Rostam aanza kutikiswa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rostam aanza kutikiswa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amosam, Aug 21, 2009.

 1. Amosam

  Amosam Senior Member

  #1
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  • Akutana na kigingi Igunga
  ZAMA za mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kushinda kinyang'anyiro cha ubunge bila kupingwa ndani ya chama chake, sasa zimefikia tamati, imefahamika.

  Anayejitosa kumaliza himaya ya Rostam ni Deusdedit Mtambalike, mkuu wa wilaya wa zamani na mwanasiasa mwenye msimamo usioyumba.

  Akizungumza na MwanaHALISI kwa njia ya simu kutoka Igunga, mwishoni mwa wiki, Mtambalike alithibitisha kujitosa katika kinyang'anyiro jimboni Igunga katika uchaguzi mkuu ujao.

  Amesema, "Katika hili, hakuna mwenye uwezo wa kubadilisha msimamo wangu."

  Akiongea kwa kujiamini, Mtambalike alisema, "Nagombea. Huyu bwana amezoea vya bure. Nataka hela zake zitumike vizuri," alisisitiza. Alisema tayari yupo Igunga kutekeleza kile alichokiita "Mkakati wa kuwaokoa wana-Ingunga."

  Rostam aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1994 katika uchaguzi mdogo uliotokana na kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Charles Kabeho.

  Tokea wakati huo, Rostam amekuwa akijijengea utamaduni wa kupita bila kupingwa katika uchaguzi, ndani na nje ya chama chake.

  Mtambile ambaye ni hasimu mkuu wa kundi la watuhumiwa ufisadi, amekuwa akitajwa kuwa ni mwiba mkubwa kwa Rostam, kutokana na kukubalika kwake ndani ya Igunga.

  Mbali ya kuwa ni mwenyeji wa huko kwa asilimia mia moja, Mtambalike ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja, ikiwamo kuzungumza kwa ufasaha lugha ya Kinyamwezi ambayo ni maarufu katika eneo hilo.

  Akizungumza kwa kujiamini, Mtambalike alisema, "Mwaka 2000 nilitaka kugombea, akaniomba nimuachie. Akasema hatagombea tena katika uchaguzi wa mwaka 2005. Nikamkubalia," alisema.

  Alisema, "Lakini ilipofika mwaka 2005, Rostam akawachezea wananchi wa Igunga baada ya kubadilika na kuamua kuchukua fomu za kuwania nafasi hii. Safari hii, nimekuja kufuta umungu mtu wa bwana huyu."

  Anasema amejipima na ameona kuwa anazo sifa zote zinazohitajika na kwamba yeye ni zaidi ya Rostam. "Unazungumzia sifa za uongozi, mimi ninazo nyingi. Mimi ni mwadilifu na mwaminifu kwa taifa langu. Hii ni sifa kubwa ya kukabidhiwa jukumu hili," anasema.

  Mtambalike anasema, tofuati na miaka ya nyuma, uchaguzi wa mwaka ujao, utakuwa mgumu kwa Rostam kutokana na wana-CCM wengi kuutamani ubunge wake.

  "Safari hii, mambo hayatakuwa mazuri kwa ndugu yangu. Tuko wanachama wengi wa CCM tuliojitokeza kutaka nafasi hii," alisema.

  Alipoulizwa amejiaandaa vipi kukabiliana na kigogo huyo aliyekwisha jigamba kuwa miongoni mwa "wafanyabiashara wakubwa," Mtambalike alijibu haraka, "Nimejiandaa vya kutosha. Sina fedha, lakini nina watu."

  Alisema, "Hapa ndiyo nyumbani kwetu. Nimezaliwa hapa. Nimekulia hapa. Karibu wapigakura wote wananifahamu, nami nawajua na kuwaheshimu. Sasa unataka nijiandae na nini zaidi ya kuwa mwadilifu," alijigamba.

  Alipong'ang'anizwa kwamba Rostam anajua iwapo yeye Mtambalike atagombea ubunge katika jimbo hilo alisema, "Bila shaka anajua."
  Alipoulizwa Rostam anajuaje wakati yeye hajamwambia, Mtambalike alisema, "Nakwambia anajua. Anajua kwa sababu, wapambe wake wako hapa na wananiona napita vijijini kukutana na marafiki zangu kwa ajili ya kuweka mambo sawa."

  "Nakwambia anajua, lakini hana la kufanya. Hapa ninapozungumza na wewe niko Igunga, tena vijijini kabisa nakutana na marafiki zangu. Watu wake wako hapa, wananiona na wengine nimewaambia hata mimi mwenyewe, kwamba katika uchaguzi ujao, hapa hapatatosha," alisema.

  Taarifa kutoka Igunga zinasema, hali ya kisiasa ya Rostam imeanza kuwa ya mashaka katika siku za hivi karibuni, hasa baada ya Kanisa Katoliki kusambaza waraka unaotoa wito kwa wananchi kujadili wale wanaotaka kuwachagua kuwa viongozi wao.

  Kutajwa kwa Rostam katika mahusiano mbalimbali ya biashara na mikataba yenye utata nchini, kunaweza kuzaa maoni toauti katika mijadala juu ya wanaotakiwa kuchaguliwa kuwa viongozi.

  Rostam amewahi kunukuliwa akisema hatagombea tena ubunge wa Igunga, ingawa taarifa za hivi karibu zimesema amebadili msimamo wake huo na kwamba tayari ameweka makakati wa kutetea kiti chake.

  Mtu mwingine anayetajwa kugombea ubunge Igunga, ni Peter Kafumu, Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini.
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Rostam Rostam Rostam:

  1. Mwenye laana ya watumwa walioachwa wakati mababu zake wakiendesha biashara ya utumwa!!!

  2. Mwenye laana ya vilio vya wanyama wetu waliouwawa kupata nyara!!!

  3. Mwenye vilio vya miti yetu iliyokatwa magogo kupelekwa nje!!!

  4. Mwenye laana ya watanzania kwa kodi zao zilizotumika kulipa gharama za Richmond!!!

  5. Mwenye laana ya watanzania wanaoteseka kwa madhara ya EPA kama master mind akitokomea na bilion 40 za Kagoda!!!

  6. Mwenye laana ya watanzania hasa wanasiasa wazalendo kwa kupenyeza pesa ili kuyumbisha Siasa hasa chaguzi mbalimbali.

  7. Mwenye laana...endelea...
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  swali lililopo mbele yetu? nani atamuidhinisha kugombea hicho kiti wakati RA ndio anachagua wagombea na kuwapitisha kwa kutumia pesa, labda Deusdedit Mtambalike aamue kugombea kwa tiketi ya vyama vya upinzani, ni matumaini yangu anaweza akashinda lakini sio kwa CCM hii iliyopo
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo anatafuta dau la kusafiria tu ,yaani hapo akipelekewa kibegi kilichojaa minoti isiyohesabika ,unafikiri ataenda kugombea ,yaani anapewa nusu akijitoa na kuwacha kuzungumza anamaliziwa dili ,hii ni Tanzania na fedha bado ina cheo mbele ya maisha ya mtanzania anekandamizwa na CCM.
   
 5. c

  chuli Member

  #5
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo sio anayetoa rushwa peke yake ila ni pamoja na anayepokea na kama tunavyojua ni afadhali mjinga sababu ukimfundisha madhara ya rushwa ataelewa kuliko mpumbavu ambae kila siku anaambiwa kwamba kura yake ina thamani kuliko hela, khanga, chumvi n.k lakini haelewi anaendelea kupokea kuchagua mafisadi sasa hapa hata tukisema vipi! Kama hatutatafuta dawa ya upumbavu ni bure!

  Mimi nahisi ufisadi ni tatizo la kiroho hivyo tuandae maombi maalum ya watanzania wote wanaochukia ufisadi bila kujali dini wote tufunge siku nzima tusile ili tumsihi MUNGU atuondolee hili balaa la ufisadi na aondoe upumbavu ndani ya jamii yetu afungue macho yetu na masikio yetu tuone, tusikie, tuelewe ili tuache kupokea na kutoa rushwa!
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Peter kweli wa kule ndanindani wanakovua samaki nafikiri kama Itumba vile or...., Huyu Deusdedit Mtambalike! kazaliwa Igunga....Mhhh sijui! wengine tulimwona tu Nzega akifundisha shule enzi zile na vituko vyake vya enzi za kijana katoka Teachers college, Rostam katokea wapi? bado kitendawili lakini ana vijisenti pia hata kama hatagombea bado anataka kuwa na remote wake Bungeni ambaye kama kweli ataupata ubunge basi JK atampa key position mtu wake ambaye ni wazi Peter Kafumu,
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Salute Mkuu mwiba
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  MMhm..
  Labda wale wenye tamaa ya fedha... na hili ni la mtu binafsi zaidi na sio la kichama?
  Maalim Seif kung'ang'ania uprez kwa miaka 15 sasa ana maana gani?
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hao kina mtambalike usikute wameshalipwa na huyo huyo RA ili ionekane wanamuandama kumbe ndo wanamsafishia njia ya kutoka salama. Sidhani kama RA anataka sana kuendelea kuwa ktk siasa hasa za bungeni so long kwa,mba yupo ktk CC ya chama dume inamtosha sana. Na kwa kuwa ameshaona aina ya ngoma ichezwayo anaweza akawa ameshatafuta wachezaji wake wa kulipwa wacheze ngoma kwa niaba yake.

  Siasa za bongo unafiki mtupu. utakuta mtu anaongea mpaka povu linamtoka lakini moyoni ana lake jambo....
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  msukuma -mhindi wa tabora,tuache kudanganyana jamani......
   
 11. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  duhhh hii kali kwahiyo refa naye anacheza?
   
 12. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  jiwe la mbali aliuhi nyoka mkuu, CC ni kitu kidogo sana ndani ya bunge, bungeni ndiko kunako mambo yote ya ufisadi yanapoanzia na uwezi kuwa na influnce kama huko mbali na bunge na ndio kisa cha bwana RA kungangania ubunge hata baada ya kuomba apewe mpaka 2000tu,
  kwa mtazamo wangu huyu bwana atagombea kwa asilimia kubwa tu
   
 13. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tilishauliza huko 'Asia' kuna wabunge au wafanya biashara wenye asili ya Africa?
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  usanii mtupu, angekuwa mwadilifu asingetamani kutumbukia kwenye dimbwi hilo chafu - angegombea kwa tiketi ya chama tofauti. Tetesi zasema Chakaar hatagombea tena - hana shida na Ubunge, ameshajenga himaya ya kutosha nje na ndani ya Bunge.
   
 15. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Chakaar ndiye RA mkuu?
   
 16. H

  Heri JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ningependa kukubaliana na hoja ya kuwa RA anatafuta exit kwenye politics za Tanzania. Kuna maneno kuwa familia yake haipo Tanzania. Kuwepo kwake CC kuna mpa influence kiasi fulani kwenye system. His popularity/respect among fellow politicians/MP inapungua siku hadi siku.

  Hataweza kukaa muda mrefu Tanzania kwa sababu hatima yake haswa baada ya 2015 haijulikani. Dont be surprised to hear that he has a heart condition
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rostam hatagombea tena Ubunge Igunga, hana muda wala kazi zake haziwezi kumpa nafasi hiyo kwani yupo ngazi kubwa zaidi ya Ubunge..Yeye ni ktk management ya Lowassa kuhakikisha uchaguzi ujao ushindi unapatikana..
  Lowassa ni mbunge hivi lini kahudhulia vikao vya bunge na mara ngapi!.fanyeni utafiti, bado tu hanjaipata picha kamili
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Watu waadilifu wajitokeze kwenye kila jimbo la uchaguzi ambalo hivi sasa linashikiliwa na mafisadi ili tuwe na viongozi bora watakaotuletea maendeleo badala ya kupora utajiri wetu na kutuacha masikini. Pongezi kwa Mtambalike! Yasiwe maneno matupu fanya kweli ili utwae jimbo la Igunga kutoka kwa huyo M-Iran. Hawa akina Rostam wanauogopa sana ule waraka wa Kanisa Katoliki kwa sababu unatoa sifa za uongozi ambazo yeye na mafisadi wenzake hawana! Ndio maana wanampa pesa huyo kibabu mpagani aupige vita.
   
 19. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Umuhimu wa kuwa na wagombea wakujitegemea ndio unapoonekana kwenye sehemu kama hizi; hapa Rostam anaweza kumwaga fedha alizotuibia kupitia Kagoda na wanyamwezi wa CCm kwa njaa yao wakampitisha na kumuacha mtoto wao Mtambalike wakati wa kura za maoni. Kukiwa na independent candidates, Mtambalike ana nafasi ya kusimama tena mbele ya wana Igunga wote ambapo atakuwa na nafasi kubwa ya kumshinda huyu fisadi; mradi Mtambalike asiuze utu wake kwa fedha za huyu bulushi na kuwadhalilisha wanyamwezi!!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Aug 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Bulesi,
  Tatizo la Igunga ni kwamba Rostam hasimami tena kugombea Ubunge sasa utajua vipi kama Mtambalike sii mtu wa Rostam kwani kuponda mtu unaweza kufanya sana na nakuhakikishia wagombea wote wa CCM hutafuta baraka za watu kama Rostam kwanza kabla ya kujitambulisha..
  Msemo wa Lipumba - Hata mtambo mpya unaweza kuwa feki!
   
Loading...