Romantic | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Romantic

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtabaruka, Oct 30, 2008.

 1. M

  Mtabaruka Member

  #1
  Oct 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za leo wakuu, napenda kuuliza ni mambo gani yatakanayo kufanywa na mwanume ili kuwa romantic kwa mwenzake. Noambeni ushauri maana hili swala limekuwa tatizo sana kwenye uhusiano wangu na wife. Asanteni
   
 2. W

  Wakwetu Senior Member

  #2
  Oct 30, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kusilizana ndani ya nyumba na kuheshimiana ndio hasa vikubwa unatakiwa ufanye. Pale unapofanya kosa kiri kweli umefanya na omba msamaha kama linafaa kuomba msamaha. Usiwe jeuri wa kupinga makosa yako.
   
 3. M

  Mtabaruka Member

  #3
  Oct 30, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante, hayo uliyosema nayatekeleza vizuri tuu. Ila mwenzangu amekuwa akinilalamikia sana simuamshi hisia zake inapofikia tendo na ha feel kama kuna upendo wangu kwake. Pengine kufafanua vizuri mimi huwa na choka sana na kazi maana huanza mchana na kumaliza 6 usiku kila siku J´tatu mpaka Ijumaa. So huwa inapita kama one week hivi bila kufanya. Sasa hili limekuwa likimkosesha raha sana mwenzangu. Yeye kwa sasa hivi anasoma chuo tuu.
  So nimgependa kupata maoni ni jinsi gani nitakavyoweza kumridhisha mke wangu nampenda sana.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Kaka, honestly katika masuala unayotakiwa kuyapa msisitizo mojawapo ni hilo la kumpa mkeo haki ya unyumba regardless how busy you are. Unatakiwa kuwa makini sana hiyo hali ya mkeo kukulalamikia kuwa hafurahii tendo hilo kwa kuwa wewe unakuwa unachoka sana linaweza kuwasababishia mtafaruku ndani. wanawake ni wepesi kushawishika kutoka nje ya ndoa yake ili kutafuta faraja ya kimapenzi. Kwani mkeo hataamini kama wewe kweli unachoka kwa kazi bali atajua kuwa una nyumba ndogo ukiwa huko unapata mapenzi ya hali ya juu then ukifika kwake unatimiza wajibu tu lakini si kumpa mkeo mapenzi kwa kiwango cha kumridhisha. So mzee pamoja na kazi zako nyingi jitahidi sana kupanga muda ambao utautumia kumpa raha mkeo otherwise ndoa yako itayumba. Kuna wanaume wako midomo wazi kama mamba kusubiri akina mama waliokuwa heart boken na waume zao then wawape faraja na jamaa wakikamata mzigo demu anaweza kuhamia kabisa huko!!!!!!!!!!!!
   
 5. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pole sana mkuu,kwakweli kuhusu kuchoka na kazi nakuhurimia ,maana nalielewa hilo,kwakua yeye anasoma tu ingemfaa yeye akubembeleze hiyo jtatu mpaka ijumaa,kwakukufanyia massage na mabusu motomato etc...sasa nimesoma una jumamosi na jumapili,hizo siku mbili zinatosha kabisa kwa wk,asubuhi amka kwa kumtengenezea kikombe cha chai ya rangi au kinywaji apendacho,ikiwezekana ,muogeshe hiyo siku kwa mapenzi makubwa (kama mnaishi kwenye nyumba yenu),then hapo atakuwa amepata mood nzuri,mnaweza endelea zaidi.kama hatakuwa na assignment then mchana mnaweza kutoka na kwenda kula nje,or usiku mtoke wote mkapate dinner,or sehemu anayopenda mke wako,

  in between ,hasubuhi si uko home ww,then mchagule nguo ya kuvaa,mvalishe ikibidi,mtumie text kila wakati zenye maneno matamu,mbona wanawake ni rahisi yu,wewe mpe maneno matamu kwasana,natumaini unayajua jamani,mengine baadaye .
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kaka, usichoke basi japo kumpiga mabusu ukitoka/ukirudi nyumbani, ikiwezekana hadharani kama mpo pamoja, na wala usione tabu kumshika mkono mkeo hadharani, si umemlipia mahari bwana?...

  ...kuchoka kusikupelekee ukalala bila kumpa mabusu mkeo, na jifunze kulala ungali 'umemfunga mkanda' mkeo (umemkumbatia), mambo ya kulala mzungu wa nne, au nyote mmgeukia ukuta wake siyo 'Romantic' kama asemavyo huyo mwali...

  ...kuongeza chachandu, mwambie basi akukande/masaji kabla hujalala upatwe nawe kupunguza machovu, huenda kwenye hilo kukakuamshia hisia, ama?

  natumai mchango huu utakusaidia japo kidogo...
   
 7. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60


  mhhhhhhh hii theory utaleta ugomvi bure humu, wasiolipiwa mahari je?
   
 8. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Ndugu Mtabaruka
  1.Wanawake ni watu wa hisia sana ndio maana anaweza kukwambia haupo romantic ukashindwa kuelewa. Na wanaume hufikiri kununua chakula, kujenga nyumba na kutoa hela ndio vitajenga mahusiano ya ndoa. Jaribu hatua hizi chache

  2.Mkumbushe mkeo mara kwa mara kuwa unampenda, kwa txt msg, mkiwa peke yenu n.k. Waume wengi hufikiri baada ya kuoa mke hapaswi kuambiwa maneno aliyokuwa akiambiwa wakati wa uchumba. Wakishaoa basi wao na kazi kazi na wao. Roomantic life ni ongoing process haifi ila una renew every now and then.

  3.Hata ukichoka kumbusu,kumkumbatia, kumshika mkono kwatosha.

  4. Wanawake hupenda wanaume wanaowauliza uliza: muulize siku yake imekwendaje, kakumbana na kipi na kama asubuhi alikuambia atakuwa na test, follow up how the test was.

  5.Unapopata nafasi weekend hapo sasa mpumzike pamoja.
  Usisahau zawadi ndogo ndogo like chocolate, handerchief, kibanio cha nywele au chochote unachohisi kinachomu-impress. Kina mama wanapenda sana vizawadi na dio maana anasema haupo romantic, hata kama unampa hela ya kutumia si vibaya siku ukimnunulia night wear nk


  6.Hata kama mna watoto treat her like those old days na si kama mtu aliyezeeka wewe saa zote mama fulani, let her continue being your darling, your sweet rose n.k
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi mdekeze ili umuonyeshe kwamba you care about her. Siku moja moja kama pochi linaruhusu (weekend) mwende kula nje wanawake wengi hupendelea dinner katika mahoteli mazuri lakini ambayo bei zake ni poa. Pia ukumbuke kununua Valentine card (February 14 siku ya wapendanao) na siku zake za kuzaliwa na pia siku za anniversary zenu na kama ikiwezekana mkaenda kusherehekea kwa kula nje. Ni vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji kuvunja bank ili uweze kumudu gharama zake.
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Weekend moja moja unampa huduma ya malkia,unaamka asubuhi na kutayarisha kifungua kinywa,kama unajua kupika unampikia chakula cha mchana au usiku na kumkalisha kwenye kochi[miguu yake unamwekea mto kwenye stuli]na kumnawisha na kumletea kila kitu yeye asiamke pale.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu jikaze lasivyo wenzio wataanza kukuchapia nje shauri yako.
  Kazana kula protein ziamshe munkali kama karanga mbichi kama unakunywa jaribu kubost kidogo na karanga mbichi angalau mara 2 kwa wiki jiwekee ratiba hata kama umechoka una mlidhisha mwenzio.
   
 12. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu,kila mtu anaromantica kivyake,mfano,mm huw sitaki makuu,ukifanikiwa kuniongelesha kwa upole kila wakati ,nakunirespect,like kuniambia ratiba zako kila siku ,pamoja na kuwa mkweli ,basi mm hiyo tosha,so kwakukusaidia zaidi,peleleza anapenda nn huyo mke wako,so na wewe uma palepale.
   
 13. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Dadangu hiyo ya kutoa ratiba yangu ya kila siku itakua ngumu sio kwamba nafanya kitu kibaya lakini nahitaji uhuru wakujipangia mambo yangu nakubadili ikibidi,kama ntachelewa kurudi homa nitakujulisha hiyo ni haki yako.
   
 14. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [Dadangu hiyo ya kutoa ratiba yangu ya kila siku itakua ngumu sio kwamba nafanya kitu kibaya lakini nahitaji uhuru wakujipangia mambo yangu nakubadili ikibidi,kama ntachelewa kurudi homa nitakujulisha hiyo ni haki yako)

  ohh,ss hapo hatutaelewana kwakweli,mambo ya kuvizia ,eti leo una ratiba hii,mi nachopenda ,uniambie tu leo nitachelewa napita...,na sio unakurupuka tu na kujiendea unapotaka,basi hata nitextie basi,ninapata moja moto moja baridi,mhh hapo hapana.
   
  Last edited: Nov 1, 2008
 15. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  L,nimecheka mpaka basi,yaani kunijulisha tu jamani,na hiyo ndicho nachopenda,wala sina makuu jamani.
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kukujulisha nitafanya kwa simu au hata sms nachoongelea ni ile kukuambia asubuhi kuwa leo jioni nitachelewa,mara nyingi plani hizi huanzia mchana rafiki ananipigia simu kuna kitu muhimu anataka tujadili au hatujaonana siku nyingi anataka tukutane kisimani(watering hole) ku-touch base.Nakuhakikishia huko nitakula kwa macho tu uko peke yako.
   
 17. L

  Ledwin JF-Expert Member

  #17
  Nov 2, 2008
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 227
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nimekuelewa,Lagatege,ia jamani,inabidi unamshtua mwenzio jaman,roho inauma ww ,ukijiamulia tu kwenda popote
   
 18. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  swadataa...!
   
 19. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #19
  Nov 7, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii haijakaa sawa, kama ndugu yangu unayaweza haya basi ndoa yako ni poa kabisa!
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Nov 7, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama walivyochangia BAK,Ledwin na wengineo , ni mambo madogomadogo sana ambayo hayahitaji gharama kubwa.Kikubwa ni wewe kujua mwenzio anapenda nini maana one person's fish is another person's poison.Siyo kila jambo kwenye mahausiano unaweza ku cut & paste.Binadamu tunatofautiana.
  Hilo la mambo ya chumbani - zingatia ushauri uliopewa usifanye masihara maana kinachotofautisha uhusiano wa mke na mume na mahusiano mengine ni hilo na si kingine.
   
Loading...