Roman Abramovich: Utajiri wa Damu, Risasi na Umafia

ROMAN ABRAMOVICH: UTAJIRI WA DAMU, RISASI NA UMAFIA


SEHEMU YA TATU



Uchaguzi ulikuwa unakaribia, wananchi walionekana dhahiri wanaegemea upande wa mkomunisti Zyuganov. Taarifa hii si kwamba ilikuwa mbaya kwa Rais Boris Yeltsin pekee bali pia na genge lake lote la “The Family” kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba kama ikitokea mkomunisti Zyaganov akichukua nchi kitu cha kwanza ambacho angekifanya ni kurejesha serikalini viwanda na makampuni yote ambayo yalikuwa yamebinafsishwa na Rais Yeltsin kwa watu binafsi.Hakuna ambaye alikuwa na jawabu kichwani wa nini hasa wakifanye kunusuru kile ambacho kilikuwa kinaelekea kutokea… baadhi ya watu kwenye inner circle wakamshauri Rais Yeltsin afute uchaguzi na atawale nchi kidikteta. Lakini hili lilikuwa ni wazo la kipuuzi kabisa labda kutokana na maji kuwafika shingoni maana mfumo huu ulikuwepo Russia huko mwanzoni miongo kadhaa nyuma na ukafeli na kudondoka.



Wakati ambapo kila mtu akiwa amechanganyikiwa na kutoa mawazo yasiyo na mbele wala nyuma kuleta auheni yoyote ndipo ambapo Abramovich akaingilia kati. Akakaa mstari wa mbele na kushika usukani wa mikakati ya uchaguzi kambi ya Rais Yeltsin. Russia ilikuwa imetoka kwenye ujamaa na ubaya ni kwamba ile akili ya kijamaa bado ilikuwa haijawaisha. Kama wasemavyo, unaweza kumtoa kijana kutoka ‘nanjilinji’ kuja mjini lakini kamwe huwezi kuitoa ‘nanjilinji’ akilini mwa huyo kijana. Nchi ilikuwa imeingia kwenye ubepari lakini wazee bado walikuwa wanawaza na kufanya mambo yao kama wajamaa. Abramovich akataka kuwaonyesha namna ambavyo chaguzi zinafanyika kwenye nchi za kibepari.



Kwanza akamshawishi Rais Yeltsin amfute kazi meneja kampeni wake. Kisha nafasi hiyo akashauri apewe mtoto wa Rais Tatyana. Kwa nini? Kwanza kwasababu Tatyana atakuwa na uchungu zaidi na kampeni hiyo kwa kuwa ‘ana kitu cha kupoteza’ kama wasiposhinda. Lakini pia kama ambavyo nilieleza kuwa Tatyana hakuwa binti legelege wa kula mkate kwa siagi tu, bali alikuwa ni mpambanaji haswa. Lakini tatu Abramovich alitaka Tatyana ashike wadhifa wa meneja kampeni kwa kuwa alikuwa rafiki yake na walau alikuwa kwa mbali Tatyana alikuwa ameanza kuwaza nama ambavyo yeye Abramovich anawaza. Wanasema ukikaa karibu na waridi lazima unukie.



Kisha Abramivich akafanya kitu ambacho kwa kipindi kile nchini Rusia hakikuwa kimezoeleka sana japo kwa nyakati zetu hizi twaweza kuona ni cha kawaida. Abramovich akatengeneza mkakati wa namna ya ‘kucheza’ na media.

Jambo moja ambalo tunapaswa kulifahamu ni kwamba katika kipindi hiki kutokana na udhaifu mkubwa wa mbinu za uongozi za Yeltsin, uchumi wa Russia ulikuwa umeyumba sana kiasi kwamba mpaka serikali ilikuwa imechacha kweli kweli. Serikali kwa kipindi hicho ilikuwa inajiendesha kwa kutumia fedha za mkopo dola bilioni kumi ambazo serikali ilikuwa imekopeshwa kutoka IMF.

Sasa basi, vituo vya televisheni vyote ambavyo awali vilimilikiwa na serikali vilikuwa navyo vimebinafsishwa. Kwa hiyo hata serikali ikitaka kurusha matangazo walikuwa wanapaswa kulipia. Lakini serikali ilikuwa imechacha.

Abramovich akaitisha kikao maalumu na watu ambao walikuwa wamebinafsishiwa vituo vya habari nchini Russia na hata wale ambao wamejitutumua kuanzisha vya kwao wenyewe. Abramovich alikuwa na ombi moja tu kwao… waache kurusha habari yoyote kumuhusu Zyuganov, mpinzani mkuu wa Yeltsin ambaye alikuwa anaongoza kwenye kura za maoni na badala yake vyombo vyote vya habari virushe habari kuhusu kampeni za Rais Yeltsn.



Abramovich akawaeleza kwamba atafanya kila namna mpaka Rais Yeltsin ashinde kiti cha Urais na akishashinda ‘atawakumbuka’ wamiliki hao wa vyombo vya habari kwa hicho walichokifanya.



Hakuna mmliki yeyote wa chombo cha habari ambaye alikataa ‘ofa’ hiyo. Hakuna ambaye hakutaka ‘kukumbukwa’ pindi ambapo Yeltsin akishika muhula mwingine.



Katika kundi hili la wamiliki wa vyombo vya habari ambao Abramovich alikuwa anamlenga hasa alikuwa ni swahiba wake wa zamani Berezovsky. Yule Oligarch ambaye alimtambulishaga kwa Yumachev. Berezovsky alikuwa anamiliki ‘media house’ ambayo ndiyo ilikuwa ina ushawishi kuliko vyombo vingine vyote. Sio tu kwamba alikuwa amemlenga kwa kuwa alikuwa na media house yenye nguvu zaidi, Abramovich alikuwa na wazo lingine la siri zaidi, wazo mwanana kabisa ambalo kama likitimia basi laweza kumfanya ghafla kuwa moja ya watu matajiri zaidi nchini Russia na duniani. Nitaeleza baadae…



Kampeni ikaendelea… kufumba na kufumbua, kila televisheni, kila redio, kila gazeti kila siku kukicha kulikuwa na habari moja tu, Boris Yeltsin, Boris Yeltsin, Boris Yeltsin. Tofauti na ambavyo Yeltsin alikuwa amezoeleka kwamba sio ‘mtu wa watu’ lakini ghafla Yeltsin alionekana akiwa na haiba nyingine mpya kabisa. Kila siku yuko mahala fulani… leo ametembelea shule fulani ya upili Moscow, kesho yuko sokoni akisikiliza shida za wachuuzi, kesho kutwa yuko kiwanda fulani akila chakula cha mchana na wafanyakazi. Warusi walishuhudia Yeltsin mpya ambaye hawakuwahi kumuona. Yeltsin akaongeza ruzuku kwa wanafunzi, akatoa fedha nyingi kutoka serikalini mabilioni kwa ajili ya kuwalipa pensheni wazee. Na kila hatua, kila kitu haijalishi ni kikubwa au kidogo ndogo kiasi gani kiliripotiwa na kila chombo cha habari nchini Russia.



Vyombo vya habari vilimpamba kwa kila namna ambayo waliweza huku wakiwaeleza wananchi kwamba wakimchagua Zyuganov kutokana na sera zake zinaweza kuifanya Urusi kuingia kwenye vita.



Mara moja mikutano ya kampeni ya Yeltsin ikaanza kujaa watu kwa mafuriko. Yeltsin akageuka kuwa ‘sweetheart’ wa Warusi wote. Katika mikutano Yeltsin aliongea kama mtu muungwana tofauti na kawaida yake ya kufokafoka kama jendaheka. Aliongea kwa ustaarabu na kumwaga ahadi kedekede.



Siku ya uchaguzi ikawadia, December 5, 1996. Kura zikapigwa. Siku moja mbele matokeo yakatangazwa… Boris Yeltsin alikuwa ameshinda kti cha Urais kwa kupata 52% ya kura zote zilizopigwa. Yaani kama mtu alikuwa amelala usingizi miezi mine nyuma na kuamka siku hiyo umwambie Yeltsin alikuwa amemshinda Zyuganov angeweza kukuona ni mwendawazimu.

Yaani ndani ya miezi mine tu, ‘adacadabra’ za mikakati ya Abramovich zilikuwa zimebadili mioyo ya warusi kumchukia Yeltsin na sasa kuwa ‘sweetheart’. Ilikuwa nikitu ambacho hata Yeltsin mwenyewe hakutegemea.



Baada ya Yeltsin kuapishwa kushika muhula mwingine wa uongozi watu wa kwanza kuhakikisha wanapata ‘mnofu’ mnono zaidi walikuwa ni ule Utatu Mtakatifu. Tatyana, Yumachev na Abramovich. Tatyana akateuliwa na baba yake kuwa rasmi mshauri wake mkuu. Yumachev akateuliwa kuwa katibu Mku Kiongozi… na Abramovich… naam Abramovich akateuliwa kuwa nani? Waziri Mkuu? Hapana… Waziri wa Mambo ya Nje? Hapana… Waziri wa Ulinzi? Hapana… aliteuliwa kuwa nani?

Abramovich alikataa kupewa nafasi yoyote ile ndani ya serikali. Uwendawazimu? No… Abramovich, a born tactician… anaona kile ambacho wengine hawakioni.

Alimweleza tu Yeltsin kwamba ameshiriki namna ile katika uchaguzi na kuhakikisha anashinda kwa kuwa anampenda Yeltsin kama baba yake kabisa na anadhani ndiye mtu sahihi zaidi kuingoza Russia.

Moyo wa Yeltsin ukamomonyoka na kububujikwa kabisa… hakika huu ni upendo wa kuzidi kipimo, mtu anakupigania kwa jasho na damu ushinde kiti cha Urais alafu hataki umlipe kwa kumpa cheo chochote? Yeltisn akajihisi kama amepata mtoto wa kiume ukubwani… tena mtoto mtiifu na mwenye kumpenda baba yake.



Japokuwa kipindi hiki Abramovich hakuwa tajiri kabisa hata kidogo kama tumjuavyo sasa, lakini Abramovich alikuwa anajua ni nini anakitaka… hakutaka papara ya kurukia vyeo vya serikali… alijua lengo lake hasa liko wapi. Kila kitu sasa kilikuwa kiko sawa, mkakati wake umeenda vile ambavyo alikuwa amepanga. Kitu pekee alichohitaji sasa ilikuwa ni subira… naam, subira… subira ni ‘necessary ingredient of genius’.



Akasubiri serikali iundwe. Wagawane vyeo. Walioukwaa uwaziri na ukuu wa maidara washerehekee na kupongezana, kisha aingie ‘kazini’.



Miezi kadhaa ikapita… serikali mpya ikiwa imeshaundwa na imetengemaa na inafanyakazi zake kama kawaida. Huu sasa ulikuwa ni wakati muafaka aliokuwa anausubiri.



Siku hiyo miezi ya mwanzoni kabisa mwa mwaka 1997 akampigia simu yule swahiba wake wa zamani, Bw. Berezovsky. Yule jamaa mwenye media house yenye nguvu zaidi kipindi kile nchini Urusi, ambaye pamoja na wamiliki wengine wa vyombo vya habari kipindi kile cha kampeni Abramovich aliwaomba wamsaidie Yeltsin kushinda kiti cha Urais na kuwaahidi Yeltsin atawakumbuka kwenye utawala wake.

Alipompigia simu na Berezovsky kumuuliza wanakutana kwa lengo gani…. Akamjibu jibu moja tu kwamba, “muda wa Rais kuwakumbuka umewadia.!”

Boris hakujua na hakuna ambaye angeweza kujua zaidi ya Abramovich mwenyewe kwamba, ndani ya wiki chache baada ya simu hiyo Abramovich alikuwa anaelekea kuwa moja ya binadamu mwenye utajiri mkubwa zaidi juu ya uso wa dunia.





Naomba mniruhusu leo saa tatu na nusu usiku niweke sehemu ya nne.







The Bold - 0718 096 811

To Infinity and Beyond
Hivi mkuu, wewe ndio uliye andika story kumhusu Raisi wa nchi ya Rwanda Mh. Paul Kagame na kusomwa na Dulla Planet mnamo mwezi wa tano mwishoni au wa sita mwanzoni kwenye radio station?
 
Du, yupo vizuri. Afanye mpango tuipate hapa JF


Sio hii hapa??..ila haikufika mwisho....huyu mkuu ni noma boss

 
Sio hii hapa??..ila haikufika mwisho....huyu mkuu ni noma boss

Sina uhakika sana sababu sikuifuatilia vizuri kwa kuwa ilikuwa ikiruka hewani mida ya asubuhi kwenye saa 1 hadi 2 hivi
 
The bold kaka upo wapi? tuna shauku huku tupe update ya sehemu ya tano mkuu
 
SEHEMU YA TANO:

Yuri Skuratov aliporejeshwa kazini na bunge kiburi kikamjaa zaidi… akaitisha mkutano mwingine na wanahabari na kuwaeleza kuwa ana ushahidi wa kutosha dhidi ya Roman Abramovich na Berezovsky na anakusudia kuwafungulia mashtaka ya kuhujumu uchumi. Watu wa system walifurahi kweli kweli wakijua huo ndio mwisho wa Abramovich… kama wangelijua kipindi kile Abramovich ni mtu wa namna gani wasingelithubutu kumtikisa. Walikuwa wanapima kina cha bahari kwa goti la mguu…
.
.
.
.
Naisubiri kwa Hamu.
 
Back
Top Bottom