Rostam aibukia kanisani!

Hivi hiyo albam haijatoka tu?
Nina hamu sana ya kuiskiliza maana hata uzinduzi nadhani itakuwa labda ni Rostama ama Lowassa.
 
Kanisa lingekuwa na masikio lingeshasikia, wametandika kitanda chao cha unafiki sasa wamelala na mafisadi, wamefumwa wanang'aka huku wakijibaraguza kuficha utupu wao!

Naam na ni unafiki wa hali ya juu kumkana RA wakati pesa zake za kifisadi wametia ndani. Warudishe hizo pesa ili kurudisha imani ya waumini kwa kanisa hilo.
 
Rostam akanwa

2008-07-10 11:47:37
Na Lucy Lyatuu na Simon Mhina


Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, limemkana Mbunge wa Igunga Bw. Rostam Aziz na kusisitiza kwamba, hana usafi kama alivyojitapa kwamba amesafishwa na kanisa hilo.

Aidha, Kanisa hilo limesikitishwa na kukanusha matamshi yake ya kulisifu kanisa kwa kutambua usafi wake kutokana na tuhuma za ufisadi zinazomkabili.

Taarifa ya KKKT iliyotolewa jana na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Balozi Richard Mariki, ilisema, kanisa halikuwa na taarifa ya ujio wa mwanasiasa huyo katika Usharika wa Kinondoni.

Taarifa hiyo ilisema kanisa limegundua kwamba, Bw. Rostam, alialikwa na kikundi kidogo ndani ya usharika huo ambacho hakikuwa na mamlaka ya kumwalika.

``Tunasikitika kusema kwamba, kanisa halikuwa na taarifa ya ujio wa Bw. Rostam na tunapenda kuwaarifu kuwa, taratibu za kuwaalika wageni kwenye shughuli za kikanisa, hazikufuatwa,`` ilisema taarifa hiyo.

Kanisa hilo limetoa taarifa hiyo kuafuatia kikao cha dharura cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi hiyo kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambapo kilijadili kwa kina taarifa zilizoandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu Bw. Rostam, kutembelea Usharika wa Kinondoni.

Taarifa hizo zilihusu madai ya Bw. Rostam, akipongeza KKKT kutambua usafi wake kutokana na tuhuma za kashfa za ufisadi zilizotolewa dhidi yake kwa nyakati tofauti.

Alinukuliwa akisema hayo katika uzinduzi wa kanda za kwaya ya Amkeni iliyopo chini ya Usharika wa Kinondoni.

Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa madai yaliyotolewa na Bw. Rostam, hasa ya kudai kanisa limetambua usafi wake, si sahihi na nipotofu.

``Kutokana na ukikukwaji wa taratibu hizi hayo madai yaliyonukuliwa katika vyombo vya habari kwamba ujio wa Bw. Rostam katika usharika wa Kinondoni na tafsiri ya ujio huo kuwa Kanisa linatambua usafi wake si sahihi na nimadai potofu,`` ilisema sehemu moja wapo ya taarifa hiyo.

Ilisema kanisa hilo haliruhusu sharika zake zitumike kama jukwaa la kisiasa la kujisafisha au kuwasafisha mafisadi.

Badala yake ilisema KKKT imekuwa mstari wa mbele katika kupinga na kukemea mambo ya ufisadi na linaunga mkono juhudi zote za kuutokomeza uovu huo.

Kufuatia ujio huo batili wa Bw. Rostam katika kanisa hilo, KKKT imewaomba radhi waumini wake, wananchi na wale wote wenye mapenzi mema ambao kwa namna moja au nyingine wamekwazwa na tukio hilo.

``Jukumu la kanisa ni kuokoa roho za watu, na si kukumbatia mafisadi na wala rushwa,``ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kwamba, kuanzia sasa, kanisa litachukua tahadhari kubwa kuhakikisha kuwa jambo kama hilo halitokei tena.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Bw. Rostam alikiri kusikia habari za KKKT kumkana na kumkandia.Hata hivyo, alisema kwa vile habari hizo hajazipata rasmi, apewe muda ili aweze kutafakari kwanza.``Hilo ni jambo zito kidogo, ngoja nipate muda wa kutafakari,``alisema.



Jumapili iliyopita, Bw. Rostam alitembelea kanisa hilo na kushiriki katika uzinduzi wa kanda za kwaya ya Amkeni na kutoa msaada wa Shilingi milioni tano, seti ya vyombo vya muziki na jenereta lenye thamani ya Sh. milioni 2.6.
  • SOURCE: Nipashe
 
Rostam hilooo!usitutishie na vijisenti vyako!sisi maskini jeuri ipo siku utalitambua hili!
ulifikiri utafanikiwa kujisoap kupitia kanisa sasa umeula wa chuya!
 
Rostam hilooo!usitutishie na vijisenti vyako!sisi maskini jeuri ipo siku utalitambua hili!
ulifikiri utafanikiwa kujisoap kupitia kanisa sasa umeula wa chuya!

