Roho za aina tatu zenye thamani alizoziacha duniani profesa mkulima Yuan Longping

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG11458322209.JPG



2BD1AA9996E24D3EAA1688899094767F1059E847_w1000_h667.jpeg


"Mwanadamu ni kama mbegu, anatakiwa kuwa mbegu bora. "

Haya ni maneno ambayo mwanasayansi wa kilimo wa China anayejulikana kama "Baba wa mpunga chotara " Profesa Yuan Longping alikuwa akipenda kusema wakati alipokuwa hai.

Mei 22, 2021, Yuan aliaga dunia mjini Changsha, Hunan akiwa na umri wa miaka 91. Katika mwaka mmoja uliopita, watu wamekuwa wakiendelea kutoa heshima za aina mbalimbali kwa mwanasayansi huyo ambaye "alibadilisha ulimwengu kwa mbegu mmoja". Mei 22 mwaka huu ni kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Yuan Longping, na hisia za watu kwake zilifikia kilele. Basi je, kwa nini tunamuenzi sana Profesa Yuan? Kwa maoni yangu, tunachokumbuka ni roho za aina tatu zenye thamani alizoziacha duniani.

Kujitolea maisha yote kwa ardhi

Akijiita kama "msomi mkulima" , ingawa alizaliwa katika familia ya wasomi, Yuan Longping alijitolea maisha yake kwa ardhi, na hata kabla ya kufariki, bado alisema, "sijamaliza shughuli za mpunga chotara, lakini nitastaafu." Wakati wa uhai wake Yuan alikuwa na "ndoto ya kufurahia kivuli cha mpunga". Mnamo Septemba 2021, mpunga wenye urefu wa zaidi ya mita 1.8 hatimaye ulijaa shambani wakati wa mavuno. Ijapokuwa hakuuona kwa macho yake, lakini inaaminika kwamba pia aliweza kuona akiwa mbinguni. Baada ya Yuan kufariki, watu wengi walisema, "Yuan hatimaye amekumbatia na kulala vizuri katika ardhi aliyoipenda kwa moyo wote."

Kutatua shida ya kula kwa Wachina bilioni 1.4

China ina watu bilioni 1.4 , ambayo ni sawa na 20 % ya watu wote duniani, lakini ardhi yake ya kilimo inachukua chini ya 7% ya dunia nzima. Kama nchi kubwa inayogharimu mpunga, Yuan Longping alielewa kuwa lengo hili linaweza kufikiwa tu kwa kuongeza uzalishaji. Mapema miaka ya 1970, Yuan na timu yake walifanikiwa kulima mpunga chotara wa kwanza wenye nguvu, ambao ulitoa 20% zaidi ya mpunga wa kawaida. Kutokana na mafanikio ya mpunga chotara wa Yuan, watu bilioni 1.4 wa China wametatua kabisa tatizo la ulaji, na pindi tu matumbo yao yanaposhiba ndipo wanaweza kuwa na nguvu ya kutimiza uhuishaji wa taifa lao. Tunaweza kusema kuwa hii ni roho ya uzalendo aliyokuwa nayo Yuan Longping, ya kujitolea bila ubinafsi kwa nchi na wananchi wenzake.

"Ndoto ya kufunika dunia nzima”

Mbali na "ndoto ya kufurahia kivuli cha mpunga", ndoto nyingine kubwa ya Yuan Longping ilikuwa ni "ndoto ya kufunika dunia nzima". Yuan Longping alipenda teknolojia yake ya mpunga chotara na upandaji ifike nje ya China, na kwamba nchi za Afrika ni sehemu muhimu ya ndoto yake hiyo. Katika kongamano la kimataifa la tasnia ya mpunga lililofanyika mwishoni mwa Juni 2019, Yuan Longping aliwaambia wajumbe kutoka nchi 15 za Afrika walioshiriki katika kongamano hilo kuwa, "usalama wa chakula hauhitajika China pekee, bali pia nchi za Afrika. Ni muhimu kufanikisha teknolojia ya mpunga chotara kupatikana na kuota mizizi barani Afrika!"

Ingawa Yuan Longping ametangulia mbele ya haki, naamini kwamba iko siku ataona kwamba Waafrika wanamiliki bakuli la chakula kwenye mikono yao wenyewe. Kama balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki alivyosema katika salamu zake za rambirambi za kumkumbuka Yuan Longping, "Profesa Yuan Longping ni shujaa wa chakula, na amechangia sana juhudi za kuwasaidia watu wa nchi mbalimbali haswa za Afrika kuondokana na umaskini na kujenga jamii ya binadamu yenye hatma ya pamoja.”
 
Back
Top Bottom