Rolnado watatu maarufu duniani ambao wameshachukua Ballon d'Or na mchezji bora wa Fifa

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,322
17,822
Kuna Ronaldo watatu maarufu sana ktk historia ya soka ambao wamesha wahi kushinda tuzo za Ballon d'Or .
Wawili wanafahamika zaidi kwa jina la Ronaldo mmoja akiitwa Ronaldo de lima na mwingine ni Cristiano Ronaldo.

Huyu wa tatu anafahamika zaidi kama Ronaldinho Gaucho. Ingawa wengi hawajui au wanajua ila hawaja zingatia ukweli kwamba huyu jamaa jina lake halisi ni Ronaldo de Assis Moreira, au maarufu kama Ronaldinho.

Tujiulize kwanini hakupenda kujitambulisha zaidi kama Ronaldo?
Je, alitaka kuweka utambulisho wake wa kipekee hakutaka kutembelea jina la Ronaldo ambae tayari alikuwa maarufu wakati huo?
Kama ni hivyo unahisi jamaa(Gaucho) anajiamini sana kipaji chake hakutaka kutembelea nyota ya mtu?
Mwisho tujiuize Cristian Ronaldo alipendelea kuitwa Ronaldo wakati yeye ni Cristiano kwa vile alitaka kutembelea jina la Ronaldo halisi?

Toa maoni yako mdau.
 
Back
Top Bottom