Roman Charity: Story ya kusikitisha yenye upendo

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Unaweza kudhani picha hii ina Maudhui ya Ngono lakini sio, Picha hii ni alama ya kitu ambacho kwa sasa kinaitwa "Roman Charity"

Ilianzaje Roman Charity?

Hapo zamani katika roma ya kale (Acient Rome) aliishi mzee mmoja anaitwa Cimon, mzee hakuwa na ndugu Zaidi ya binti yake aliyeitwa Pero.

Ilitokea Cimon akafungwa kifungo jela bila kula mpaka afe.

Kwa kuwa mzee hakuwa na ndugu mwingine Zaidi ya binti yake Pero, binti yake aliomba sana apate nafasi ya kuonana na baba yake, alikataliwa mara nyingi ila hatimaye alikuja kukubaliwa.

Alikubaliwa kwa sharti moja kwamba hatakiwi kuingia na chakula chochote. Maaskari walimkagua kabla hajaingia kuhakikisha hana chakula.

Baada ya kuiona hali ya baba yake Pero alishindwa kuzuia chozi lake, baba yake alidhoofika mno kwa kukosa chakula, na alitakiwa afe.

Screenshot_20200721-123523.jpg


Pero alimwangalia baba yake kwa jicho la huruma kama mama, Binti pero alikuwa mzazi akiwa na mtoto mchanga, ili kuokoa maisha ya baba yake akaanza kumyonyesha kila siku baba yake mpaka akapata afya tena.

Walinzi walishangaa sana kwanini Cimon hafi pamoja na Kupita siku zote hizo? Wakaanza kumpeleleza binti yake Pero.

Siku moja wakamfuma akimnyonyesha Baba yake, wakamkamata na kumpeleka kwa bwana Jela, bwana Jela alimwachia huru Cimon baada ya kuona upendo wa aina yake uliooneshwa na Pero ambao hakuwahi kuuona kabla.

Mapenzi ya wazazi kwa watoto ni kawaida, ila ya watoto kwa wazazi ni mara chache, na mara nyingi ni watoto wa kike wanaoweza kuonyesha upendo wa aina hiyo!
 
Back
Top Bottom