Mi nakwambia anaweza akaenda na watu huyu!
Keshawapa pesa nyingi sana hawawezi kumtema hivi hivi tu!
Kwani First Lady hata kama ingekuwa wewe ungekubali kweli?
 
teh teh tehh umesahau kuwa ni mwana sisiemu mwandamizi? maneno mingi mingi vitendo hakuna.

Words create mama itafika mahali hao ccm wenzake watammaliza kama wanavyomalizana wenyewe kwa wenyewe.
 
Words create mama itafika mahali hao ccm wenzake watammaliza kama wanavyomalizana wenyewe kwa wenyewe.

ndo kusema wht goes around comes around sio? watammaliza kama alivyotumaliza kwa ufisadi?
 
Huyu bwana atatafakari saana mwaka huu maana naona ninakuwa siku ya kufa nyani.alikfikiri kapumua oxgyen kumbe ndo kwanza kavuta kambondoixide/na carbonmonoxide ya kutosha.Akitafakari vibaya anaweza kulazwa kwa mapresha na kisukari

Hawa KKT tamko sawa tumewasikia je,na vijisent vyake wamerejesha ?
 
Huyu bwana atatafakari saana mwaka huu maana naona ninakuwa siku ya kufa nyani.alikfikiri kapumua oxgyen kumbe ndo kwanza kavuta kambondoixide/na carbonmonoxide ya kutosha.Akitafakari vibaya anaweza kulazwa kwa mapresha na kisukari

Hawa KKT tamko sawa tumewasikia je,na vijisent vyake wamerejesha ?

Mkama..Unataka kuniambia wakisema wanarudisha milioni saba unusu Rostam hatadai ZOTE ambazo ameshawahi kutoa na hata misaada aliyowahi kutowa huko nyuma?

Ama wewe unaamini kuwa hizo milioni tano na genereta ndiyo zili linunuwa kanisa?

Mi nafikiri mchango wa Rostam si EM SABA TU BANA.
Ukisema ROSTAM ARUDISHIWE KILA KITU KANISA LINAWEZA KWENDA MUFLIS!
 
Hakuna 'mbinu' katika ukweli. Hata mafisadi watumie mbinu gani kujisafisha, bado 'kweli' itashamiri. Kama ukweli hautathibitika leo utathibitika kesho ana keshokutwa.

Inasikitishwa kuona kwamba zoezi zima la kujikosha ni kuchezea hisia za wananchi kwa kutumia dhiki ama umbumbumbu wao wa kuelewa mambo.
 
Maneno ya KKKT yamekosa kitu muhimu. Kama kweli wanapinga kwa vitendo wangeuelekeza usharika wa kinondoni kurudisha mchango aliotoa rostam kwa kuwa ni wa kifisadi
 
Maneno ya KKKT yamekosa kitu muhimu. Kama kweli wanapinga kwa vitendo wangeuelekeza usharika wa kinondoni kurudisha mchango aliotoa rostam kwa kuwa ni wa kifisadi

Hawawezi!

Mchango wa ROSTAM si wa sharika moja tu!

NI MCHANGO WA KKKT NZIMA...I mean mchango wake unajulikana na KKKT TAIFA!

Na ndio maana hawataki kugusia hapo kwenye pesa!
Jamaa unaweza kuta alishakuwa Mlutheri kisirisiri...!
Maana ana mizizi sana!
Kwani hata kauli ya kupinga si ya KKKT MAKAO MAKUU...NI YA USHARIKA WA PWANI!
Malasusa kasusa!
Kimya tu.
 
hili suala lote ni kama mfano wa abiria, gari, mmiliki wa gari, na dereva wa gari.

Gari (kanisa - KKKT Kinondoni)
Dereva wa Gari (Mchungaji - KKKT Kinondoni)
Mmiliki wa Gari (KKKT Dayosisi)

Dereva wa Gari ana uhuru wa kumpakia Abiria yeyote (hata Rostam Aziz) lakini kwa kibali cha Mmiliki wa Gari. Inapogundulika kuna abiria alipanda bila ya Mmiliki kupewa taarifa basi kosa si la abiria ila la Dereva! Na hapa ndipo KKKT waliposimamia! They are right!

Na Abiria (Rostam) alikuwa ana haki ya kupanda kwenye Gari (KKKT Kinondoni)kwani alisimamiwa na Dereva (Mchungaji - KKKT Kinondoni). Sasa kama Abiria aliacha "vumbi" ndani ya Gari si busara kumwambia njoo chukua vumbi lako, hapo kinachohitajika ni busara ya Mmiliki wa Gari.
hata yule Yuda Iskarioti wa Biblia alipopewa pesa ya kifisadi, baadaye alitaka kuirudisha lakini wenye pesa wakamwambia kiendacho kwa mganga hakirudi.
Aliishia kujiua.
Wana kwaya wale tu hizo milioni zao 7 na kazi kwa RA sasa kupata hukumu.
Na asulubiweeeeeeeeeeeeeee.
 
