Roho yangu inakuwa ngumu kuamini kuwa hii ni damu yangu

Wakuu

Huyu demu nilitemana nae baada ya kugundua kuwa anagongwa na jamaa mwingine ilikuwa mwezi mmoja kabla ya kugundua aliniambia kuwa anamimba, baada ya kugundua na kumtema nikamwbia tusubiri mtoto azaliwe tutajua cha kufanya, kweli mwaka Jana mwezi wa kumi nilipigiwa simu na dada mtu kuwa mdogo wako Yuko hosp amewapa namba wanipigie wanipe taarifa.

Pia, hawana pesa ya kufanya operasheni na kununua dawa, nikaingiwa na huruma kutokana na maelezo Yao nikawaza siyo vizur mtu afe sababu ya pesa nayoweza kuitoa nikawatumia kama 250k iwapush, alivyojifungua wakanipigia simu kutaka kujua nafanya utaratibu gani wa kwenda kujitambulisha na kuhusu huduma ya mtoto.

Nikawaambia sina hakika na huyo mtoto kama ni wa kwangu nitaendelea kusaidia vile navyoweza Ila kuhusu kuja kujitambulisha au kumchukua bint yenu kukaa nae hapana tusubiri mtoto akue, hawakunielewa ila Mimi niliendelea kushikilia msimamo wangu, nikawa natoa huduma miezi mitatu imepita bint nikimwambia nitumie pic ya mtoto anasema simu yake mbovu Ila kwenye social media anampost Jambo ambalo silipendi, dogo amefikisha miezi sita nikamwambia tena naomba unitie picha za dogo jibu lake ni lile lile. Baati nzur nikabahatika kukutana nae nilichoka kichwa mpaka vidole.

Mimi ni mweusi na mama ake ni mweusi huyo dogo Hana dalili zozote za kuwa mweusi Leo hata kesho, Hana dalili zozote za kutanana Kwa namna yoyote na mtu yeyote katika familia yetu, anasura ngeni kabisa machoni pangu,. Nikamuuliza huyu ndo mwanagu akaniambia isikuchanganye rangi huyu ni mwanao nafsi yangu na hisia bado zinakinzana na maamuzi yangu kuwa Ile ni damu yangu, na nikiwaza chanzo cha kutema nae alitoka Kwa jamaa siku hiyohiy. Akaja kwangu.

Mpaka sasa sijatoa taarifa kwa mtu yeyote upande wa kwetu nasubiri mtoto afikishe mwaka mmoja,

Mapenzi hasara

26yrs




Sent using Jamii Forums mobile app
Kama mimiii tu !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom