Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,665
- 239,156
Hili la Roma kushirikiana na baadhi ya wasanii kutumbuiza Ikulu , kwenye ile ripoti ya Mchanga ni lazima lijadiliwe.
Ikumbukwe kwamba ni majuzi tu huyu jamaa alitekwa na wanaosemekana ni watu wasiojulikana , ambao baadhi ya wadau wamewaita " watu wa serikali " rejea bastola alioonyeshwa Mh Nape Nnauye.
JF ikishirikiana na Dunia nzima ikapiga kelele hadi Roma akapatikana , labda kwa ufupi niseme kwamba bila kelele za dunia nzima , huyu jamaa angepotea moja kwa moja , Shukrani kwa wote waliopaza sauti kuhakikisha usalama wake , Mungu atawalipa.
Sasa cha kushangaza ni kwamba ameonekana kushirikiana na waliotuhumiwa kumteka !
Swali ni je Roma bado yuko chini ya ulinzi , waliomteka ndio wamuongoza au ni uzalendo wake mpya kwa Nchi yake ?