Roman Abramovich: Utajiri wa Damu, Risasi na Umafia

View attachment 1176753


Wakuu sana, nimewakumbuka… nilijipa likizo ya karibia mwaka mmoja sikuwepo humu. Uzee unaninyemelea na majukumu yanaongezeka, kwa hiyo ni busara sana kujipa mapumziko ili kukimbizana na ratiba katika maisha halisi nje ya mitandao.
Yote juu ya yote… nimewakumbuka mno.

Mniwie radhi sana kwa kushindwa kuimaliza makala ya “The Richest Man in Africa” pamoja na “Ujasusi Sebuleni Kwetu”.
Kwa namna upepo unavyovuma hapa nchini kwa sasa sidhani kama ni muda muafaka kuendeleza ule mjadala…tusubiri kwanza upepo utulie kidogo na ikimpendeza Mwenyezi Mungu basi tutamalizia.

Kwa muda huua mbao sikuwa hewani nimekuwa na tafakari nyingi sana na hizo tafakari zimepelekea kuandika makala nyingi. Kwa wale ambao niko nao kule ‘nyumbani kwangu’ WhatsApp nime-share nao makala kadhaa ambazo sijawahi kuziweka humu kwa kipindi hiki ambacho nilikuwa kimya.

Leo kama siku ya kurejea kwangu tena hapa jukwaani nimeonelea niwashirikishe moja ya tafakari ambazo nimeweka kwenye maandishi kuhusu moja ya masuala yanayotutoa jasho na kutufanya kuamka saa kumi na moja asubuhi kukimbizana na jua… kutengenza utajiri.
Tafakari hii tutaenda nayo mpaka mwisho pasipo kuishia njia. Ni andiko refu sana lakini nitaliweka mpaka mwisho kwa ‘episodes’.


Tafakari hii nililianza nikiwa najiuliza moja ya maswali ambayo yawezekana wote humu kuna wakati umewahi kujiuliza na pengine kujijibu…



HOW TO BECOME A BILLIONARE.?


i)Invent – kama una uwezo mzuri wa kiakili buni kitu kipya ambacho kitakuwa na uhitaji mkubwa kwenye jamii.

ii)Innovate – tafuta kitu fulani, bidhaa au huduma na kisha boresha ufanisi wake au ufanyikaji wake na kisha ifanye kibiashara huduma hiyo au bidhaa.

iii)invest – tafuta biashara au kampuni ambayo………


Wrong..!!

Haya ndiyo majibu ambayo bila shaka yanatujia vichwani endapo tukipatwa na ndoto za labda siku moja kutengeneza utajiri wa kuzidi dola bilioni moja za kimarekani. Tunafikiria kufanya bunifu, kuboresha huduma, kuwekeza au kuwa wajasiriamali. Mbaya zaidi tunaamini kwamba yeyote yule ambaye amefanikiwa kuupata utajiri wa kiwango hicho cha ‘kufuru’ basi twamuhusudu kwamba ni mfanyabiashara au mjasiriamali nguli na hodari au labda ni mbunifu au mgunduzi mwenye akili iliyopitiliza. Nimekuwa nikiamini hivi pia kwa miaka mingi sana huko nyuma, nakumbuka nikiwa mwanafunzi wa sekondari niliwahi kutawaliwa sana na ‘wehu’ wa kutamani sana siku moja kuwa billionaire. Kuna jamaa mmoja muhindi alikuwa na duka maeneo ya upanga UN road la kuuza vitu kwa rejareja. Nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Castro, basi tulikuwa tukitoka shuleni tunapita mara nyingi sana dukani kwake kwa ajili ya kuchukua jarida la Forbes. Dukani kwa huyu jamaa ndio mahalapekee ambapo kipindi hicho nilikuwa nafahamu naweza kulipata jarida la Forbes. Nakumbuka namna ambavyo ungeniona kipindi kile macho yakijawa na tabasamu pindi nikishika tolea jipya la Forbes… namna ambavyo nilikuwa makini kufuatilia orodha ya matajiri wakubwa zaidi duniani… kipindi kile ningeweza kukutajia mabilionea wakubwa wa dunia kutoka kichwani kuanzianamba moja mpaka namba thelathini, majina yao, kiwango chao cha utajiri na majina ya kampuni zao… unguli wa Carlos Slim, Buffet na Gates… historia za kusisimua za kina Lakshmi Mital… kuibuka kwa kina Aliko Dangote na Mike Adenuga ambao walikuwa ni ‘newbies’ kipindi kile kwenye orodha ya Forbes. I loved it… breathed it, nilisoma Forbes kama msahafu na ikanipa ndoto za ajabu… kutamani kwamba niumize kichwa na kufanya gunduzi moja matata sana ya kunifinya siku moja kuwa na ukwasi huo kufikia dola bilioni moja za kimarekani.

Lakini kadiri ambavyo miaka iliongezeka na kuanza kufunguka macho kuelewa mfumo na mwenendo wa dunia nikaelewa kwamba kuwa bilionea ni kitu ambacho kinahitaji zaidi ya talata ya biashara, zaidi ya ujasiriamali na zaidi ya kufanya gunduzi au bunifu murua. Unaweza kuwa tajiri, unaweza kuwa milionea kwa kufanya gunduzi au bunifu makini au kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali makini. Lakini kufikia ukwasi wa ubilionea… sio ubilionea kama ule wa Arusha wa kununua Nissan Patrol na kuwa na nyumba Njiro kesho kila mtu mtaani anakuita bilionea… hapana, naongea kuhusu ubilionea halisi wa ukwasi wa kuzidi dola bilioni moja… zaidi ya shilingi trilioni mbili za kitanzania… utajiri ambao Watanzania wawili tu wamefanikiwa kuufikia, ‘mtoto wa mjini’ Rostam Aziz na mhafidhina wa kibiashara Mo Dewji. Ukwasi wa ngazi hiyo unahitaji zaidi ya talanta ya ujasiriamali na biashara na zaidi ya upekee wa gunduzi na bunifu.

Niliwahi kuandika kwenye mada moja, “katika kila kila utajiri kuna ukafiri nyuma yake.!” Kuna ngazi ya utajiri ili kuifikia inahitaji purukushani, ‘kash kash’ na kufanya mambo ambayo yawezekana wengine hatuna kifua kuyafanya.

Nitatoa mfano… mfano wa moja wa billionare ambaye anahusudiwa sana ulimwnguni na moja ya mabilionea wa kupigiwa mfano sana ni Billionare Roman Arkadyevich Abramovich au kama ambavyo anajulikana kwenye inner circle pale Kremlin, ‘Oligarch Abramivich’ au ‘Mr A’.

Huyu muheshimiwa akiwa na umri wa miaka 34 tu Roman tayari alikuwa na tittle ya ‘Oligarch’, title ambayo jamii ya Urusi imewapachika watu wenye ushawishi mkubwa nchini humo na ambao wako kwenye ‘inner circle’ ya utawala wa nchi ya Russia. Katika miaka hiyo 34 tayari alikuwa anamiliki kampuni kubwa ya uzalishaji mafuta ya Sibneft na pia alikuwa moja ya wanahisa wakuu wa kampuni ya RUSAL (Russia Aluminum) ambayo kwa kipindi kile ndio ilikuwa kampuni inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa zaidi wa Aluminum wakichangia zaidi ya 9% ya Aluminium inayotumika duniani kote. Katika umri huu wa miaka 34 ni ngumu kusema kwa hakika hasa utajiri wa Oligarch Abramovich ulikuwa unafikia kiasi gani kutokana na usiri kuhusu mapato yake, lakini hakuna shaka kabisa kwamba utajiri wake ulikuwa unazidi dola bilioni 6 za kimarekani.

