Rostam Aishtaki Mwanahalisi

MwanaHabari

JF-Expert Member
Nov 9, 2006
442
13
MFANYABIASHARA maarufu nchini,Rostam Azizi Pichani,amemshitaki Mhariri wa gazeti la kila wiki la MwanaHalisi na wachapishaji wake akitaka alipwe Sh bilioni tatu kwa kuchapisha habari zinazomkashifu zikimhusisha pamoja na mambo mengine, kashfa ya Kampuni ya Richmond.

Rostam ambaye pia ni Mbunge wa Igunga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam wiki iliyopita, akimtumia wakili Kennedy Fungamtama. Licha ya kutaka alipwe kiasi hicho cha fedha, Mbunge huyo pia anaiomba Mahakama kutoa amri ya muda kulizuia gazeti hilo, wakala wake au yeyote kuchapisha habari zinazomkashifu.

Zaidi ya hayo, mfanyabiashara huyo ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Kamati Kuu, anaiomba Mahakama iliamuru gazeti hilo kumwomba radhi kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo kwa uzito uleule au zaidi baada ya hukumu yake.

Pia anaomba alipwe gharama za kesi. Rostam anadai kuwa gazeti hilo la MwanaHalisi lilichapisha habari za uongo na za kumkashifu katika toleo lake namba 084 la Februari 13 hadi 19, mwaka huu, chini ya kichwa cha habari, "Richmond ya Rostam Azizi, Ndiye aliyeileta nchini." Kulingana na mfanyabiashara huyo, kichwa hicho cha habari pamoja na habari yenyewe, zinaonyesha kuwa yeye ni mdanganyifu, asiye mwaminifu, mtoa rushwa na anayetenda matendo maovu na mtu anayeshiriki katika mambo ya udanganyifu.

Rostam anadai kuwa licha ya kuweza kupatikana kwa taarifa sahihi na za wazi kwa urahisi na kwamba kwa njia yoyote ile hajashiriki katika matendo hayo maovu, gazeti hilo liliendelea na kampeni chafu dhidi yake katika toleo lake la 085 la Februari 20 hadi 26, mwaka huu. Anadai kuwa gazeti hilo linadaiwa kuchapisha habari nyingine kwenye ukurasa wa pili chini ya kichwa cha habari, "Kikwete amtosa Lowassa" likimhusisha na biashara zake na kampuni yake, kwamba ni mtu anayefahamika kwamba anaweza kubadilisha ukweli kukidhi matakwa yake.

Mbunge huyo analituhumu gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari kama hizo katika toleo lake la 087 la Machi 5 hadi 11, mwaka huu na toleo la 093 la Aprili 16 hadi 22, mwaka huu likimwonyesha kuwa si mtu muadilifu na anatumia vibaya nafasi yake kwa maslahi yake binafsi. Mfanyabiashara huyo analalamika kuwa maneno hayo yalikuwa na nia ya kumchafua katika biashara na kazi yake kama Mbunge; hivyo kuharibu wasifu, tabia, uadilifu na hadhi yake na kuonyeshwa kwenye jamii kuwa ni mtu wa kashfa, asiye na maana na mdanganyifu.

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo, amejijengea hadhi kama raia mwema, mfanyabiashara, mwanasiasa na mtu wa kuaminika kwa miaka mingi na kutokana na kashfa hiyo, amevunjiwa hadhi mbele ya jamii. Mbunge huyo amedai kuwa anastahili kulipwa kutokana na udhalilishaji huo kwani hadhi yake imeshushwa kiasi cha kuathiri biashara na kazi yake kwa kiwango cha kushindwa kuendesha kazi na biashara yake kwa urahisi.

Habari hii na Faustine Kapam

Habari kutoka (http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/)
 
Anatapa taba tu huyo,

Mimi nashangaa sana , hawa MAFISADI na pesa zote hizo walizochukua haziwatoshi? Hivi wanawafanya wa TZ ni watu mbumbumbu sana , eti anashtaki ndio nini? ama tuone kama hajaiba.

Yeye ni fisadi tu afanye afanyavyo hawezi kutudanganya.
 
Hapa ni pazuri nafikiri tunaelekea kwenye ushindi watanzania tumechoka kumlipa FISADI pesa kila siku.

Mwahalisi kuguswa ni kugusa watanzania.
 
kafungua kweli kesi ?Je washauri hana wa kumweleza kwamba aachane na haya ? Je ataweza mikiki ya mahakamani maana Mwana Halisi atapata mawakili kibao na kupambana na hapo unaweza kushanaa viongozi wa CCM sasa wanaitwa Mahakamani .Ni kweli kafungua ama waandishi tu jamani ?Maana tuliambiwa Masha kafungua ikawa hadithi hadi sasa .
 
OMG, Huyu ana lazima gani ya kuonekana kama yeye ni mtu safi wakati sio safi? Anataka nini haswa? uraisi? Basi sasa ndio kachemka kabisa! Na itambidi azitumie hizo billions zake za Richmond ili kuhonga waandishi wote waliobaki Tz wasimwangaze uchafu wake!
Tanzania tumeingiliwa kweli na uzungu matata?
 
Anatapa taba tu huyo,

Mimi nashangaa sana , hawa MAFISADI na pesa zote hizo walizochukua haziwatoshi? Hivi wanawafanya wa TZ ni watu mbumbumbu sana , eti anashtaki ndio nini? ama tuone kama hajaiba.

Yeye ni fisadi tu afanye afanyavyo hawezi kutudanganya.

Mimi nadhani RA amefanya makusudi kwenda mahakani ili awaeleze wananchi yale alitaka kueleza bungeni akakataliwa so anajua atashindwa hiyo kesi lakini atakuwa amefikisha ujumbe kwa wahusika.

Tumpatie nafasi jamani
 
Mbunge huyo analituhumu gazeti hilo kuendelea kuchapisha habari kama hizo katika toleo lake la 087 la Machi 5 hadi 11, mwaka huu na toleo la 093 la Aprili 16 hadi 22, mwaka huu likimwonyesha kuwa si mtu muadilifu na anatumia vibaya nafasi yake kwa maslahi yake binafsi.

Okay! now he is talking, sasa cha muhimu hapa ni kwa Mwanahalisi kwenda naye kwenye sheria, ili ukweli usemwe wazi ninasema haitakuja tena nafasi kama hii, kama ikibidi tuwasaidie wenzetu wa huko gazeti la Mwanahalisi kwa hali na mali, ili hii ishu ifike mahakamani ili nyani akomwe mchana,

Wakuu wa Mwanahalisi, hapa tuko ukurasa mmoja wakuu huyu Patel ni kukutana naye mahakamani tu na apewe ukweli wa uovu wake, upo mwingi sana, labda tuanze kuwasogezea ushahidi pole pole,

wananchi hatuwezi kutishiwa nyau na mafisadi...!
 
Ukisikia mimi nakuunga mkono na kukubali ukifanya vyema ES ni kwenye maswala kama haya .You have said it all .Nakupongeza kabisa na sasa huyu jamaa nadhani kalengeshwa na ndiyo mwisho wake sasa .
 
huyo rostam anajishaua tu, anataka awaburuze watanzania waache kufuatilia uozo wake wafuatilie kesi yake.....
 
Mahakamani si ndio kila siku tunaomba hawa watu wapelekwe !Sasa huyu katangulia mwenyewe he choose to take one for the team.Hapa ndio muda wa sisi kutumia nguvu zote kumbana mbavu let us use this chance .Ndio wakati hata tume ya Bunge iliochunguza kusaidia hapa kutaja wanachujua juu ya hili .Pia inaonekana anataka kusema alichobaniwa bungeni something is cooking si bure wacha wakaang'nane!
Ila awezi kukimbia ngoma hii wakati ametokakusema kampuni iliyoridhi tender ya Richmond anaubia nayo,anafikiri watu hawajui mambo ya sheraton ya bongo kubadilishwa majina kila kukicha kukwepa kodi!Nao wanataka kuleta janja ya nyani kula hindi bichi.
MwanaHalisi anahitaji mawakili wa kuaminika ikiwezekane tuchangie wa Tz.
 
Nafikiri Rostamu ana ambition yake lakini waliomshauri nafikiri wamepotea kidogo. hapa alipokwenda hapashikiki Tanzania ya sasa uzalendo siyo pesa, pesa haitafanya kazi.

Alizoea kuwanunua akina Mkapa sasa atakoma tu unajua wengine tulifikiri dili limemalizwa bungeni tunashukuru ameingiza kichwa mwenyewe. Majibu yake atayapata vizuri.

Kauli mbiu sasa: Taifa Mbele pesa nyuma.

Sasa hivi inatakiwa mambo yote yaende pamoja uraia wake na biashara zake
 
Mahakamani si ndio kila siku tunaomba hawa watu wapelekwe !Sasa huyu katangulia mwenyewe he choose to take one for the team.Hapa ndio muda wa sisi kutumia nguvu zote kumbana mbavu let us use this chance .Ndio wakati hata tume ya Bunge iliochunguza kusaidia hapa kutaja wanachujua juu ya hili .Pia inaonekana anataka kusema alichobaniwa bungeni something is cooking si bure wacha wakaang'nane!
Ila awezi kukimbia ngoma hii wakati ametokakusema kampuni iliyoridhi tender ya Richmond anaubia nayo,anafikiri watu hawajui mambo ya sheraton ya bongo kubadilishwa majina kila kukicha kukwepa kodi!Nao wanataka kuleta janja ya nyani kula hindi bichi.
MwanaHalisi anahitaji mawakili wa kuaminika ikiwezekane tuchangie wa Tz.

Duh! I love JF yaaani mawe huwa ni kutoka kila kona!
 
kapeleka kesi ili apewe nafasi ya kusema atakacho na kujisafisha kwenye magazeti, ikisha ataifuta.

haiwahi kuwa kesi kubwa hii ataifuta
 
this is a libel case...anakila haki yakushtaki.. its ccalled the law.. I love it. Itasaidia ku maintain standards kwenye media waandishi waandike bila uoga ila ukweli.. sio opinions, we have vijiwe for that. we want facts.. and RA anaweza kujikuta anaibika if they can prove on a balance of probabilities kuwa he = RICHMOND then ataUMBUKA so this case is a good thing...lol
 
Mie nasema Mwacheni aende,Nenda Baba,Nenda Rostam,Nenda Aziz
Na nitamwandikia Kubenea Allegataion cha nini cha kufanya ili tuchukue ushindi mwingine wa chee.Nadnani wakati umefika kwa kupata maamuzi kutoka katika haki ipatikane,billioni tatu si mchezo

hapo ndipo akutuelezee nani ni mmilikiwa RDC sababu ushahidi tunao,na nadhani itakuwa muhimu kuwepo kwa mashahidi kama DR. Msabaha.

Serikali imeshindwa kuwachukulia Hatua,sasa haki kupatikana mahakamani,Ripoti ya Mwakyembe itasaidia sasa kujua what is behind the scene.

Go Rostam,Go Aziz,Go and GO to heal
 
RA ni mfanyabiashara 'mwenye mafanikio' makubwa, ila nina mashaka na uwezo wake wa kuchambua mambo. Bahati mbaya kwangu sijawahi kumsikia akifanya uchambuzi wowote au hata kusoma.

Ukiichoma nyama yenye mafuta mengi huwa inaufanya moto uwake zaidi.
 
.
Kulingana na mfanyabiashara huyo, kichwa hicho cha habari pamoja na habari yenyewe, zinaonyesha kuwa yeye ni mdanganyifu, asiye mwaminifu, mtoa rushwa na anayetenda matendo maovu na mtu anayeshiriki katika mambo ya udanganyifu.

Which is true. We are slowly seeing the battle taking another turn, instead of "mdanganyifu, asiye mwaminifu, mtoa rushwa na anayetenda matendo maovu na mtu anayeshiriki katika mambo ya udanganyifu"
to be brought to justice, we see him trying to play with justice to bring the honest ones to justice. I hope the justice will be in favour of the truth and reality not money as it has mostly been.
I think he has started his end, let us give him a big clap!!
 
Sijui kama huyo Rostam amekurupuka maana ukiangalia toleo analo lilalamikia ni la muda mrefu huenda amekaa na wanasheria na majaji na washauri kibao kuona jinsi watakavyo weza kulishitaki gazeti hilo!
Pia inasekemekana Mwakeyembe hua analiandikia gazeti hilo na pia alivujisha baadhi ya siri ya tume kwenye gazeti hilo kabla ya kuwasilisha bungeni!
Sidhani huyo Rostam atakuwa punguani kiasi hicho pamoja na ufisadi wake anajua anacho kifanya!
HIVI SIMBA MWENYE NJAA AMEKWENDA KUWINDA NYAMA AMEANZA KULA GHAFLA UNAMCHUKULIA NYAMA KUTOKA KINYWANI MWAKE!UNATEGEMEA NINI!!!
 
RA ni mfanyabiashara 'mwenye mafanikio' makubwa, ila nina mashaka na uwezo wake wa kuchambua mambo. Bahati mbaya kwangu sijawahi kumsikia akifanya uchambuzi wowote au hata kusoma.

Ukiichoma nyama yenye mafuta mengi huwa inaufanya moto uwake zaidi.

Mafanikio ya wizi na hujuma kwa Taifa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom