Rostam aibukia kanisani!

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!
 
hakya mungu
kumbe hell inawafundisha watu kuipenda mbingu?
 
Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).

Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...

Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.

Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!

Huyu fisadi naona ana wasiwasi mkubwa. Kanisa linastahili kuzikataa fedha zake zilizotokana na ufisadi. Huyu jamaa kwanza ni mkristo au ndiyo mfa maji...?
 
kwa kweli hilo kanisa lilipokea fedh ya rostam, ambayo ni ya wizi, watajuta. ni kama vile vipande thelathin yuda iskariote alivyomuuza navyo Bwana wa uzima, YAANI YESU, JINA KUU KUPITA YOTE
 
Hiki ni kiji part tu cha 'operation jisafishe' ya mafisadi lakini mwizi ni mwizi tu, tule hivyo vijisenti vyetu wanavyoturudishia kiaina lakini 2010 sanduku la kura lifanye kazi yake.
 
Hiki ni kiji part tu cha 'operation jisafishe' ya mafisadi lakini mwizi ni mwizi tu, tule hivyo vijisenti vyetu wanavyoturudishia kiaina lakini 2010 sanduku la kura lifanye kazi yake.
Hela chafu itabakia kuwa chafu. Ukiipokea wakati mwingine yaweza kukutia nuksi tu. Lakini simhukumu mheshimiwa moja kwa moja ingawa sijui kama naye ni muumini wa KKKT au kakaribishwa kwakuwa 'anazo' ili awe mwezeshaji kwa shughuli ya kwaya naye akaamua 'kutuma salaam' kwa kumalizia ili waumini waifanye kazi ya kuiombea nchi...!

Angerahisisha angetutajia mchawi nani... Fuatilia Majira la kesho kwa habari zaidi
 
This proves how these people are ready to go to cleanse themselves. But they are wrong, as always
 
Arudishe Kanisani? Hili Bado Litaendelea Kuwa Chukizo Mbele Ya Mungu Wetu, Na Kamwe Hakuna Takayesalimika!
 
Kanisa lishinikizwe lirudishe hizo pesa za fisadi haraka sana, juzi juzi tu makanisa yalikuwa yanakemea mafisadi na ufisadi na kutaka JK awashughulike mafisadi. Leo wanatizama pembeni na kuchukua pesa kutoka kwa fisadi. Viongozi wa Kanisa hilo waache unafiki na kuzirudisha pesa hizo haraka sana au wazipeleke kwenye vituo vya watoto yatima.
 
Nilshawashauri wakiri makosa yao, Waombe msamaha kwa watanzania na warudishe mali zetu!

Kwenda kanisani tu na kutoa pesa ni kuomba huruma bila ya ukweli kuwekwa wazi!

Bado wanaendelea kukataa USHAURI na wasidhani kuwa hiyo kwaya itawasaidia lolote na kudai amani iombwe bila ya kutoa UFAFANUZI WEWE KAMA MTUHUMIWA NI SAWA NA VITISHO!

Na huyo aliyemwalika huko ni nani?

Tunataka HAKI...Tumewapa OPTIONS wao wakafikiri sisi ni wajinga!

Tafadhali viongozi wetu eleweni hilo na kama ni kweli mnataka amani...Then mnajuwa cha kufanya!

Mkiendelea kugangamala na kudai kuwa mnaonewa na huku mkidai amani itapotea na hivyo nchi iombewe na bila kutoa ufafanuzi...

Then naomba nchi iuombee UHURU WETU ILI TUUPATE BILA YA KUMWAGA DAMU!
 
Kuna Mwenye Simu Ya Askofu Dr Malasusa! Huyu Askofu Anachukia Sana Ufisadi, Na Kama Zimetolewa Kkkt Manake Ni Kwenye Himaya Yake. Tumpigie Tumpe Live Kuwa Hili Halikubaliki
 
Kanisa lishinikizwe lirudishe hizo pesa za fisadi haraka sana, juzi juzi tu makanisa yalikuwa yanakemea mafisadi na ufisadi na kutaka JK awashughulike mafisadi. Leo wanatizama pembeni na kuchukua pesa kutoka kwa fisadi. Viongozi wa Kanisa hilo waache unafiki na kuzirudisha pesa hizo haraka sana au wazipeleke kwenye vituo vya watoto yatima.

Nakubali kuwa zirudishwe kwa masharti kuwa zitapokelewa tena MARA BAADA YA RIPOTI ZOTE KUSOMWA NA RAIS KUTOA UAMUZI!
 
Hiki ni kiji part tu cha 'operation jisafishe' ya mafisadi lakini mwizi ni mwizi tu, tule hivyo vijisenti vyetu wanavyoturudishia kiaina lakini 2010 sanduku la kura lifanye kazi yake.

Nina wasiwasi hata 2010 watanzania watarudia yale yale, tusidanganyike na ufahamu wa watu wachache hapa JF tukajua kuwa ndio mawazo ya watanzania, si kweli. Asilimia kubwa ya wapiga kura wako huko vijijini wasikujua ni nini kinaendelea, (rejea watu wote wanaotaka kujisafisha wanarudi kujisafishia vijijini maana wanatambua kuwa kule watu wana imani na chama na viongozi, maana hawajui kilicho na kinachotokea). Hivyo basi usitegemee maajabu sana 2010 unless jitihada za hali ya juu zimefanyika kuwafahamisha wote kuhusu ufisadi huu.
Na hii inatakiwa iwe ni wito kwa wapenda maendeleo wote,vyombo vya habari na watu binafsi kuhakikisha kila Mtanzania ana taarifa sahihi kuhusu ufisadi, mafisadi na madhara yake.......
 
Huyu fisadi naona ana wasiwasi mkubwa. Kanisa linastahili kuzikataa fedha zake zilizotokana na ufisadi. Huyu jamaa kwanza ni mkristo au ndiyo mfa maji...?

Kama ni Hivyo yule kama sikosei ni Zakayo ama Zakaria aliyekua Fisadi wakati wa YESU ,basi kama ni hivyo YESU angewaambia wale Masikini wasipokee zile fedha za fisadi zakayo.

ILa Yesu alimwambia nenda kawagawie mali zako zote za kifisadi masikini na uje unifuate.

KKKT ni moja ya kanisa linalosaidia masikini/yatima moja kwa moja mie bado sioni misingi ya kuzikataa fwedha hizo.
 
Mnakumbuka A Bible Story, Wakati Akina Mitume Walipokuwa Wanatoa Mapepo Na Kukemea Mashetani, Akatoka Mtu Mmoja Akataka Kununua Kipaji Hicho Kwa Pesa? Rostam Anatak Kulinunua Kanisa, Kama Alivyowanunua Akina Makamba, Chitaliko, Serukamba, Jk, Mamvi N.k

Kamwe Aiachwe Akaikebehi Madhabahu Ya Bwana Wa Majeshi, Kwa Visenti Vyake Vya Ufisadi
 
Itakuwaje...?

Waandishi wa habari wanaeneza chuki... Huyu ni mtuhumiwa tu... Hata biblia inasema tusihukumu... Au wengine watasema 'Ambaye si fisadi na atangulie kumrushia jiwe..."

Well, heri mimi sijamhukumu
 
KKKT ni moja ya kanisa linalosaidia masikini/yatima moja kwa moja mie bado sioni misingi ya kuzikataa fwedha hizo.

Fisadi anatenda dhambi ya kuwaibia Watanzania. Kanisa linakemea dhambi za fisadi huyo, halafu linaangalia pembeni na kupokea pesa toka kwa fisadi yule yule ambaye kanisa lilimkemea. Kama huo siyo unafiki sijui ni kitu gani. Kanisa litahalalisha vipi kwa waumini wake kuhusu kupokea pesa toka kwa fisadi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom