Rostam atingisha mkutano wa hadhara igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam atingisha mkutano wa hadhara igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fisadi Mtoto, May 22, 2009.

 1. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Leo mheshimiwa Rostam kapokelewa kwa shangwe kubwa na msululu mrefu wa wapiga kura wake kwenye uwanja wa samora mjini Igunga,baskeli pikipiki pamoja na maelfu ya wakazi walijumuika kwenye mapokezi hayo....kisha aliwahitubia akichanganya lugha ya kisukuma na kiswahili pamoja na mambo mengine ya maendeleo aliwataka wananchi wake wayapuuze maneno ya kejeli yanayotolewa na Mengi dhidi yake.aidha alitoa tahadhari kwa wabunge wa mkoa wa tabora wanaopenda kuongozana na Mengi kwenye ziara zake za mkoa wa tabora na kuwa kamwe hawatvumiliwa tena jambo ambalo lilishangiliwa kwa nguvu kubwa
   
  Last edited: May 23, 2009
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Asante FM, tunapenda updates kama hizi. Kudos mkuu
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Waache wafu wazikane wenyewe huko Igunga na kiongozi wao, maana kama hizi habari ni za kweli basi sikio la kufa hilo!

  William.
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Duh, kama ya Mh Chenge baada ya kutuhumiwa kuwa na vijisenti alikimbilia kwao BAriadi na kupokelewa na maelfu ya wapiga kura wake. Ni kama vile Lowasa baada ya kuvulwa Uwaziri Mkuu; alikimbilia kwao Monduli na kupokelewa na maelfu.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nadhani kinachotokea ni ujumbe kwa wana harakati. Mwananchi wa kawaida anachoangilia ni jinsi gani mahitaji yake ya kila siku (maji,chakula,malazi,mavazi,ada,matibabu,burudani etc.) yanavyoweza kupatikana. Iwapo kuna anayedhibitisha kuwapunguzi burden ya kuyapata mahitaji hayo, basi wao watamuunga mkono. Kinachotokea hapa na kilichotokea huko nyumba ni ujumbe kuwa maneno matupu ya kiharakati hayapeleki effect yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Harakati zozote ni lazima ziambatane moja kwa moja na kuwawezesha watu kumeet their immediate needs.Na ndio maana wamishionari walikuwa wanagawa nguo, vyakula etc.
  Wale ambao wamekuwa wakilaumiwa iwapo wanaprove kumpunguzia mwananchi wa kawaida burden, however miner it may seem, hutuzwa kwa vifijo vya aina kwa aina.
  Ninachoona ni ujumbe ambao umekuwa ukitolewa kwa wanaharakati mara kwa mara, sasa ni juu ya wanaharakati jinsi watavyoamua kuupokea ujumbe huu. Wanaweza kuamua kuwalaumu wananchi wa kawaida au kupata fundisho na kufanya kilicho sahihi.
  Huu ni ujumbe, na si kitu kingine.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  RA jana alikuwa mjini Dar mzee hii umetengeneza ama?!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anatoa tahadhari hii yeye kama nani? Hicho ambacho hawatavumiliwa ni kitu gani? Kwa nini 'ugo,mvi' wake na Mengi anataka kuufanya kuwa ni wa wananchi wote wa Tabora? Amechanganyikiwa?
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Masa, kuna tofauti ya saa nyingi sana kati ya jana na leo, na tabora kwa mtu kama RA mwenye ndege zake mwenyewe, anaweza kuwa Dar leo na akafika Tabora leo leo
   
 9. F

  Fisadi Mtoto JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2009
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 639
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nilipoleta taarifa kuwa kubenea kashindwa kesi mliniambai nimetunga lakini mlipokua ni kweli hamkuniomba msamaha.sasa now unasema hapa si kweli,huu ni ukweli na ndio ilivyo,magazeti mengi hayajapata nimeongea na msaki leo hajui.mimi nimesikia hutuba nzima na aziza mbunge wa viti maalumu alikuwepo akishangila japo huwa anazunguka na Mengi kumbe anamchora,na baskeli mia tatu alizogawa tabora kapewa na mengi kwa habari ambazo sijathibitisha
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu you took the word from my mouth? yeye ni nani?

  Ukistaajabu ya Mussa.., ama kweli pesa za bure bure zinalevya, inafikia mahali mtu anajisahu na kuona wanadamu wenzie wote kama vikaragosi vyake! Kwahiyo anawakemea wabunge wenzake wasitembee na Mengi?
  Yaani ana mamlaka hadi ya kuchagulia wenzie nani uongee naye, nani utembee naye makubwa haya nye!
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hata AntiChrist akija na kujitamburisha leo hii hawezi kosa Wanachama na wapenzi.Rostam siyo Fisadi wa kwanza kushangiliwa na hawezi kuwa wa Mwisho vilevile.Kwa tabia yetu ya kujivunia mtu tajiri atokeaye kwenu hata kama utajiri wake ni kidonda ndugu kwenu, haya mamboo ya kushangilia watu watushindishao njaa za matumbo na bongo zetu hayata kaa yaishe.Nawapongeza wote waliojitokeza kwenda kumshangilia shujaa wao Rostam. Ombi langu kwao ni moja wasirudi nyuma waendelee kumshangilia hadi awafikishe pale maono yake yaishiapo.
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  May 23, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  well said ....naomba kibao cha Les MWENGE ...vijana wa CTU arusha ,dansi lao hata muungwana JK akiwa capt alikuwa akilicheza....

  kibao- KILA MNDU AVE NA KWAO.

