ROMBO, KILIMANJARO: Madiwani watatu wa CHADEMA, wawili wakiwa viti maalum wahamia CCM

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Madiwani watatu wa Chadema, wakiwamo wawili wa Viti Maalumu, Martha Ushari na Juliana Malamsha na Diwani wa Kata ya Kilamfua Mokala, Frank Joseph wamejiuzulu na kuhamia CCM wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro leo

=======

Taarifa sahihi zinaeleza kuwa Madiwani hao wanatokea wilayani Rombo na sio Siha kama ilivyotangazwa awali..


Habari zaidi: Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg.Polepole akiwa kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu wilaya ya Rombo amepokea madiwani watatu wa Chadema Halmashauri ya wilaya ya Rombo,

Juliana Malamsha,(Diwani Viti Maalum), Marta Ushaki ( Diwani Viti Maalum) na Frank Joseph Umega(Kata ya kelamfua Mokala Mamlaka ya Mji Mkuu).

Wamejiuzulu udiwani wao na nafasi zao zote ndani ya Chadema na wameomba kujiunga na CCM kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya wilaya ya Rombo na Kikao cha chama kimewakubalia kujiunga na kuwapokea ndani ya CCM.

Na, Nusu ya Baraza la Madiwani Halmashauri ya Rombo wameomba kujiunga na CCM kwa mujibu wa Ndg.Polepole
 
Hapo hasara ni Diwani Mmoja tu,
Hao wengine wacha wakawe "Vitu Maalum" wa CCM
 
Kuhama ama kuhamishwa? Wacha wafanye biashara maanake wengine hawajawahi kuishika milioni kumi cash kwa wakati mmoja! Na hao wabunge njaa wakiziona udenda unawatoka. Kwa hapo siha huyo dk anapigwa bao takatifu asubuhi na mapema kwa taarifa nilizonazo.
 
Madiwani watatu wa Chadema, wakiwamo wawili wa Viti Maalumu, Martha Ushari na Juliana Malamsha na Diwani wa Kata ya Kilamfua Mokala, Frank Joseph wamejiuzulu na kuhamia CCM wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro leo

Chanzo: Mtanzania


Duh, halafu wote ni KLM, hapo sasa, ukiona mpaka KLM wanashuka kwenye Meli ya chadema inayozama ujue hapo hakuna tumaini tena amebakia kapteni tu!
 
Back
Top Bottom