Unaweza kujiuliza ni kwa namna gani katika umri mdogo kiasi hicho mtu anaweza kuwa na utajiri wa kupindukia kiasi hicho na hata kuwa moja ya wamiliki wakuu wa kampuni ya kuzalisha zaidi ya 9% ya aluminium inayotumika duniani.
Nataka tutazame mfano wa Abramovich kupata picha ni kwa namna gani unapaswa kuwa na ‘ngozi ngumu’ kupitiliza ili kuukwaa ubilionea.



Tuanze mwanzo kabisa….

Roman Arkadyevich Abramovich ni yatima aliyelelewa katikika umasikini wa kupitiliza na baadae kufanikiwa kuwa moja ya matajiri wakubwa zaidi kuwahi kutokea duniani. Historia yake ni mwanana kabisa kumtia mtu moyo namna ambavyo unaweza ‘kuinuka kutoka mavumbini na siku moja kuketi na wafalme.’ Wazazi wake walifariki angali bado akiwa mdogo kabisa kabisa na hivyo kupelekea yeye kulelewa na nduguze waliokuwa wanaishi kaskazini mwa Urusi kwenye eneo la Komi.

Japokuwa wazazi wake na yeye mwenyewe wameishi maisha yao karibia yote nchini Russia lakini asili yao hasa ni Israel. Babu yake mzaa baba, mzee Nahim Abramovich alikuwa ni mfanyabiashara ambaye aliishi pamoja na mkewe (bibi mzaa baba) Tauba Berkover waliishi wote huko jamuhuri ya Lithuania kwenye jimbo la Taurage. Baba yake Abramovich, Arkady Abramovich alikuwa ni afisa wa serikali katika jamuhuri ya Lithuania. Mama yake Abramovich aliyeitwa Irina Michaleno wazazi wake (babu mzaa mama) Vassili Michalenko na mama yake (bibi mzaa mama) Faina Grutman nao wote waliishi jamuhuri ya Lithuania. Wazazi wake (Arkady na Irina) walifariki akiwa mdogo kabisa… mama yake Abramovich, Irina alifariki Roman akiwa bado mchanga kabisa na baba yake Arkady alifariki kwa ajali ya gari miaka michache baadae. Na ndio hii ilisababisha Abramovich kwa mara ya kwanza kabisa kwenda kuishi Komi kwa nduguze, kaskazini mwa Urusi na baadae Uktah eneo lenye baridi kweli kweli na umasikini uliokithiri.

Katika ujana wake Abramovich aliwahi kujiunga na jeshi kwa muda mfupi sana kabla ya kuacha na kuanza kufukuzia ndoto zake. Kama ilivyo ndoto ya vijana wengi Tanzania miaka ya nyuma “kwenda Dar es salaam kutafuta maisha” ndicho hicho pia kinawakumba vijana wengi duniani kote kutaka kwenda kwenye miji mikubwa ya nchi zao husika, ndicho hiki pia alikifanya Roman… aliondoka Uktah na kwenda Moscow ‘kutafuta maisha’. Akiwa Moscow alifanya akili ya kujiunga na kozi ya masuala ya mafuta na gesi katika taasisi ya Gubkin Institute of Oil and Gas ambako alikuwa anasoma huku akiuza matairi chakavu ya gari ili kuweza kujikimu kimaisha. Akiwa bado anapambana kutafuta nafuu ya maisha hapa Moscow ndipo pia alikutana na mkewe wa kwanza, Olga na kumuoa.
Maisha hayakuwa mepesi sana kwa Abramovich… kipindi hiki ni kipindi ambacho Urusi ilikuwa inapitia kipindi cha mpito mgumu sana wa kiuchumi na kifalsafa. Ni kipindi ambacho ujamaa ulikuwa unadondoka na ubepari kushamiri nchini Urusi. Ni kipindi ambacho Urusi ilikuwa moja ya sehemu hatari zaidi kuishi kutokana na uhuni na ubabe ambao ulikuwa unatokea Urusi na nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki. Ni kipindi hiki ambacho nchi za ulaya mashariki zilibatizwa jina la “Wild East”. Abramovich alifanya kila aina ya kazi ya hali ya chini, kuanzia kuuza bidhaa ndogo ndogo mitaani mpaka kuwa makenika kwenye viwanda na hata kuwa ‘bodyguard’.

Waswahili tunasema kwamba “anayejua, anajua tu”, kwamba kuna watu unaweza kuwapa ndimu ukidhani unawakomoa lakini atakushangaza kwa kuikamua na kutengeneza ‘juisi ya lemonade’ na kuinywa kwa raha mustarehe. Ndicho ambacho Roman alikifanya, kuanguka kwa ujamaa na kuibuka kwa ubepari, tena ubepari wa kihuni na ubabe aliona yaweza kuwa fursa adhimu kabisa kwake… akaanza kufanya biashara ya kila namna. Roman akaanzisha biashara ya kuuza midoli… ile biashara ya kuuza tairi chakavu akaikuza zaidi na kuifanya kwa upana na mpaka kuwa wakala rasmi wa tairi mpya kutoka viwandani.
Lakini moja ya biashara ambayo ilimsaidia kumpa ‘connections’ ilikuwa ni pale alipofungua biashara ya kutoa ulinzi binafsi (bodyguards). Pale juu nilieleza kwamba kipindi anaanza maisha Moscow Roman aliwahi kufanya kazi ya u-bodyguard, lakini safari hii sio yeye alikuwa bodyguard bali alikusanya vijana wake kadhaa na kufungua kama kampuni ya kutoa ulinzi kwa wadosi.

Nimesema kwamba hiki ni kipindi ambahi Urusi ilikuwa ni ‘Wild West’, kipindi ambacho uhuni na ubabe ulikuwa ndio namna ya maisha. Kipindi ambacho ujamaa unandoka, serikali ikibinafsisha nyenzo zake za kiuchumi kwa watu wachache. Hapa kwetu Tanzania tumepita pia kwenye kipindi kama hiki hiki na wazee wetu wanajua shurba waliyopitia… anguko la ujamaa na kuibuka kwa ubepari. Kipindi ambacho tulibinafsisha kila kitu na kuacha wake zetu tu. Tofauti ni kwamba hapa kwetu wajanja ambao walibinafsishiwa mali za nchi walikuwa wanashindana ni yupi ambaye atatoa rushwa kubwa zaidi… lakini kule ‘Wild East’ haikuwa rushwa tu pekee… naam, ilikuwa lazima utoe rushwa kubwa kumzidi mwenzako lakini aliyekuwa mtemi na muhuni zaidi ndiye ambaye angeweza kujihakikishia umiliki wa kiwanda au rasilimali husika. ilikuwa ni kula au uliwe. Jifunze kula ‘nyma ya mtu’ au subiri ufanywe kitoweo.

Katika biashara za makampuni makubwa kuna kitu kinaitwa ‘hostile take-over’. Yaani kwa mfano bwana Mo Dewji na kampuni zake za MeTL waanze kuuza hisa za kampuni zake za MeTL Group kwa umma… anakuja mtu ambaye kwa muda mrefu alikuwa anatamani aiweke MeTL mikononi mwake… tumuite mtu huyu Paul (mfano tu). Ananunua hisa nyingi zaidi kumuwezesha kupata ujumbe wa bodi ya wakurugenzi wa MeTL. Kisha anaanza kukaa kwa siri na wanabodi mmoja mmoja na kuwashawishi kumuondoa Dewji kama MD na Mwenyekiti wa bodi … kikao kinaitwa, kura zinapigwa… bodi inamuondoa Dewji kuwa MD na mwenyekiti wa bodi na kumfanya Paul kuwa MD na mwenyekiti mpya wa bodi. Dewji anabakia kuwa mwanahisa tu wa kawaida kama wengine bila uwezo wowote wa kimaamuzi juu ya kampuni yake ambayo aliinzisha. Hii inaitwa ‘hostile take-over’. Lakini kipindi hicho huko ‘Wild East’, Urusi ya miaka hiyo walikuwa na namna ya tofauti ya ‘Hostile Take-over’. Tajiri mwenzako anakuvizia, anakuteka… anakutesa mpaka unasaini makaratasi. Kisha anakutandika risasi na kesho yake inatangzwa kuwa kampuni/kiwanda chako ni chake na mliuziana kwa maandishi na nyaraka anazo. Wiki moja baadae mwili wako unaokotwa jalalani and nobody cares, maisha yanaendelea… Wild wild East.!!

