Rostam amgeukia Nape Nnauye

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

picture-9.jpg

Na Alfred Lucas - Imechapwa 14 September 2011


nape3.jpg


NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa hali si shwari tena. Wanaojiita waasisi wa "mpango wa chama wa kujivua gamba" wameanza kutuhumiana kukivuruga chama, imefahamika.Taarifa zinasema mlengwa mkuu wa kinachoitwa, "kukivuruga chama" ni Nape Nnauye, katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi na Uenezi.

Nape anadaiwa kukivuruga chama kutokana na hatua yake ya kwenda Inguga, wiki mbili zilizopita. Inadaiwa hatua ya Nape kwenda Igunga imewaudhi baadhi ya wakubwa zake, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na katibu mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, ambaye anadai kuwa uamuzi wa Nape waweza kudhoofisha nguvu ya CCM.
Hatua ya Mukama inatokana na uamuzi wa CCM kumpigia magoti Rostam Aziz, mmoja wa watuhumiwa watatu wa ufisadi wanaotakiwa kujiondoa ndani ya chama hicho.

Wengine wanaotakiwa kuondoka ni Edward Lowassa na Andrew Chenge.
Tayari Rostam amejiuzulu nafasi zake zote kwenye chama hicho, ukiwamo ubunge wa Igunga na ujumbe wa NEC.Mukama na Kikwete ndio waliasisi mpango wa chama wa kujivua gamba, Aprili mwaka huu, kwa madai kuwa watuhumiwa hao watatu wa ufisadi wanakishushia hadhi chama hicho mbele ya jamii.

Habari kutoka ndani ya CCM mjini Dar es Salaam na makao makuu mjini Dodoma zinasema, Mukama alimtuhumu Nape kwa hatua yake ya kwenda Igunga gafla, akisema imelenga kukidhoofisha chama hicho.
Nape alikwenda Igunga tarehe 4 Septemba 2011, kwa kile alichodai kutoa pole kwa familia ya wazazi wa mtoto Peter Ezekiel, aliyefariki dunia papohapo baada ya kugongwa na gari la mizigo, wakati mgombea wa CCM, Dk. Peter Kafumu akichukua fomu.

Taarifa zinamnukuu Mukama akimueleza Nape, "…nimeambiwa umekwenda Igunga, wakati Kamati Kuu ya chama imekuzuia kwenda huko. Unataka nini? Mbona unataka kutuharibia uchaguzi," alifoka Mukama.

Vyanzo vya taarifa kutoka CCM vinasema, Mukama aliamua kuchukua hatua hiyo ili kumfurahisha Rostam ambaye sasa anaonekana lulu ndani ya chama hicho.
Wachambuzi wa mambo wa ya kisiasa wanasema, hatua ya CCM kumdhoofisha Nape kwa kukumbatia watuhumiwa wa ufisadi, inazidi kukimaliza chama hicho kikongwe nchini.

Kwa mujibu wa waliokaribu na Nape, safari ya kiongozi huyo mjini Igunga ililenga kuwatambia baadhi ya wapinzani wake wa kisiasa waliodai Rais Kikwete amempiga marufuku kukanyaga huko wakati huu wa kampeni.
Kuthibitisha madai hayo, Nape aliandika katika mtandao wa JamiiForum, mara baada ya tukio hilo la Igunga, "Mlisema chama kimempiga marufuku Nape kukanyaga Igunga, nikasema tusubiri.

Leo, mmeona nilivyotinga Igunga…"
Kwa mujibu wa mashuhuda, mara baada ya Nape kutoka nyumbani kwa wazazi wa Peter Ezekiel, alikwenda moja kwa moja kwenye baa maarufu iitwayo The Peak, ambapo inadaiwa alinisurika kichapo kutoka kwa mmoja wa mabaunsa wa CCM.Inadaiwa kijana huyo wa miraba minne aliyefahamika kwa jina moja la Shaban, ambaye inadaiwa ni kutoka kwa kundi la Rostam Aziz, mara baada ya kumuona Nape kwenye baa hiyo alifoka, "Wewe unatafuta nini hapa?"Naye Nape akajibu, "Wewe unafahamu unaongea na nani?" Shaban akajibu, "Ndiyo. Nafahamu kwamba wewe ni Nape Nnauye."Kauli hiyo ilianza kumfanya Nape anyong'onyee kidogo, lakini mtoa taarifa anasema alijipa nguvu na kusema, "…Nimekuja kikazi. Tupishe tunamazungumzo yetu."Shaban aligoma kuondoka na kisha akasema, "…Ondoka hapa, vinginevyo tutakuonyesha. Umekuja kutuharibia uchaguzi siyo?"Mara baada ya kauli hiyo, taarifa zinasema Nape aliondoka katika eneo hilo na kuingia kwenye gari lake haraka kuelekea Singida.

Alipoulizwa na waandishi wa habari mjini Igunga kwa nini anadhani amefanyiwa vurugu, Nape alisema, "Hakuna kitu. Nilikuwa napita njia tu."
Sokomoko hilo lilitinga hadi kwa viongozi wake wakuu wa chama, Mukama na Rais Kikwete. Inadaiwa mara baada ya kupata taarifa hizo, Mukama kwa hasira alihoji, "Nape kwa nini umekwenda Igunga?"Alisema, "Umekatazwa na Kamati Kuu usiende Igunga, sasa mbona umekwenda?" Alipojaribu kujitetea kwamba alikwenda huko kuhani, Mukama alisema, "Nani amekutuma? Nani amekuruhusu? Kijana, tafadhali usituharibie uchaguzi," Mukama anaripotiwa kufoka.

Gazeti hili lilipomtafuta Nape kuthibitisha madai hayo, alijibu kwa sauti ya unyonge, "Alfred, mimi sina la kusema juu ya hilo." Akauliza,

"Jamani, mimi kijana mwenzenu. Nimewakosea nini? Niambieni basi."
Kwa upande wake, Mukama alipoulizwa alianza kwa kucheka, "Aaah aaah aaah…umeyapata wapi hayo?" Akasema, "Sikiliza Alfred, hilo suala la Nape achana nalo. Si suala la magazeti…""…Fahamu sisi hatufanyi kazi za kiutendaji na magazeti. Isitoshe si vema kuzungumza mambo mazito kama haya kwenye simu. Nakwenda Zanzibar, nitarudi kesho (jana Jumanne). Njoo ofisini keshokutwa (leo Jumatano), tuzungumze."Alipoelezwa gazeti liko mbioni kwenda mtamboni, Mukama alisema, "Sawa, lakini kwanini usije ofisini?"Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa, tarehe 9 Septemba 2011, Nape akiwa Dodoma anajiaanda kuelekea Igunga kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za chama chake, ghafla aliitwa na Mukama na kuambiwa, "…hutakiwi kukanyaga Igunga."Alisema, "Nimeambiwa unajiandaa kwenda Igunga? Mbona wewe kijana husikii," alisikika Mukama akimueleza Nape.

Pamoja na kwamba Nape ndiye katibu mwenezi wa CCM, hakuwapo Igunga wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo na hatarajiwi kutia mguu.
Mbali na Nape, CCM inadaiwa kumzuia Samwel Sitta, Christopher ole Sendeka na Dk. Harrison Mwakyembe ambao walipendekezwa na Nape kuendesha kampeni hizo, kwa kile kilichoitwa, "Kutomuudhi Rostam." Baada ya ufunguzi wa kampeni, Mukama akiwa mwenye furaha, aliwaambia baadhi ya viongozi na wanachama wa chama hicho waliokuwapo mjini Igunga, "Tumefanikiwa sana katika mkutano wetu huu. Kuna watu wengine bwana, hawana discipline (nidhamu); hawana adabu wanajiona wanaweza kuvuta watu kwenye mkutano."Mwiguru (Nchemba) anafanya kazi nzuri sana. Ameratibu mkutano huu vizuri. Kampeni zimekwenda vema. Ni kijana mwenye busara sana yule," ameeleza mtoa taarifa akimnukuu Mukama.









 
Wow Poor Nape Nnauye... Sasa atasema nini? LOST IN TRANSLATION???
 
mie siamini kama kuna watu wenye akili timamu bado waishabikia ccm wananchi wanachezewa kekundu na keusi wao wanashangilia.
 
niliwahi kumwambi humu huyu nape akajifanya mjanja ....anapenda sifa sana yule ...natamani lile baunsa lingemtandika
 
Baada ya kugundua kwamba habari zilizoandikwa kwenye gazeti hilo ni za uongo, nyie mnaoshabikia na kumuombea mabaya Nape hamjui kwamba ni mateka wa ufisadi na mnashabikia madhila ambayo wananchi wanafanyiwa na mafisadi? Nyie pia mnasaidia "kumtorosha mwizi".
 
mie siamini kama kuna watu wenye akili timamu bado waishabikia ccm wananchi wanachezewa kekundu na keusi wao wanashangilia.

NILISHASEMA HAPA NAPE NI BWABWA DIZAIN MKANIBISHIA MWANGALIENI MKONONI ANAVAA KIKUKU NA MGUUNI PIA NASIKIA ANACHO SASA WAMEMTUMIA NA WANAMTEMA KAMA TAMBARA BOVU ILA NASIKIA ANAMPANGO WA KUJIUNGA cuf
 
NILISHASEMA HAPA NAPE NI BWABWA DIZAIN MKANIBISHIA MWANGALIENI MKONONI ANAVAA KIKUKU NA MGUUNI PIA NASIKIA ANACHO SASA WAMEMTUMIA NA WANAMTEMA KAMA TAMBARA BOVU ILA NASIKIA ANAMPANGO WA KUJIUNGA cuf
mtaishia ivo ivo kumzushia mara cuf mara ccj..huyu n ccm damudamu...najua cdm mnamtaman aje cdm
 
Kutumia wataalamu wa uongo kuuficha ukweli hakumaanishi kwamba ukweli utapotea bali ni kama kutoa majibu ya uongo kwa mgonjwa ambapo ugonjwa ukidhihiri hata asiye mataalamu atabaini mgonjwa yu taabani......na hatutohitaji tena utaalamu katika kubaini ukweli ...
 
mwambieni aje CDM, msimshitue kuwa nimewaambia atajua nyie mwambieni kimya kimya atakuja tuu huku CDM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom