Ronaldinho anusurika na mashtaka ya utakatishaji pesa na kuendesha magenge ya uhalifu nchini Paraguay, atarajiwa kukiri makosa na kuachiwa huru.

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,448
17,147
Waendesha mashtaka nchini Paraguay wanatarajia kuhitimisha uchunguzi wa kesi ya Ronaldinho baada ya kukamatwa miezi 4 iliyopita na hati bandia ya kusafiria ya nchi hiyo.

Waendesha mashtaka wameshindwa kumuunganisha Ronaldinho na kaka yake kwenye utakatishaji pesa na uendeshaji wa magenge ya uhalifu, Ronaldinho amekua akitoa ushirikiano wa kutosha kwa wanedesha mashataka.

Hadi sasa Ronaldinho yuko jela ya nyumbani, ama house detention, ambako anashikiliwa kwenye hotel ya kitalii baada ya kutoa dhamana ya Dollar laki 8.

Ronaldinho anatarajia kukubali makosa ama plea bargaining na waendesha mashtaka na kuachiwa huru.

Sources: Ronaldinho could get plea bargain
 
Back
Top Bottom