Chadema kama itachukulia umuhimu wa kuanza kujipanga hivi sasa na kuwa na makada wao mikoani, Wilayani na vijijini haki ya mungu 2015 wanamvua nguo CCM mchana kweupeeeee kwani waTz walivyochoka na usanii hawatachagua tena usanii wa hawa jamaaa, wengi waliochagua Chadema hawakuwa wanachama wa Chadema bali walifuata Nondo zilizokuwa zinamwagwa na Dr wa ukweli, Dr wa Phd, Dr wa kung'oa ufisadi, Dr wa walala hoi waleee kama mtawakumbuka 70% waliotajwa na JK kwamba ni fuata upepo na kweli wamemhakikishia kuwa upepo ukielekea mashariki na wao hukohuko hawaangaliii makunyanzi ya mtu, kofia, fulana, wala khanga zao, nilifurahi sana pale Mwanza vijana walivyokuwa wanaweka shinikizo la kutangazwa mshindi kwani pia kulikuwa na baadhi ya askari waliokuwa wakitoa signal za chadema lakini kwa kificho ili mabosi wao wasione madole mawili alama ya ushindi ndipo nikajua kuwa CCM wamekwishney na 2015 wasifikiri askari watazuia vijana wa chadema kwani na hao askari nao choka mbaya, wamepigika kama mimi na wewe, kila la kheri Chadema wangu
 
Mimi kwanza nashauri wawekwe ndani Segerea halafu wakitoka tuwafikirie kwakua hata huko walikotoka ndani ya CCM wamekishakisanii chama chao!:A S angry:
 
kweli maana watakuwa wameshatoka kule,lakini tatizo ni je wote wameisha? je wajua kuwa kuna mafisadi wengi tu ambao majina yao hayako popular ndani ya chichiemu?mi nadhani njia mbabdala ni kuhama tu nchi:tape:
Mimi nahamia CCM
 
Soma nyuma ya kadi yako ya Chadema utapata jibu.

hayo ni maneno tu hata kwenye kuta yapo kwani hao ccm hawana maneno kwenye kadi zao? mbona kwenye kadi nyuma hakuandikwi kuwa ukiwa hawara/mke/mkwe na jamaa wa karibu wa viongozi wa juu chadema utapitishwa viti maalumu?

Kwahiyo maneno nyuma ya kadi yasikubabaishe............
 
Kosa kubwa ni kwamba Chadema hawana Makamanda au tuseme wamefurahi kuongeza wabunge na sasa wanakwenda likizo kulala mpaka 2015, ukweli Chadema kama itachukulia umuhimu wa kuanza kujipanga hivi sasa na kuwa na makada wao mikoani, Wilayani na vijijini haki ya mungu 2015 wanamvua nguo CCM mchana kweupeeeee kwani waTz walivyochoka na usanii hawatachagua tena usanii wa hawa jamaaa, wengi waliochagua Chadema hawakuwa wanachama wa Chadema bali walifuata Nondo zilizokuwa zinamwagwa na Dr wa ukweli, Dr wa Phd, Dr wa kung'oa ufisadi, Dr wa walala hoi waleee kama mtawakumbuka 70% waliotajwa na JK kwamba ni fuata upepo na kweli wamemhakikishia kuwa upepo ukielekea mashariki na wao hukohuko hawaangaliii makunyanzi ya mtu, kofia, fulana, wala khanga zao, nilifurahi sana pale Mwanza vijana walivyokuwa wanaweka shinikizo la kutangazwa mshindi kwani pia kulikuwa na baadhi ya askari waliokuwa wakitoa signal za chadema lakini kwa kificho ili mabosi wao wasione madole mawili alama ya ushindi ndipo nikajua kuwa CCM wamekwishney na 2015 wasifikiri askari watazuia vijana wa chadema kwani na hao askari nao choka mbaya, wamepigika kama mimi na wewe, kila la kheri Chadema wangu
Broda ushauri wako mzuri, lakini hiyo kwenye rangi umepata wapi mwenzetu?, mi sijasikia imetolewa lini!
 
Back
Top Bottom