Rose Mayemba, Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe akamatwa na kuhojiwa na Jeshi la Polisi. Aachiwa kwa dhamana

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,841
Yaani tunataka kweli kurudi kule kule?
----
Update: 1
JamiiForums imezungumza na RPC Mkoa wa Njombe na amethibitisha kuwa Mwenyekiti CHADEMA Mkoa wa Njombe Rose Mayemba amekamatwa kwa Mahojiano zaidi baada ya kuweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii uliomhusisha Rais. RPC amesema kuwa kosa lake lina dhamana na ataachiwa nje ya dhamana.

Update: 2
Rose Mayemba amepata dhamana baada ya kutoa maelezo kwa muda wa saa mbili na kutakiwa kuripoti Ofisi ya RCO Njombe siku ya Jumatatu saa 2:00.


Ujumbe unaodaiwa kumuingiza matatani Rose Mayemba
Mayemba.JPG
 
Rose Mayemba ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe anahojiwa na RCO wa Mkoa huo kwa tuhuma nzito za kumkashifu Rais wa Tanzania kwa kutweet mambo ya Katiba mpya mtandaoni

Tweet yenyewe hii hapa

Rais tayari ameanza kujibu mapigo ya wapinzani,madai ya KATIBA MPYA ameyaita "CHOKOCHOKO"...Hizi ni dalili tosha kwamba uwezo wake wa kuhimili mambo mazito ni mdogo sana.Kuna kila dalili akakosa uvumilivu mapema. Matumizi ya dola hayakwepeki.TUJIANDAE

No_Hate_No_Fear_on_Instagram:_“Taarifa___Mwenyekiti_wa_Chadema_Mkoa_wa_Njombe_@rose_mayemba_am...jpg


Mungu ibariki Tanzania
IMG_20210709_033502_318.jpg
 
Nimegundua kiti cha uraisi ni hot seat , 😀😀😀😀 ni kazi ngumu Zaid ya watu wanavyoifkria , mwingine huko Haiti wamemuwasha risasi ....Ila nafkri viongozi watembee na katiba , wakiona haijitoshelezi wanabadili iendane na matakwa , Ila kuendesha nchi Kwa mlengo unaoona ww unafaa aisee utaishia kupata taabu sana
 
Sioni tatizo kwenye hiyo tweet ya mdada, polisi ndio wanapenda kuleta sintofahamu kwenye mambo yasiyo na maana, tena bora huyo dada kasema Rais hawezi mambo makubwa akimaanisha anayaweza madogo.

Kwangu mimi hata hayo madogo hayawezi, kwani teuzi anazofanya nyingi huzitengua hata kabla ya masaa 24 kupita.

Natumai polisi baada ya mahojiano yao na huyo dada watamuachia huru, muhimu wasimpachike kesi ya upngo kwa kuja kutuambia wamemkuta na Cocaine.
 
Hao POLISI mbona wasikukamate wewe mtoa POST?!!!

Mnaanza UJINGA WENU WA AWAMU ILIYOPITA eee?!!! Si ndio ninyi MAZWAZWA?!!!

#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom