Rose Mayemba, Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe akamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi. Aachiwa kwa dhamana

Kama mbwai na iwe mbwai.
Unamtukana mtu unakula Geda nzuki
Ukidoge Yoko geli ni yako pia
Unamaliziwa na Rear choke
 
Mkuu, mimi binafsi toka siku ya kwanza sikuwahi kuamini kuwa mama will be any different from her predecessor kwa sababu yeye pia ni zao la uchaguzi wa 2020. In those 100 days of her presidency, she was giving just a palliative care, now we're all in for it. Let's wait for the worst
The worst ipi
Watu mnapenda kukuza mambo

maandamano na vurugu sijui km kuna mtanzania anapenda
 
Yaani tunataka kweli kurudi kule kule?
----
Update: 1
JamiiForums imezungumza na RPC Mkoa wa Njombe na amethibitisha kuwa Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe Rose Mayemba amekamatwa kwa Mahojiano zaidi baada ya kuweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii uliomhusisha Rais. RPC amesema kuwa kosa lake lina dhamana na ataachiwa nje ya dhamana.

Update: 2
Rose Mayemba amepata dhamana baada ya kutoa maelezo kwa muda wa saa mbili na kutakiwa kuripoti Ofisi ya RCO Njombe siku ya Jumatatu saa 2:00.


Ujumbe unaodaiwa kumuingiza matatani Rose Mayemba
View attachment 1845997
Hapa kiss ni lipi?
 
Chadema hawa walioshindwa mpaka sasa kusimama na kudai justice for TL (Lissu) mbele ya JPM mpaka sasa..
Chadema hawa walioshindwa mpaka leo kushinikiza wapi alipo Ben Saanane na hatua zichukuliwe kwa waliompoteza au kumuua.
Chadema hawa ambao mpaka sasa hawajui wachukue hatua gani juu ya wabunge haramu walioko bungeni..
Chadema hawa walioshindwa kushinikiza chama chao kutoa bank report yao inayoonyesha hawapokei ruzuku kutoka serikalini kutokana na uwepo wa wabunge wao bandia..

Kifupi CDM bado ni wachanga sana kwenye siasa na kumejaa utoto mwingi saaana...hawapo tayari kupewa dola kama chama mbadala..

..hiyo inamaanisha ccm ni chama chenye hila na kinachodhulumu haki za wananchi.

..na chama cha aina hiyo hakistahili kupewa dhamana ya kuongoza dola.
 
Ujinga Ujinga Tu,Haya Ndio Mambo Pia Ambayo Yalikuwa Yananiudhi Kutoka Kwa Magufuli, Naona Sasa Yanaanza kujirudia Kwa Huyu Mama.
 
Kama ni kweli kwamba Rais Samia Suluhu Hassan amethubutu kuita madai ya Katiba chokochoko basi moja kwa moja hayo mamlaka aliyopewa na Katiba yanamzidi kimo na huo ndio ukweli.

Kama Polisi wamemkamata huyo mwenyekiti wa Chadema, Rose Mayemba kwa dai kuwa kamkashifu Rais, hao polisi hawajui wajibu wao kwa mwananchi raia wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Rais anatakiwa ajitokeze mara moja akemee kitendo hicho cha kukamatwa kwa raia asiye na kosa lolote zaidi ya kutumia haki yake ya maoni aliyopewa na Katiba hiyo hiyo iliyompa Rais mamalaka aliyo nayo.
 
Back
Top Bottom