Mkuu sikuwahi kutegemea wewe kuja na maneno haya ya jazba na ya vitisho kwa watu kisa una wajua watu.Kazi yao ni kutafuta kumfahamu fulani ni nani na anachangia nini?wewe nimmojawapo ambmao mnatumia jina la bandia kama mimi.. kama wao ni wapuuzi kw amantiki ya kutumia majina yao ya bandia,basi nawewe utakuw ani Mpuuzi tu kwa maana hiyo.Usimtishe mtu sababu unaweza kujiona ni bora zaidi ya mtu mwingie .

Mkuu Gembe,

Kama huelewi ni vyema kuuliza badala ya kurukia usiyoyaelewa, nimesema hivi na ninarudia kuwa hapa JF kuna vibaraka wa Rostam na Lowassa, ambao ingawa wanatumia majina ya bandia ninawajua na ninasema tena ni wapuuzi kwa sababu sisi wa-Tanzania hatuwezi kuchezewa nao, sasa eti na wewe umeamua kujiweka kundi hilo la vibaraka wapuuzi wanaokuja hapa kuwasafisha hao mafisadi, sasa untaka nikusaidiaje?

Acha kurukia usiyoyajua mkuu, haya hayakuhusu soma kama huelewi uliza mbona unanitumia maneno mengi sana kwenye PM, sasa haya imekuwaje na wewe ni mmoja wapo nini? Halafu aliyekuambia kuwa mimi ni Zitto kama unavyosema kwenye PM ni nani? Hivi leo kumepita nini hapa JF, maana sasa I am lost!

Maneno ya mafisadi mbona yamewakuta wengi hapa, au ndio? Mkuu Gembe ni haki yangu kuandika ninachokijua na wewe pia, lakini sio haki yako kunivalisha maneno ya uongo, nimesema kuwa wale vibaraka wanaotumwa hapa kujaribu kutuchanganya kuhusu mafisadi ni wapuuzi na ninawajua na ikibidi ninaweza kuwataja majina, sasa haya wewe yamekukutaje na huhusiki na ufisadi wala hao vibaraka?

Ibara ya 18 inatoa uhuru wa mtu kueleza habaro yoyote kwa mtu yeyote bila kuvunja sheria ya nchi.na inandelea kumruhusu mtu kushikilia habari na kumweleza yeyote habari aliyonayo.

Kama unawaju basi wataje wote ambao ni wapuuzi sababu inaruhusiwa

Mkuu mbona hueleweki, nikiamua kuwataja hawa vibaraka utakuwa ni uamuzi wangu bro sio wako wewe na sheria zako! Eti hiyo sheria yako inasema kuwa ni lazima niwataje?
 
mbona KKKT wapo kimya kuwakemea mafisadi waliomo ndani ya kanisa kama mlezi KKKT dayosisi ya mashariki Benjamin Mengi,na Kaka yake ambaye ni mfanyabiashaara maarufu Reginald Mengi walowatapeli wazungu na kuwafukuza nchini,au michango yao ni mikubwa kwa kanisa,jamani nani hawafahamu wafanyabiashara haramu wengi ni wana jumuia ya KKKT.nani hawafamu akina Kibo Mareale na biashara zao ,nani hafahamu kuwa katibu mkuu nsaafu kwa KKKT tz AMZA MWAENEGOA,alivyokuwa fisadi kiasi cha kukataliwa na akina CLEOPA MSUYA waziri mkuu msaafu,hata ALIPOGOMBEA UBUNGE NA KUSHINDA ALMASHAURI KUU YA CCM LIKAKATA JINA LAKE,
Nina wasiwasi na katibu mkuu wa sasa inawezekana Mengi kamweka mfukoni."Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni",kwa hili KKKT wamemuonea ROSTAM,kama binadamu kama ana makosa ilitakiwa aombewe ili arudi kundini,tujifunze kutoka kwa yesu na zakayo,
Viongozi wa dini msichanganye siasa na dini

Hapa umeongea ukweli ndugu yangu maana RA amekuwa akitupiwa lawama bila sababu za maana.
RA alialikwa hapo kanisani, hakujipeleka. Aliombwa msaada wa kuchangia hiyo kwaya na yeye kwa uzalendo na upendo aliokuwa nao aliamua kutoa sh mil 7.6, sasa kwanini leo alaumiwe kwa hilo?.
Na hata kama alikwenda kanisani mwenyewe kuna ubaya gani?, kanisa ni nyumba ya Mungu kila mtu anaweza kuingia humo. Yesu mbona alikuwa anaongea na watoza kodi pamoja na kula nao chakula pamoja?.
Jamani KKKT ni wanafiki na si vyema kumtupia lawama RA ambazo si zake.
 
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Mashariki na Pwani, limetoa taarifa likimkana Rostam Aziz kwa kudai kwamba kanisa halikumualika rasmi kwani aliyemualika hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo na hakufuata taratibu zilizowekwa na kanisa hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom