“Roma haikujengwa kwa siku moja”

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,316
10,782
u! Aidha kumbuka Roma haikujengwa kwa siku moja, ujenzi wa miundombinu ndiyo mwanzo wa maendeleo ya wananchi.

Mara kadhaa huu usemi, “Roma haikujengwa kwa siku moja” umesikika kutoka kwenye vinywa vya wanasiasa na hata wananchi. Leo katika uzi mmoja ambao naona umeshafutwa, nimekutana tena na usemi huo kama inavyoonyesha hapo juu.

Hapa naweka tafakuri yangu juu ya usemi huu.

Huu usemi wa “Roma haikujengwa kwa siku moja” ni excuse kubwa ya CCM. Kwanza huu usemi ulianza kutumiwa na Wafaransa kwenye miaka ya 1100, na kuingia kwenye semi za Waingereza kwenye miaka ya 1500. Hii inaonyesha ni kiasi gani ‘context’ ya namna usemi ulivyoanza. Wafaransa walitumia usemi kama kisingizio cha umasikini wao.

Pili, wanaoendelea kutumia usemi huu, wanasahau mazingira ambayo ‘Roma’ ilikuwa nayo wakati inajengwa na mazingira yaliyopo sasa hivi. Roma ilijengwa kwenye mazingira magumu sana: watu walikufa kwa mafua tu, kiwango cha uelewa, elimu na utaalamu kidogo, teknolojia duni sana n.k.

Ona hapa jinsi mafua yalivyosumbua ‘Waroma’Reviewing the History of Pandemic Influenza: Understanding Patterns of Emergence and Transmission

Ebu angalia hapa magonjwa yaliyowaua ‘Waroma’ wakati wanaanza kuendeleahttps://www.historylearningsite.co.uk/britain-1700-to-1900/industrial-revolution/diseases-in-industrial-cities-in-the-industrial-revolution/

Leo hii kuna maendeleo makubwa sana kwenye nyanja za afya, elimu na teknolojia duniani. Hivyo haiwezekani ati taifa liendelee kwa spidi ambayo ‘Roma’ ilitumia.

Angalia hapa baadhi ya maendeleo kwenye sekta ya afya:



Maendeleo kwenye elimu:5 Emerging Trends in 21st-Century Education | Getting Smart

Maendeleo kwenye teknolojia:StackPath

Kama ingekuwa kwamba “Roma haikujengwa kwa siku moja” kwa mazingira ya maendeleo hayo, Taiwan, Hong Kong, Korea ya Kusini na Singapore zilizokuwa masikini kama Tanzania nazo hadi sasa zingekuwa masikini. Hizi zinajulikana kama the “Asian tigers”. Zimekuwa kwa kasi kwa ndani ya miaka 30 tu (1960s - 1990s).

Jifunze kidogo kuhusu ‘the Asian miracle’ hapa:Tiger Economy.
Na hapa:


Hizi ziliwekeza haswa kwenye elimu ambayo ikafanya uwekezaji wa viwanda kuwa na maendeleo makubwa na athari chanya kwenye chumi zao. Soma hapa: https://content.taylorfrancis.com/b...-X&isbn=9781134677153&format=googlePreviewPdf


Hizi nchi hazikukubali kuingizwa mkenge na Benki ya Dunia na sera zake za uliberali mamboleo. Hazikukubali kuendeshwa kutokea Washington - kwa the


Soma hapa kuhusu sera ya viwanda ambayo hizi nchi zilienda nayo:https://ora.ox.ac.uk/objects/uuid:3...at=application/pdf&type_of_work=Working+paper

Malizia na hii kuelewa namna ambavyo the Asian tigers walijiweka mbali na sera za Benki ya Dunia: https://www.researchgate.net/profil.../Graduated-Sovereignty-in-South-East-Asia.pdf

Sasa ndugu zangu wa CCM, ebu niambieni hiyo ‘model’ anayoitumia Magufuli na serikali yake ni ya wapi? Ya kuwekeza kwenye miundombinu kwa pesa nyingi hivyo, ili taifa kuendelea.

Hakuna haja ya ku “invent the wheel”, ilhali blueprints mbalimbali zipo. Ni kiasi cha kuiga tu na kuzirekebisha ili ziendane na mazingira yetu. Maendeleo makubwa kabisa katika nyanja nilizozitaja hapo juu yanatuwezesha tuweze kuendelea kwa kasi zaidi ya the Asian tigers. Reinventing the wheel, matokeo yake ni kupiga mark-time tu: kila anayekuja anaanza na vyake. Kwa staili hii hakika inakuwa sahihi kusema ‘Roma haikujengwa siku moja’.

Nawatakieni msimu mzuri wa sikukuu.
 
Kila kiongozi Africa hapa lazima awe na hii excuse , lakini wanasahau zipo nchi zinaendelea na zimeendelea kwakasi zama hizi kama Malysia, Singapore, SouthKorea, China, Indonesia, Brazil,Mexico Thailand nk
Hawajui kwamba Mchina anaendelea kwa kasi kwakutumia teknolojia ambayo Mzungu aliigundua miaka tele nyuma...
 
Back
Top Bottom