Katika mazingira kama haya ambapo miili ya matajiri, waandishi wa habari na hata viongozi wa kisiasa ilikuwa inaokotwa kila siku imetupwa mitaani unaweza kupata picha ni kwa namna gani ambavyo biashara ya u-bodyguard iliweza kushamiri. Matajiri walikuwa na hofa na maisha yao muda wote, kwa hiyo walihitaji ulinzi muda wote. Biashara ya Roman ikashamiri.
‘Dili’ hizi za kulinda matajiri na bishara zake za hapa na pale zilimpa ‘connection’ na kusaidia kujuana na watu muhimu ndani ya Moscow. Moja ya watu hawa muhimu ambaye baadae alikuja kuwa kama ‘mentor’ wake alikuwa ni Boris Berezovsky Mwanamahesabu nguli na mhadhiri wa chuo kikuu ambaye alikacha kufundisha chuo na kugeukia biashara ili asipitwe na upepo wa utajiri uliokuwa unavuma Urusi kipindi hicho.

Berezovsky alikuwa ni moja ya ma-Olygarch wa kwanza kabisa ndani ya Urusi. Nimeeleza pale mwanzoni Oligarchy ni watu wa namna gani. Borozevsky alikuwa ni moja ya matajiri wakubwa zaidi Urusi kipindi hicho ambaye alinufaika sana na ubinafsishaji wa mali za umma. Oligarch Boris Berezovsky hakuwa tu Oligarch bali alikuwa ni sehemu ya ma-Oligarch wachache ndani ya Urusi ambao waliojulikana kama ‘The Family’.
The Family ilikuwa ni ‘inner circle’ ya watu wachache sana ambao walikuwa karibu na Rais wa Urusi kipindi hicho Boris Yeltsin. Watu hawa walikuwa ni wanafamilia wa Yeltsin pamoja na matajiri wachache sana akiwemo Berezovsky. Kikundi hiki cha matajiri wachache pamoja na familia ya Rais ndio kiuhalisia ndio walikuwa wanaendesha nchi.

Kwa hiyo kitendo cha Abramovich kujiweka karibu na Berezovsky ilimaanisha kwamba alikuwa amefanikiwa kujenga urafiki na moja ya watu muhimu zaidi ndani ya Urusi na mwenye ushawishi ndani ya inner cirle ya Rais.

Watu wenye asili ya uyahudi twaweza kuwachukia na kuwasema tutakavyo kwa uonevu ambao labda wanaufanya… lakini jambo moja ambalo hatuwezi kubisha ni uwezo wao wa asili kiakili na kimkakati. Japokuwa Abramovich kwa kipindi hicho alikuwa ni mrusi tu lakini kuna damu ya kiyahudi ilikuwa ndani yake na ni wakati huu ambao alidhihirisha umahiri wake kimkakati.

Baada ya urafiki wao Abramovich na Berezovsky kukomaa na kushibana, Abaramovich alimuomba Berezovsky amsaidie kumtambulisha kwa watu muhimu Kremlin. Moja kwa moja Berezovsky akahisi labda Abramovich anataka kutambulishwa kwa Rais au mawaziri na akamjibu bado hajafikia ngazi ya kutambulishwa kwa watu hao… lakini Abramovich akamwambia hapana haitaji kutambulishwa kwa Rais au mawaziri… anahitaji kutambulishwa kwa mtu anaitwa Valetin Yumachev ambaye kipindi hicho alikuwa ni afisa wa kawaida tu wa Ikulu kitengo cha habari na maelezo na hukuwa na ushawishi kwa Rais Yeltsin. Berezovsky alishangaa maana Yumachev hakuwa na ushawishi wowote ule pale Kremlin.

