Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,492
2,000
"Kama msanii unang'ang'ana kuimba siasa na kukosoa serikali basi amua kuachana na muziki uanzishe chama cha siasa. Lakini kama unataka kupata maslahi kwenye muziki, basi nyimbo hizo hazilipi. Haiingii akilini nina shahada nne halafu msanii ambaye hajaenda hata shule anatunga nyimbo za kunikosoa. Wewe na darasa la nne lako sijui la 7 utanionya mimi mwenye degree nne na nimefundisha vyuo vikuu mbalimbali?"

Dr.Harisson Mwakyembe (PhD), Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo.!
 

Fiati

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
1,249
2,000
Mwanamuziki ni mwanafasihi ni Kama mwandishi wa kazi za kifasihi anaweza kuandika au kuimba matatizo yanayoikumba hadhira yake na kujaribu kutoa suluhisho kupitia kazi yake ya kifasihi. Mwambie huyo Dr ampe hai Farouk topan na Tamthiliya zake Aliyeonja Pepo na Mfalme Juha.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,670
2,000
Eti kuwa na degree 4 ndio utakiwi kushauriwa?

Roma degree 1 tu lakini anawahenyesha Phd holders za majalala ajibu hoja zake sio kuongelea mambo binafsi hata wakina Makonda ni zero lakini kila siku anawaelekeza cha kufanya mawaziri mbona ujamjibu wewe Mwakyembe?.

Kumbe ndio maana nchi kaachiwa Magufuli aiendeshe anavyotaka Katiba na sheria kaweka pembeni kisa PhD holder
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom