ROMA Mkatoliki unaogopa? Mbona hutoi wimbo kuhusu hali ya sasa?

KING DUBU

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
919
1,239
Sisi wadau wa ROMA mkatoliki msanii wa Hip Hop tunatamani sana kusikia na kuona Ngoma mpya kutoka kwako.

Kwa matukio yalivyo sasa naamini una mengi ya kuyazungumzia kwa Kuangalia uongozi wetu wa awamu ya 5. matukio ya Mwafwaaa, Bashite, Kuliwa kwa fedha Za wahanga wa tetemeko, fukuzana ya CCM, hofu ya Chadema(Ukuta), kuongezeka kwa ugumu wa maisha, Tatizo la mikopo, Milioni 50 kila kijiji, Hongera ya kununua Bombardier. Na mengine mengi.

Usiogope Si kawaida yako. Tunakumbuka vibao kama Viva ROMA Viva, Mr. President, Mathematics, 2030, Tanzania, hivi japo havipigwi redioni vinabaki kuwa conscious Music vinaeleza ukweli come on ROMA.

Tunasubiri kibao matata.
========

Msanii ROMA aliwahi kujibu swali hili kwenye interview hii;

 
Teh teh.....ana ndugu wanamtegemea.....wasije wakamuweka mahali salama.
 
'' Walioacha tiz wakawa kama mrisho ngasa, mi nakomba pesa zote nasepa kama LOWASA ''
 
Roma ulikua mbele sana kukosoa issues za serikali zinapoenda komba

Saizi umesizi kimyaaaaa like sio political rapper saizi umesha pata issue kibao fanya udondoshe ngoma moja juu ya hali ya nchi mukulu Bashite nk

Kitaaa tutakusupport hata song ikifungiwa sisi tutakua nazo kama albam za vinega

Usiogope
 
Aiseeee!!! Mahali nchi imefka kwa hili linaloendelea

Nataman tu ney wa mitego na roma watoke na ngoma moja
Maana hayo madongo yatakua co ya nchi hii
 
Back
Top Bottom