Ronaldinho Arejea Kichovu

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Hatimaye yule kinara wa zamani wa samba, Ronaldinho Gaucho, amerejea jana rasmi kwenye kikosi cha Selecao. Lakini alishindwa kuwathibitishia washabiki wa soka kuwa bado ana kiwango hivyo kupelekea kocha wake kumtetea. Wapenzi wa mchezaji huyo, kina Gang Chomba, wapo kimya baada kukatishwa tamaa na uchovu na ulegelegea wa kiungo huyo mchezeshaji aliyekuwa anasifika kwa kasi na pasi za ajabu wakati wa enzi zake.

Kwa taarifa zaidi soma: Brazil boss Mano Menezes insists Ronaldinho can still cut it - ESPN Soccernet
 
Nawe kama haujaangalia mechi ya jana piga kimya tu! Nakwambia ya kwmb yule mshikaji yuko matawi ya juu kisoccer,kama kweli ungekuwa umeangalia yani ungekuwa na la kuwajuza WanaJF wapenda soccer na usingekuwa umeripoti km ulivyo ktk thread hii ya ku2danganya wadau wa soka. Alipiga faul zote isipokuwa corner moja tu aliyepiga yule dogo foward wa Santos Neymar nyingine yote ilimhusu R. Gaucho.
 
Hatimaye yule kinara wa zamani wa samba, Ronaldinho Gaucho, amerejea jana rasmi kwenye kikosi cha Selecao. Lakini alishindwa kuwathibitishia washabiki wa soka kuwa bado ana kiwango hivyo kupelekea kocha wake kumtetea. Wapenzi wa mchezaji huyo, kina Gang Chomba, wapo kimya baada kukatishwa tamaa na uchovu na ulegelegea wa kiungo huyo mchezeshaji aliyekuwa anasifika kwa kasi na pasi za ajabu wakati wa enzi zake.

Kwa taarifa zaidi soma: Brazil boss Mano Menezes insists Ronaldinho can still cut it - ESPN Soccernet

Inaelekea wewe una chuki binafsi na Dinho au you did not understand what was written in the article. Nakushauri usome tena.
 
tembo (gaucho) hata akonde hawezi kuwa kama sungura (vichezaji vya vyombo vya habari)........................kama uliangalia game kwa makini usingethubutu kunena uliyonena!gaucho fundi
 
Yule mwanasaikatri maarufu, Elisabeth Kübler-Ross, alipata kueleza kwa kina hatua kuu ambazo wanadamu hupitia wanapokabiliwa na hali ya kifo/kufa. Mojawapo ni hatua ya kuukataa ukweli au, kwa Kiingereza, 'denial'. Hii ndiyo hali ambayo mashabiki wa Ronaldinho wanaipitia sasa hivi - hali ya ya kutoukubali ukweli kuwa kiwango chake kiko mahututi na kinaelekea kifoni. Jitihada za kurudisha hicho kiwango zinazidi kugonga mwamba kiasi cha kwamba wataalamu wa soka wameanza kudai kuwa kocha wa Brazili kamrudisha kikosini ili tu aonekane ni mwema kuliko kocha wa zamani aliyefanya maamuzi magumu ya kumuacha kwenye kikosi kilichocheza Kombe la Dunia baada ya kugundua kuwa hana kasi ya kuwachezesha wachezaji vijana na wenye kasi kama Neymar. Wachezaji huja na wachezaji huondoka. Gaucho inabidi astaafu awapishe wenzake.

"Menezes had been accused of using Ronaldinho's recall as a cynical ploy to win over ailing support in Brazil" - Brazil boss Mano Menezes insists Ronaldinho can still cut it - ESPN Soccernet
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom