Roma Mkatoliki amesema amechoka na salamu za pole huku akiwataka Watanzania wafunge file

UCD

JF-Expert Member
Aug 17, 2012
7,667
2,000
Akizungumza hivi punde tu na Kituo cha Redio ambacho kinakuja na Kasi ya Kimbunga cha Efm katika Kipindi maarufu cha ' Joto la Asubuhi ' Msanii Ibrahim Musa ( Roma Mkatoliki ) amewataka Watanzania waache sasa kumpa pole kila mara na kila wamuonapo na badala yake amewataka sasa ' wafunge file ' juu ya lililomtokea ( sakata la Kutekwa )

" Unakuta Mtu uko zako barabarani au Kituo cha Mafuta unajaza Mafuta halafu anakuja tu Mtu anakusalimia haraka kisha maongezi yake mengi ni ya kuuliza tu nini kimenitokea hali ambayo huwa inanikera sana na ndiyo maana leo kupitia Redio yenu nasema kuwa naomba tufunge file juu ya kilichonitokea na badala yake sasa tujikite katika maendeleo, harakati na tugange yajayo " alisema Roma Mkatoliki.

Najua hata humu Jamvini JF wapo wale Watu ambao kila kukicha wamekuwa wakijifanya kumpa pole ambazo haziishi na amezichoka mno sasa hivyo Roma Mkatoliki amesema kuwa sasa anataka ' file lifungwe ' rasmi na mgange yajayo.

Kwa tafsiri iliyo fupi sana ambayo inaweza isieleweke vyema kwa wengi ni kwamba hapa Roma Mkatoliki anasema kwamba wengi wa wale wanaojifanya kumpa salamu za pole na kumtia moyo ni ' Wanafiki ' watupu ( ukimuondoa tu GENTAMYCINE pekee ) hivyo amewachoka na mkome!

Kila siku mnajifanya kumpa pole wakati hata Nyumbani Kwake kwenda tu kumtembelea mlishindwa au basi hata tu kumtumia Pesa katika Simu ili angalau zimfute machozi mmeshindwa lakini humu Mitandaoni mnajishebedua na kujitutumua kujifanya mmeumia na kilichomtokea.

Roma Mkatoliki nikupongeze sana na nimefurahi mno leo ulivyowapa ' makavu ' Watanzania wanafiki wanafiki na naungana nawe kwa 100% hasa ulipowaambia kuwa sasa unawataka ' wafunge file ' na wagange yajayo. Na labda nikuibie tu siri Roma Mkatoliki unaweza kukuta katika hao hao wanaojifanya kukupa pole na kukutia moyo wamo wale Watekaji wako au Ndugu zao au hata Wanafamilia wao.

Safi sana Roma Mkatoliki sasa ' wafunge file '.

Nawasilisha.
Sasa wewe una matatizo gani mkuu!!? Roma amesema ufunge file lakini wewe umefungua thread humu JF!!! Naona una akili za kuvukia barabara tu!!
 

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,452
2,000
Wasanii wa Tanzania bwana.
"eti akiwa Petrol Station kuweka mafuta "..

Anawajulisha wananchi kuwa na yeye ana OPA sio!?

So poor upstairs..!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom