Rostam anastahili miaka mingine 5 ya ubunge!

TrueVoter

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
2,197
1,772
national examinations council of tanzania

csee 2009 examination results


s0713 igunga secondary school


div-i = 0 div-ii = 2 div-iii = 16 div-iv = 64 fld = 37
 
..matokeo ya moja ya EXTENDED PRIMARY SCHOOL makao makuu ya wilaya igunga.
 
Tanzania bila ufisadi inawezekana jamani! tuachane na huu ugonjwa wa ER, RA, Kala Maji etc
 
Pamoja na kuwa simpendi RA lakini sipendi wala sitaki kumhukumu kwa kigezo kimoja tu. Sijui watu wa Igunga wanamuonaje? Pamoja na kwamba kitaifa RA hafai kwa lolote lakini inawezekana kabisa akawa ananya vizuri jimboni mwake. Plz wananji wa Igunga tiambieni hali ya muheshimiwa huyo huko ikoje?
 
nani asiyejua jamaa ni business man - hupo pale kuvaa koti la uanasiasa ili kutekeleza azma yake - hayupo katika maslahi ya wana igunga. - hana uchungu na nchi hii huyu jamaa.

ila kwa kuwa wanaingunga na watanzania tulio wengi ni watu wa njaa basi nafikiri tutamchagua tena - pilau kwenye masinia - ngoma pale shule ya msingi igunga mpaka asubuhi.

nafikiri akichukua form - bado atakuwa mbunge tena miaka 5 ijayo - ingawa binafsi inaniuma saana.
 
Rostam hajawahi kuuliza swali lamsingi,swali la nyongeza na wala kutoa mchango wakati wa mjadala kwa vikao vyote vya bunge-2005-2009 pamoja na Lowasa na Husein Mwinyi" kutokana na tafiti iliyofanywa na Taasisi ya Uwazi-INFOSHOP;
source: mwananchi febr24,2010pg7

Ni wazi hawa wapo bungeni kwa maslahi yao tuuuuuuuuuuuuuuu.........................
 
Niniii? EL hajawahi kutoa mchango wowote bungeni? jamani hebu tuwe makini na post zetu vinginevyo tutajaza pumba humu!
 
Na atashinda tu Kama akitaka kugombea nchi si ilishanunuliwa na wenye pesa zao! Though hakuna marefu yasiyo na ncha! kuna siku wataamuka kwenye usingizi huu, ipo siku!!!
 
kwa kuwa Mh Mangula alishasema kuwa ccm uongozi na ubunge vinategemea nani anavijisenti kuliko wengine so si ajabu akashinda ukuzingatia mwaka huu Igunga njaa kali sana
 
...sifa zote anazopewa rostam zingeleta maana pale tu angalau matokeo ya shule hii yangekuwa mazuri,vile yeye kama mbunge angehakikisha shule inakuwa na walimu wa kutosha na mazingira mazuri ya elimu bora angalau kuonyesha kuyajua matatizo ya msingi ya wanaigunga!kama zaidi ya robo tatu ya wanafunzi wamefeli hata cheti hawapati,itawasaidia nini wao hata kama igunga kuna barabara ya lami na mabwawa anayosema rostam amechimba ilhali wangali wajinga??
 
Rostam hajawahi kuuliza swali lamsingi,swali la nyongeza na wala kutoa mchango wakati wa mjadala kwa vikao vyote vya bunge-2005-2009 pamoja na Lowasa na Husein Mwinyi" kutokana na tafiti iliyofanywa na Taasisi ya Uwazi-INFOSHOP;
source: mwananchi febr24,2010pg7

Ni wazi hawa wapo bungeni kwa maslahi yao tuuuuuuuuuuuuuuu.........................

Labda kuhusu swali la msingi lakini hili la maswali ya nyongeza na kutoa mchango wakati wa mjadala nadhani jamaa hatendewi haki maana nakumbuka niliwahi kusikiliza mchango wako mwaka 2006.

Hata hivyo kuhusu Rostam kustahili kuwa mbunge tena inategemea mtu anaangalia ubunge kwa mantiki ipi. Kama ni ile ya kiutamaduni yaani mbunge ni KIONGOZI na MWAKILISHI wa matatizo ya wapiga kura wake katika ngazi za kitaifa basi ni wazi hafai lakini kama ni katika mantiki ya kisasa ya kuwa mbunge ni MFADHILI wa kuhudumia matatizo ya wapiga kura wake kwa VIJISENTI vyake basi naamini bado anafaa kuendelea.

Well, ukitilia maanani Chama chake kimebaki kuwa ni Muundombinu wa Uchaguzi tu (electoral machinery only) then ni wazi Rostam ni mtaji ambao hauwezi kutupwa kutokana na makelele ya WEHU wa wachache wa jamiiforums na magazetini.

Huo ndio ukweli mchungu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom