Rosemary Mwakitwwange mbona haya hukumbana mbavu Prof. Lipumba kwa maswali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rosemary Mwakitwwange mbona haya hukumbana mbavu Prof. Lipumba kwa maswali?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Oct 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Mratibu wa mdahalo wa Prof. Lipumba jana alichagua maeneo saba ya kumuuliza Profesa ambayo yalikuwa katika nyanja za utawala bora, uchumi, serikali ya umoja, udini, staili za kampeni za CUF, hatma ya EAC na mikakati ya kiujumla ya kiutekelezaji wa serikali ya CUF katika kuhakikisha sera zake inazitekeleza.

  Mimi sina tatizo la maeneo aliyoyachagua na ninafikiri yalikuwa ni sawasawa tu lakini ni maswali aliyomwuliza Prof. Lipumba ndiyo hayakuweza kutoa picha haswa ya utawala wa CUF utakuwaje na kukosekana kwa kumbana mbavu Prof. Lipumba kulimpa kiburi mgombea huyu hata kudiriki kudai ya kuwa serikali yake ndiyo pekee itakayoweza kuwaunganisha watanzania.

  Kwenye suala la utawala bora, Prof. Lipumba alijikita kwenye sakata la Radar lakini hakuonyesha udhaifu wa vyombo vya utawala bora kama anaufahamu na ataupatia tiba kivipi ili masuala kama ya Radar yaweze kushughulikiwa ipasavyo. Prof. Lipumba alionekana kujiamini yeye kama Raisi angeliweza kushinikiza watuhumiwa wa Radar kufikishwa mahakamani bila ya kuelewa ya kuwa uchunguzi na ushahidi ndiyo mihimili ya kulitendea taifa haki na yeye kamwe sio wa kuzifanyakazi hizo.

  Rosemary Mwakitwange alitakiwa kumhoji Prof. Lipumba juu ya udhaifu wa taasisi za umma katika kuimarisha utawala bora na kwa kutofanya hivyo wapigakura hawajui CUF ina mikakati ipi ya kuimarisha utawala bora.

  Katika masuala ya kiuchumi, Prof. Lipumba alitumia muda mwingi kujigamba ya kuwa yeye amebobea katika uchumi badala ya kulijibu swali aliloulizwa na Mwakitwange ambalo lilikuwa utawala wa CUF una mikakati ipi katika kuimarisha benki za kitanzania dhidi ya ushindani wa kutoka nje.

  Prof. Lipumba badala ya kutuelezea ni jinsi gani ataziondolea benki zetu vikwazo katika ushindani kama vile vya kimtaji, serikali kuwekeza pesa zake kwenye benki hizo na kuzitumia kupata mikopo kila inapoihitaji, kuzipunguzia mzigo wa kodi, ajira kwa wazalendo..n.k

  Rosemary Mwakitwange: Kwa kutombana mbavu Prof. Lipumba kwenye maeneo ambayo alipaswa kuyaongelea alituacha tudhani ya kuwa Prof. Lipumba pamoja na tambo zake kebekebe kuwa yeye ni mwanafalsafa ya uchumi pengine hajui changamoto zinazoikabili sekta ya mabenki yetu hususani ya kizalendo.

  Kwenye serikali ya umoja ambayo ni ngonjera sasa ya CUF, Prof. Lipumba alipaswa aulizwe juu ya serikali hizo zimeonyesha kudhoofisha utawala bora kwa sababu upinzani unakuwa haupo na hivyo serikali haina wa kuikosoa kama vile ilivyotokea Zimbabwe na Kenya.

  Katika suala la udini maswali ambayo watazamaji wengi tungelipenda kufahamu Prof. Lipumba angelijibu nini ni kwenye viwanja vya Mahakama za Kadhi na taifa hili kujiunga na shirika la kidini la OIC ambazo ni sera za CUF. Haya maswali ni ya muhimu kwasababu ndiyo yanaelekea kuipeleka nchi hii njiapanda katika migawanyiko ya kidini ya ukiukwaji wa katiba.

  Kwa kukosa maswali kwenye eneo hili mratibu wa mdahalo huo hakututendea ubinadamu hata kidogo kwani kama CUF wakishinda uchaguzi huu inaamana wapigakura wengine watakuwa wamefanya maamuzi ambayo hayana taarifa hizi za sera hii ya wenzetu.

  Kwenye EAC, maswali ya muhimu yalikuwa ni kipaumbele cha CUF ni muungano wa kisiasa au wa kiuchumi. Hili hatulijui hadi tutakapokwenda kupiga kura. Jingine ni wabunge wa EAC CUF inaonaje kuhusu kubadili ile "TREATY" ili wapigiwe kura ya moja kwa moja na raia. Na lingine swali lilikuwa kuhusu kudhoofishwa kwa muhimili wa kimahakama ambao hauna sauti na kesi za kawaida nje ya TREATY kama kabla ya EAC ya zamani kuvunjwa.....


   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hizo labda ni chuki zako dhidi yake na upendeleo wa kumpenda mgombea mwingine zaidi ya yeye.

  Mimi nimefatilia kwa kina sana midahalo yote miwili ya Dr Slaa na ule wa Prof Lipumba. Kila mtu amejitahidi sana kufahamisha umma kipi atakifanya katika kuondoa wimbi hili la Umaskini wa Tanzania.

  Wote wawili mtaji wao mkuu katika kuinua uchumi wa tanzania ni kuhakikisha mali na rasilimali zote za tanzania zinatumika ipasavyo katika kunufaisha watanzania.

  Profesa alienda mbali zaidi kwa kutoa projection yake ya miaka mitano na ameieka wazi katika manifesto yao kitu ambacho hakuna hata manifesto moja ya chama chochote imeweka projection zao zaidi ya kutoa ahadi.

  Kiuchumi siku zote tunaangalia projection yako kwani hiyo inaonyesha umakini wako katika kufanya tafiti mbalimbali za kuangalia hali ya uchumi na mwelekeao wako.

  nakuomba ufahamu Prof ni Mahili sana katika uchumi na Mgombea mwenza naye amebobea zaidi katika Uchumi. naungana naye Prof kusema namuheshimu Slaa na naweza kumfananisha na Kichuguu lakini Prof ni Mlima.

  Uchaguzi mwema.
   
Loading...