Elections 2010 Roma kawafanyia nini wakazi wa Iringa?

Meale

Member
Nov 24, 2009
91
0
Nilikuwa kwenye show inaitwa 'mtikisiko' uwanja wa Samora Iringa.

Kulikuwa na wasanii wengi maarufu wa ndani na nje ya nchi wakitumbiza kama Radio na mwenzake, Chege, Juma Nature, Barnabas, Temba, Lina, Mr. T na wengine kibao. Lakini kilichonishangaza mtangazaji mara kwa mara alikuwa akiuliza bado nani? Watu wengi walipiga kelele 'Romaaa' hivyo basi nami nikapata shauku ya kutaka kumfahamu huyo ni nani kwani sijawahi kusikia nyimbo zake redioni hivyo nilihisi hakuwa maarufu.

Kila baada ya msanii mmoja kutumbuiza watangazaji waliuliza tena 'bado nani? Na jibu la watu lilibaki lile lile. Mara kadhaa MC alikuwa anatania huyo msanii ameshindwa kufika, basi watu wengi walipiga kelele warudishiwe pesa zao. Ilipofika zamu yake kutumbuiza watu walimshangilia kwa nguvu sana kuliko wasanii wote maarufu waliotangulia. Hapo ndipo nilipogundua kumbe watu walikuwa wanataka kusikia mashairi kuhusu siasa, hasa masuala ya ufisadi na utendaji mbovu wa serikali. Kila alipotaka kushuka jukwaani watu walimsihi apande tena kwa kisingizio hawasikia wimbo fulani na fulani.

Nimebaki najiuliza huyu mwamuziki amewapa nini wakazi wa Iringa hadi wakaamua kuwapuuzia wasanii wetu wote maarufu? Je ni kweli hata kwenye burudani watu wanataka kusikia siasa tu?

Mwenye mashairi ya nyimbo zake ayaweke hapa (kama hayavunji sheria za JF) ili tuyachambue.
 
Asante mkuu kwa link. Nasikia kuna wimbo wake unaitwa Mr. President, kama unao naomba tuwekee pia.
 
Jamaa ni mkali.. Eeehhh!!!

Mr. President..., Tanzania! Ha ha ha

Nitafurah sana miaka michache akiingia BUNGENI.....

SPATI PICHA, MC ROMA anatoa hoja, MJOMBA anachangia na PROFSA JAY anapga makofi 2015
 
Jamaa ni mkali.. Eeehhh!!!

Mr. President..., Tanzania! Ha ha ha

Nitafurah sana miaka michache akiingia BUNGENI.....

SPATI PICHA, MC ROMA anatoa hoja, MJOMBA anachangia na PROFSA JAY anapga makofi 2015

sasa kama jamaa ni mkali mbona hasikiki kwenye radio zetu? Au mashairi yake hayawapendezi wamiliki wa radio?
 
Du! nimeangalia huu wimbo wake Mr President! aaah! anachana waziwazi! sijui kwa nini Chadema hawakumchukua ktk kampeni wakati wa uchaguzi!heheheh! afaa angezunguka na Dr Slaa kila mkoa huyu dogo!
 
Du! nimeangalia huu wimbo wake Mr President! aaah! anachana waziwazi! sijui kwa nini Chadema hawakumchukua ktk kampeni wakati wa uchaguzi!heheheh! afaa angezunguka na Dr Slaa kila mkoa huyu dogo!

Ni kweli kabisa, yaani huyu bwana ingependeza kama angekuwa kwenye kampeni za Dr. slaa ili kusaidia kufikisha ujumbe.
 
Back
Top Bottom