Rombo: Mwili wa Kijana Godwin Massawe wakutwa msituni ukiwa hautoi harufu. Wakutwa ukiwa na Rozari na Biblia

*Nachoona hapa,Godwin alikua na tatizo la akili. Watu wa karibu naye walipigwa upofu na msimamo wake wa imani hivyo wakashindwa kumpa msaada wa kitaalam wa kisaikolojia. Naamini kwamba wanajamii tulishindwa kuwajibika kumsaidia Godwin hivyo tunapaswa kulaumiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna muujiza hapo, suala ni kwamba huyu kijana alienda porini kufunga na kuomba, na akafa kwa hypothermia kutokana na baridi kali ambayo ilimfanya apate kitu kama usingizi akiwa katikati ya maombi na hakuamka tena.

Na suala la kutonuka ni kutokana na uhifadhi wa baridi kali pia - kwani ukiweka vitu kwenye friji vinatoa harufu ya kuharibika?

Watu tuwe na kiasi katika mammbo haya. Tusiwe moto sana wala baridi.
ni muujiza bana
 
Ukonl sahihi mwili wake hauwezi nuka sababu uko eneo la baridi Kali ni kama ulikuwa kwenye freezer kutonuka sio muujiza huo
Kweli mkuu. Wanasahau kwamba kunuka ni kiendo cha kuwa na actve bacteria kwenye mwili wakiula, na kukiwa na baridi hao bactetia wanakuwa inactive.
 
SIMANZI

Godwin Frimin Massawe umeondoka katika Dunia hii lakini Tutakukumbuka na Tutakuombea.Mwanangu Godwin naamini Upo kwa Mungu unatuombea zaidi kwa jinsi kifo chako kilivyotokea. Sijawahi kusikia kifo cha aina hii zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya maisha ya watakatifu. Godiwin alihitimu Kisale secondary 2012,shule ipo mkoani Kilimanjaro wilaya ya Rombo.Alipenda kuishi maisha ya sala,kusoma bibilia kila mara na alifika mahali akasema hakuna anachokitafuta duniani zaidi ya kuishi maisha yatakayomuongoza kufika mbinguni kwa kusoma na kufuata maandiko matakatifu ya bibilia.

Alienda kufanya kazi na Wilvic labour solution kama data entry. Lakin siku moja aliamua kuacha kazi akarudi nyumbani. Alipoulizwa kwa nn alisema "anafanya kazi masaa mengii mnoo mpaka anakosa muda wa kwenda kwenye ibada,kusoma bibilia na kufanya tafakar" aliendelea kusema "kuliko niendelee na kazi ambayo inaniweka mbali na Mungu halafu nikafa naiacha bora niache nikamtumikie Mungu" Akamwambia baba yake nataka kwenda kujiunga na mabrother niwe nasali mda wote. Akapelekwa.Lakini siku moja akarudi nyumban.

Alipoulizwa akasema kule nilifikiri ni sehemu ya kusali, kuimba na kusoma bibilia mda wote kumbe hapana. Bora nirudi nifanye mda wangu wote wa sala. Siku ya jumapili alienda kanisani na hakurudi nyumbani Alitafutwa kila mahali hakupatkana,Taarifa zilipelekwa mpaka kanisan na kituo cha polisi, Ni mwezi sasa umepita.

Jana taarifa za wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu zikasema kuna mtu ameonekana alifariki muda mrefu na ana bibilia. Taarifa zilipotufikia basi baba yake anaondoka na polisi leo kuelekea msituni wakiongozwa na wale wazee wapasua mbao.

Msitu upo Kule katangara,mwisho wa watu kuishi unaingia ndani mwendo wa masaa manne. Kuna barid kali sana na wanyama wakali pia. Ndipo wakamkuta Godiwin amepiga magoti kwenye gogo, akiwa na Rozary yake shingoni na biblia ipo chini imefunguliwa kitabu cha SIRA. Godiwin ameshaoza amebaki mifupa tuu na hatoi harufu yoyote. Amevalia nguo zake vilevile. Godiwin alienda msituni kufunga na kusali mpaka akafariki.

Polisi na baba yake wakamchukua na kumpeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti kule Huruma hospital.

Taratibu za mazishi zinaendelea.Godiwin aliamua kujitoa kutuombea na kusali na Mungu aliamua tunapomtafuta tusimkute mpaka mapenz yake yatimie.Basi ni majonzi kwa familia na wazazi na wahitimu na wanafunzi wa kisale secondary, wananchi wote wa mashati rombo,kanisa Katoliki na watanzania wote kwa ujumla.

Tumuombee Godwin wakati huu akiwa na malaika na watakatifu mbinguni makao ya kusali na kumsifu Mungu milele yote.


------------------
Mwili wa kijana mwenye umri wa miaka 25 umepatikana katika msitu wa Katangara chini yake kukiwa na Biblia, huku ukiwa umevaa rozari shingoni na umepiga magoti.

Kijana huyo, Godwin Massawe, mkazi wa Kijiji cha Msaranga wilayani Rombo ambaye alitoweka Jumapili ya Januari 20 baada ya kuaga kuwa anakwenda kanisani, mwili wake ulikutwa porini Machi Mosi.

Baba mzazi wa kijana huyo, Frimin Massawe aliliambia Mwananchi jana kuwa, baada ya mwanaye kutoweka alitoa taarifa polisi na kanisani ili asaidiwe kupatikana kwake.

“Tulipeleka taarifa polisi mpaka kanisani, lakini hatukufanikiwa. Jana (juzi) nililetewa taarifa na wazee wanaopasua mbao katikati ya msitu (wa Katangara) wakasema kuna mtu ameonekana amefariki (dunia) muda mrefu,” alisema Massawe.

Alisema watu hao walimweleza kuwa marehemu amepiga magoti akiwa na Biblia huku amevaa rozari, ndipo alipoongozana nao kwenda polisi na baadaye msituni.

“Tukafika hadi Katangara na kuingia ndani (ya msitu) mwendo wa saa nne. Kule kulikuwa na baridi kali sana na wanyama wakali, lakini bado niliona maajabu ya Mungu.”

Alisema, “Huwezi amini nilimkuta mwanangu Godwin amepiga magoti kwenye gogo akiwa na rozari yake shingoni na Biblia ipo chini imefunguliwa kitabu cha Joshua huku akiwa ameoza.”

Mzazi huyo alisema mabaki ya mwili huo yalikuwa hayatoi harufu, jambo alilodai kuwa ni ‘muujiza’.

Baba mdogo wa marehemu, Simon Massawe alisema tukio hilo limewashangaza na kama familia wameumia kwa kuwa kijana wao alikuwa mtu wa maombi muda mwingi.

“Sisi kama familia tumelipokea kwa huzuni kubwa, hatukutegemea kumkuta amekufa. Ila kama amekufa kiimani let it be (acha iwe hivyo),” alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mwili wa kijana huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma iliyopo wilayani Rombo.

Mwananchi
Imani ndio msingi wa dini, pia imani ndio kitu chenye nguvu kuliko vingine vyote duniani
Mm naamini dogo aliishi alichokiamini na akafa akiamini ivo ivo...

Apumzike kwa amani mrombo mwenzangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu na wale ambao maisha yao yote ni kutafuta hela tu yani hawana hata muda wa kuzitumia hizo hela wanazozitafuta,kwangu mimi hawa wote naona wana tatizo moja.
 
tatizo la wumini wengi wa kanisa ni kusifu kulikopitiliza, yaani mtu unampa sifa hadi unakufuru. hii ni athari ya uzungu maana ndio mwenye tabia hii, kwa mzungu ukifanya kitu kizuri atakupa sifa za bwana, unabii, ufalme, utume hata uungu.
je kuna uhusiano wa rozary, bible na kutooza kwake, ni kichaa pekeee anaeweza kuamini kuwa ukifa huku umeshika amterial hayo huozi never.
mungu katuumba ili TUMUABUDU je kuabudu ni nini?, jibu ni kufanya ibada.
kila lililokatazwa ukaliacha, ukafanya lilolazimishwa kwetu hii ndio ibada yenyewe. kazi ni ibada lazima ufanye kazi, uzazi ni ibada.
 
Hapa kuna shida kidogo kwenye simulizi, mtu kaoza,kabaki mifupa,lakini, kashika kitabu kimefunuliwa na ana nguo zake.

Au ndo miujiza hiyo?
.......Mara Kaoza halafu kapiga magoti halafu amevaa rozari na nguo zake,mara alikuwa amefungua kitabu cha SIRA mara cha JOSHUA.......mchaganyiko huu kiboko
 
Mimi naomba kujua hicho kitabu cha SIRA ndiyo kipi? Kipo kwenye Biblia ipi, agano la kale au agano jipya?
Sijawahi sikia wala kukiona kabisa aina hii ya kitabu, naomba kueleweshwa tafadhali kwa mwenye ufahamu na kitabu hiki.
Waziri wa Kaskazini
 
48 Reactions
Reply
Back
Top Bottom