Roketi kuanza kusafirisha watu kati ya miji kwa dakika tu

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,323
6,848
Roketi kuanza kusafirisha watu kati ya miji kwa dakika tu

Source: Roketi kuanza kusafirisha watu kati ya miji kwa dakika tu

Hivi karibuni watu wataweza kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kutumia roketi, safari ambayo itachukua dakika chache tu, kulingana na mjasiriamali Elon Musk.

Musk aliahidi haya katika kongamano moja nchini Australia.

Inasemekana kuwa itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.

Musk amesema pia kuwa mwaka wa 2024, ataanza kuwasafirisha watu hadi Mars. Kampuni yake ya SpaceX itaanza kujenga meli za kipekee zitakazofanikisha haya, mwaka ujao.

Kwa sasa kampuni yake inatengeneza ain amoja tu ya roketi; aina ya BFR ambayo inaweza kufanya kazi tofauti tofauti ikiwemo kupeleka watu kwenye mwezi na Mars.

"Safari ambazo watu wengi wanaona kuwa ndefu zinaweza kukamilika kwa chini ya nusu-saa," aliambia umati wa watu mjini Adelaide.

"Baadhi ya wateja wetu wanataka kuona BFR ikiruka mara kadhaa kabla yaya kuwa na imani nayo," Musk alisema.

"Kwa hivyo tunachotaka kufanya ni kujenga roketi kadhaa aina ya Falcon 9 na Dragon, ili wateja wawe na urahisi, na ikiwa wanataka kutumia roketi za kale, bado tuna kadhaa."

Musk, alianza mipango ya kufanikisha safari za Mars mwaka wa 2016, na amerejea na habari zaidi.

Musk amevutia watu wengi sana ambao wamependezwa na miradi yake. Na ingawa ahadi zake mara nyingi zimechukua muda mrefu kutekeleza, baadhi imetimia.

Hii ni pamoja na kutuma na kurejesha roketi 16 duniani baada ya roketi hizo kumaliza misheni yao. Roketi mbili kati ya hizo 16 zimeweza kusafiri tena mara ya pili.

Anasema cha muhimu sana kwake ni kuunda rtoiketi ambazo zinawza kutumika tena na tena kama ndege, kwani ni inagharimu pesa nyingi sana kutengeneza roketi.
 
Sasa naweza kufika sehemu yoyote kwa mda mfupi, leta hiyo kitu tupaki Boieng na Bombardier zetu.
Ila Huyo jamaa hatatekeleza mpango huo, anaweza hujumiwa na makampuni yenye ushindani katika usafiri wa anga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paulo na timu yake walipoondoka Uyahudi kwenda kulihubiri neno kwa mataifa iliwachukua miaka kadhaa kufika Roma mahali ambapo leo ni mwendo wa masaa kama sio dakika chache tu. Au je, hakuwachukua wana Israel miaka 40 kuivuka Shamu na Sinai? Maarifa yameongezeka duniani distance is becoming insignificant.
 
Huyu jamaa ana akili sana na anakula mjani. ana ile nyingine ya hyperloop wakati wenzake wanaamini future transportation ni flying cars yeye anaamini solution iko underground ndo ana hyperloop
 
Huyo jamaa anaongea sana zaidi ya utendaji, hadi hisa za makampuni anayohusika nayo zimeshuka sana kwa sababu hazitimizi malengo.

Vitu vingi sana viko kwenye pipeline na vinamiss deadline.
 
Anayejua somo la Relativistic mechanics haiwezekani kutumia nusu saa kufika mwezini sembuse Mars unless otherwise chombo kiende kwa speed ya mwanga.
Chombo kikienda kwa speed ya light metabolic activities zote zinasimama kwa walio ndani ya chombo.Na chombo kitayeyuka kwa joto kali.
Sio kila habari inayoandikwa ni kweli zingine ni fix.
Wawadanganye wasiojua fizikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huyu mzee baba ni hatari,kwenye hyperloop tuone nani ataibuka kidedea kati yake na sir richard branson
pia kwenye neuralink akifanikiwa dah ubongo utakuwa sawa na pc i dunno
 
Anayejua somo la Relativistic mechanics haiwezekani kutumia nusu saa kufika mwezini sembuse Mars unless otherwise chombo kiende kwa speed ya mwanga.
Chombo kikienda kwa speed ya light metabolic activities zote zinasimama kwa walio ndani ya chombo.Na chombo kitayeyuka kwa joto kali.
Sio kila habari inayoandikwa ni kweli zingine ni fix.
Wawadanganye wasiojua fizikia

Sent using Jamii Forums mobile app
nusu saa ni kutoka London hadi New York mkuu.
 
Anayejua somo la Relativistic mechanics haiwezekani kutumia nusu saa kufika mwezini sembuse Mars unless otherwise chombo kiende kwa speed ya mwanga.
Chombo kikienda kwa speed ya light metabolic activities zote zinasimama kwa walio ndani ya chombo.Na chombo kitayeyuka kwa joto kali.
Sio kila habari inayoandikwa ni kweli zingine ni fix.
Wawadanganye wasiojua fizikia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umesoma kweli topic, Hakuna sehemu wanakosema anataka peleka watu mwezini wala mars kwa muda huo ila yeye anataka wasafirisha watu mji hadi mji mwingine hapa hapa dunianai kwa kutumia rocket.
Kuhusu kwenda Mars siyo kwamba anasema atatumia nusu saa.
 
Back
Top Bottom