Roma na wenzake wapatikana, wapelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay kisha Mwananyamala Hosp na kuachiwa

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,067
Msanii Roma Mkatoliki anadaiwa kupatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar.

Habari ya akina Roma kupatikana imethibitishwa na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na nani waliokuwa wamewashikilia. Kwa sasa wanadaiwa kuwepo kituoni hapo kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.

Taarifa zaidi zinafuata..

Hadi sasa bado polisi wanamhoji kituoni na kuna waandishi wa habari wapo wanamsubiria pamoja na wadau wengine wa muziki. Waliohojiwa na waandishi ni pamoja na msanii Ney wa Mitego na Rais wa shirikisho la wasanii nchini Simon Mwakifamba.

Mwakifamba kasema hivi sasa wamepata nafuu maana hata yeye alikuwa anaogopa

Ney wa Mitego amehojiwa na kusema hii inathibitisha Muziki wa Hip Hop unasikilizwa na watu wengi na una mchango kwenye jamii na wataendelea kuimba.

Roma na wenzake wamepelekwa Hospitali ya Mwananyamala

Roma ameachiliwa anaongea na waandishi wa habari anasema ni mzima wa Afya, pia anashukuru watanzania wote kwa kupaza sauti zao.





ROMAA.png

roma.jpg

Pia soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Back
Top Bottom