  Waswahili wanasema mcheza kwao huunzwa.....hata wasipomtunza bado familia yake haiwezi kumtupa...,familia inaanzia nyumbani ,mtaa,kijiji,eneo,mkoa,kanda,taifa etc....kama unaishi vema na familia yako hata ukiwa katili namna gani ....watakutetea hadi damu ya mwishi,ndivo maisha yalivyo~~~! hii ni ishara kuwa rostam anaishi vema na familia yake ya wana tabora!.....if mengi want to convince tabora to turn him down will be a wrong war strategy....hasa pale inapokuwa tayari wapo kwenye total warfare....tayari kuna tension,ingekuwa tofauti zao hazijawa wazi.....ingekuwa mbinu yake ya kutumia kina seleeli etc..ingesaidia...kumpata mgombea wa kumuondoa rostam bila watu kustuka ......

  pia lingine ni kuwa mzee mengi inaonekana anazidiwa ujanja na rostam hasa pale inapoonekana wazi kuwa rostam na wenzake wana wafuasi wanaomzunguka mengi.....cant you imagine mengi alijuwa kuwa mbunge aziza suleyman yuko upande wake na akampa baiskeli 300 na pesa ...na days after aziza huyo huyo anaongozana na rostam kwenye ziara........watu wanamlia mzee mengi pesa bila yeye kujijua...huku wenzake wanajiimarisha kibiashara na kimkakati!!
   
 13. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ibra,
  Ukifuatilia sana utakuta kuwa hawa jamaa (mafisadi= RA , Chenge, Lowasa) kutokana na mapesa waliyonayo huwa wana-organize watu wao katika hayo mapokezi. Hebu jiulize huko Bariadi, Monduli kuna watu wangapi wenye kumiliki magari mengi kiasi hicho? Ikumbukwe kuwa huko kote (Bariadi, Monduli) watu wakishaona misururu ya magari hukusanyika kwa wingi wengine bila hata ya kuwa na lengo maalum maadam tu wameona misururu ya magari, mimi natoka vijijini nina experience na hilo. Na ripoti tunayopewa ni kuwa amepokewa kishujaa. Nasema haya kwa sababu Lowasa kule Monduli mapokezi yake yaliratibiwa na somebody Nasari ambaye ana sikendo nyingi zikiwemo za ujambazi lakini ni swahiba wake Lowasa ndo maana hata kesi zake zimekuwa zikiishia hewani. Kwa kifupi mapokezi hayo yanayodaiwa kuwa ya nguvu huwa wanayaandaa wao wenyewe kwa pesa walizotuibia.
   
 14. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Kama kweli watu wa IGUNGA wameyafanya haya kwa RA, pamoja na kelele na shutuma zote anazolaumiwa huyu mtu, basi nadhani tumelogwa. Na ndipo ule usemi wa mwanafalsafa wa JF unapokuwa na nguvu ".. Miafrika ndivyo tulivyo..."
   
 15. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  We tangaaza tu kwamba baada ya mkutano kutakuwa na masinia ya wali togwa na ulabu, hiyo siku mtu haendi shambani wala nini.Kama nisemavyo kila siku kwa kunukuu maandiko yenye hekima, "Uovu haupatilizwi mpaka ujae katika kipimo chake na kufurika."Kipimo cha kukomaa kisiasa kimewekwa juu zaidi, ukinzani njiani kuelekea kwenye kilele cha ufanisi unazidi kuongezwa wengi wanakata tamaa na kudondoka bila kuguswa.Nani alikuambia Ikulu ni ya wanyonge??Ikulu ni ya wenye nguvu na nia ya kuwako huko.Atakaye kushika hatamu za kisiasa ni lazima awe bingwa wa ngwala na vipepsi.Fedha siyo pingamizi kubwa mbele ya watu wenye Nia na Ari, Ufinyu,Upotofu na Utapiamlo wa mawazo na mikakati ya wapambanao na Ufisadi Mama ndiyo pingamizi kubwa la kuwateza nguvu waliohodari kabisa.Fedha ni tatizo lililoko nje ya mpambanaji, Mawazo duni mikakati duni na Mwelekeo duni ni matatizo ya ndani ya mpambanaji yeyote yule na hapo ndipo ulipo udhaifu wote.
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0

  - Kwenye hili una point nzito sana na I am down.

  Respect.

  FMES!
   
 17. K

  Kinyikani Member

  #17
  May 23, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Fisadi kubwa kwa hapa TZ ni CCM bila ya kuliondoa jinamizi CCM ni sawa na kujambia mtoni.
   
 18. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama hayo ndiyo aliyowaasa viongozi wenzake ni dhahiri kwamba RM amembana pabaya.
   
 19. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu Phillemon Mikael,

  Ahsante sana kwa maelezo yako.

  Hivi hizo baiskeli 300 na fedha alizozitoa Mengi kuna motive gani nyuma yake? au ndiyo kusema kuwa anataka kuchukua nafasi ya 'u-king maker'?
   
 20. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli naombeni muonyeshe picha haa moja ikionyesha na tarehe ya tukio; story ya kutunga; hata mafisadi wa gazeti la Mtanzania hawajaandika; no; no thanks
   
Loading...