bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,667
Mshambuliaji gwiji huyu amefunguka maneno haya wakati akimshauri kijana Coutinho juu ya uhamisho wake kwenda pale Barcelona.
Ronaldo amefunguka na kusema Barcelona hawana upendo na wachezaji wa Kibrazil akiwemo yeye mwenyewe wakati akicheza ndani ya wababe hao wa pasi nyingi pale jimbo la catalunia,ameenda mbali zaidi na kutaja wachezaji kama Romario,Rivaldo na fundi Ronaldodihno na kusema wote hawa hawajaondoka vizuri pale Barcelona.
Pia ametoa mfano wa siku za Karibuni juu ya kijana Neymar na kusema naye hajaondoka vizuri pale Barcelona na kusema mpaka leo kuna kesi juu ya uhamisho wake kwenda kwa matajiri wa Paris PSG(Paris saint German).
Binafsi napenda soka zuri la Barcelona ila haya maneno ya Ronaldo de lima yameniacha na ukakasi kidogo tukumbuke kijana mwingine wa Kibrazil Paulinho yupo pale Barcelona na amekua akipewa muda wa kutosha tu wakucheza na wakali hao wa Katalunia.
Je maneno ya Ronaldo yanaukweli ndani yake au ni chuki binafsi tu?ni muda wa Coutinho kuamua mbivu na mbichi.