Rostam afiwa, tangazo la msiba ni utata mtupu!

TrueVoter

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
2,190
1,766
Nimeshangaa kusoma kwenye gazeti la Nipashe la jana front page, kuna tangazo la rostam kufiwa na ndugu yake wa karibu,

IPP media wameanza lini kutangaza habari za misiba ya watu, tena ikiwa na habari zisizokamilika,
1.Hakuna jina la marehemu

2.Sababu za kifo hazijaelezwa

3. Hakuna tarehe ya Mazishi yatafanyika lini.

Habari hii ilisomwa hata kwenye taarifa ya habari jumapili.Hela hizi zinatufanya tukiuke hata ethics za kuona kama upo umuhimu wowote kwa wasikilizaji kupewa taarifa za msiba wa mtu ambaye hata jina hatajwi!!

Kama hataki jina la marehemu litajwe kawa nini ametaka msiba utangazwe??
 
Last edited by a moderator:
Huu ni upumbavu, kwa nini asingewapigia simu hao jamaa zake kuwataarifu, anatutangazia sisi waTanzania kwani ni ndugu zake? Ingekuwa hivyo asingalituibia. RIP
 
hiyo ni kweli kaka hata mimi pia nimeshangaa sana maana si kawaida kwa mbunge kufiwa halafu ikawa kama ilivyotangazwa yaani ni kama mazungumzo baada ya habari kweli hata hawa IPP media sasa wamechoka.
 
Fisadi RA anatafuta sympathy toka kwa Watanzania.
 
Kwanza haielezwi kafia wapi. Nina wasi wasi huenda huyu Rostam aliwaambia wandishi wake hao wa IPP kuwa kafiwa na ndugu yake huko Dubai ili iwe loop ya kwenda huko kukimbia maamuzi ya Rais baada ya kuhutubia Bunge kesho maana nasikia baadhi ya mambo atakayoyazungumzia ni pamoja na hayo masuala ya kifisadi. Uhamiaji mcheleweshini kidogo kama atataka kwenda Dubai.
 
Bubu Msemaovyo nakupa Big up Mrembo wangu, lazima kutakuwa na kitu hapa kinaandaliwa kwani haiwezekani huyu jamaa atoe tangazo lisiloeleweka, huyu jamaa ni mtu makini sana kiasi kwamba hawezi kuwa na oversight kiasi hicho. Hiyo taarifa kwanza ilikuwa na umuhimu gani wa kutangazwa ikiwa haina jina wala mahali alipofia na alipokuwa akiishi, hiyo tu inatia shaka.

Lakini pia JK hata kama akihutubia hawezi kumgusa RA kwani ni stakeholder wa Ikulu (M-bia), RA anahisa kubwa pale kumzidi JK.
 
Tatizo la wamiliki wa vyombo vya habari hususani vya kielekroniki - Radio na Runinga wanasahau kwamba, masafa ni rasilimali ya umma na kwamba licha ya kuwa wao wamewekeza mitaji, lakini masafa angani ni mali ya wananchi wote na wao wamedhaminiwa kuyatumia ili wananchi wote wafaidike, hii ni pamoja na kufanya kazi kwa maslahi ya umma, kinachotangazwa kama habari, licha ya matakwa mengine ya kitaaluma lakini piwe kiwe na maslahi ya umma, yaani mwananchi kwanza. Niliona hii habari ITV, nilishtuka kama wengine walivyofaynya.

Lakini kingine kinachokwenda sambamba na hili ni la leo asubuhi, kwenye Matangazo ya Asubuhi Njema ya Channel Ten, ambako pia huwa kuna mapitio ya magazeti, Mtangazaji alipokuwa akipitia magazeti ... na kufika kwenye gazeti la Kulikoni na Thisday ... aliruka bila kuzisoma habari kubwa kwenye magazeti haya na ambazo zilikuwa zinaonekana exclusive ....kisa huenda kwa sababu zilikuwa zinamuhusu Manji.

Niliwahi kuona kitu cha aina hii pia kwa enzi zile TVT ambapo habari ambazo zilikuwa zinaonekana mwiba kwa serikali ... zilikuwa zikirukwa.

haya ni matumizi mabaya ya rasilimali za umma -- yaani masafa ... na hili halina tofauti na ufisadi.
 
Mie nimekuwa nikijiuliza sana toka siku nyingi kwa nini hawa jamaa wanatudharau na kutuona siye mandondocha..

I have come to know that hawa jamaa ni marafiki wakubwa,yaani kuna ka circle flani hivi ambako sijui nani alikaanzisha...

ila nchi itabadilika mpaka pale wananchi watakapoamua,ila tukiamua siye tu wachache itachukua muda.Mie nadhani watoto wa Mwanakijiji na wengine waanze kuambiwa mambo yanayohsu mabadiliko.

Ikiwezekana kuweka shheria nyumbani,hakuna kusoma gazeti lolote zaidi ya kijarida cha cheche
 
Wakuu RA ni mbia pale Ikulu. Manji aliombwa abebe mzigo wa RA Kagoda on behalf of RA and Sisiem. Nilishaesema tena kwenye thread zilizopita. Sema moderator haziweki at kwa kuwa mimi ni Junior Member. Mimi naona huyo moderator awe considerate atizame kwanza points na ukweli wake alizoweka member na si suala la "newbornies". Hakuna jipya ala ripoti hii. Subiri kesho utasikia. Au atakachokifanya ni kukandamiza hapo wachache wasio na influence kwa chama na Ikulu. Mungu Ibariki Tanzania na wahindi wake.....
 
Kwanza haielezwi kafia wapi. Nina wasi wasi huenda huyu Rostam aliwaambia wandishi wake hao wa IPP kuwa kafiwa na ndugu yake huko Dubai ili iwe loop ya kwenda huko kukimbia maamuzi ya Rais baada ya kuhutubia Bunge kesho maana nasikia baadhi ya mambo atakayoyazungumzia ni pamoja na hayo masuala ya kifisadi. Uhamiaji mcheleweshini kidogo kama atataka kwenda Dubai.

nadhani umeona mbali, thanx
 
mimi ningependa kujulishwa,huyu jamaa kafiwa na mtu au na kinu cha kutwangia mtama.
 
Hakuna hata haja ya kuangaika na masaibu yanayomkuta fisadi kwani ni malipo sasa je?
 
Back
Top Bottom