Ndio hapa ambapo nasema kuna watu ni ‘born tacticians’… akili yao inawaza kimkakati kwa kila hatua na moja wapo ni huyu Abramovich. Abramovich alielewa wazi kabisa hawezi kutambulishwa kwa Rais na japo alikuwa na tuhela tudogo twa kubadili gari na nyumba lakini ukilinganisha na ma-Oligarch kipindi hicho yeye alikuwa ni kidagaa tu, ‘hohe hahe’ ambaye hawezi hata kukaa meza moja na rais. Lakini anaitaka hiyo connecvtion kuliko kitu chochote kile ili afike pale anapopataka kimafanikio. Ndipo hapa ambako aliona kitu ambacho wengine hawakukiona… Valentin Yumachev, afisa habari mdogo wa Ikulu. Abramovich aligundua kwamba Yumachev alikuwa na mahusiano ya siri ya kimapenzi na binti wa Yeltsin aliyeitwa Tatyana. Binti huyu wa Rais pia alikuwa anapendwa mno na baba yake na alikuwa moja ya watu anaowasikiliza sana na kuwaamini.
Abaramovich akapiga hesabu zake… kama akiweza kujenga urafiki wa kushibana na Yumachev, na kisha kufanya uhusisano wa Yumachev na Tatyana ukue na hatimaye labda kuoana. Maana yake ni kwamba atakuwa ni rafiki wa mkwe wa Rais wa Urusi. Na kutokea hapo kujiweka karibu na Rais kupitia mgongo wa ‘best friend’ wake itakuwa ni rahisi kama kusaga maini.

Berezovsky akamtambulisha Abramovich kwa Yumachev. Hata Yumachev mwenyewe akashangaa… ‘mtoto wa mjini’ Abramovich ambaye ni rafiki wa ma-Oligarch kutambulishwa kwake. Kwa hiyo hata urafiki ukakua kwa haraka sana Yumachev kuona ni heshima kubwa kwake kwa mtoto wa mjini kama Abramovich kumthamini na kumuona ana umuhimu.
Lakini Abramovich alikuwa anaiona ‘potential’ ndani ya Yumachev ambayo hata mwenyewe alikuwa haioni… Abramovich alikuwa anaona miaka mitano mbele ambayo wengine walikuwa hawaioni…



SEHEMU YA PILI IKO POST #58


SEHEMU YA TATU IKO POST #151


SEHEMU YA NNE IKO POST #298


The Bold
To Infinity and Beyond
Nitag mkuu
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij addenbwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush mossad 03 white wizard xtaper Mzigua90 Ollachuga Oc Gidbang Mateja M.G Yango jipu abaa4all DIBAJI Agenda1 Grahnman The MaskmaN Slim5 Xubzero agprogrammer JoJiPoJi Architectus blance86 Mamtolo monde arabe Ngao Ya Imani stardust JK naiman64 Dharra seledunga ABB SHAMMA Richard Waziri wa Kaskazini Mwinjuma1 Kanungila Karim baracuda Mwamba028 besaro Pyepyepye Bilionea Asigwa ibn Kiti Chema Tugas Royal Warrior mederii mmangO manzi james LIKUD adrenaline Royal Son Mhadzabe salaniatz Natasha Ismail jiwe jeusi chibalangunamchezo
John Mloy conjuget Van Pauser great G Mtoto wa nzi Zeus1 hindustan Sci-Fi MAN OF PEACE kashata emnly danny baraka bb MTOTELA kbosho TEMLO DA VINCA
Uwe unanitag mkuu tafadali
 
79 Reactions
Reply
Back
Top Bottom