Roho mbaya!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,839
...Hivi,

...ni KWANINI baada ya kuachana na mtu "wengi" hutamani 'mtaliki wake' apate mkong'oto wa maisha ajute kwanini aliachana na yeye?
kuna raha gani aliyekuwa kipenzi chako akiliona joto la jiwe kwa msongo wa mawazo, mapenzi na 'kufulia' ki maisha?
 
Ukiona hivyo basi ujue huyo mwenye ki grudge bado hajamsahau (get over) huyo mwenzake....kwa sababu kama umeshasonga mbele na maisha yako hutakaa utamani jambo baya limtokee huyo aliyekuwa mwenzako. Kwanza hutamfikiria kabisa...
 
...aha ha....

halafu kuna wale ambao hufanya kila wawezalo kukupa message '(showing off)' eti wamekuwa wabora tangu waachane 'nawe!'
 
...aha ha....

halafu kuna wale ambao hufanya kila wawezalo kukupa message '(showing off)' eti wamekuwa wabora tangu waachane 'nawe!'

Oh yeah...hiyo ndio huniacha hoi kabisa. Wenyewe eti huiita "upgrading"....
 
Sio katika mahusiano tu...
Hata boss akimfukuza kazi mfanyakazi wake, hapendi kuona anafanikiwa.
Its a kind of 'i was the best you could get'!
 
...Hivi,

...ni KWANINI baada ya kuachana na mtu "wengi" hutamani 'mtaliki wake' apate mkong'oto wa maisha ajute kwanini aliachana na yeye?
kuna raha gani aliyekuwa kipenzi chako akiliona joto la jiwe kwa msongo wa mawazo, mapenzi na 'kufulia' ki maisha?

Wenye tabia kama hizi watakuwa ni wenye roho za kimaskini na roho mbaya pia. Kwanini umuombee mtu wako akutane na mabalaa ya maisha ili wewe ufurahike!? Huwezi kujua labda mambo yamkinyookea siku moja anaweza hata kukupa msaada mkubwa tu wa namna moja au nyingine.
 
Watu huwa wanaundergo healing processes in stages. Its not pure sour grapes. Its the same with losing a loved one through death. Haina maana we loved or cared for them less but we heal in different ways. Inaanza na denial, hate and contempt, self-blame na baadaye you reach level of indifference. Then you can even say that you wish them the best.

That is self-actualization...lkn it takes great character to reach that level. Haina maana ni roho mbaya, we are just not all the same to face breakups, loses, failures and even successes we react in different ways.
 
huo ni ushamba mtu mkiachana acha kila kitu mambo ya kupigana ni kizamani yamepitwa na wakati
 
inategemea kama alikutenda au ulikuwa unamweleza lkn hakuelewi mpaka mkaachana wakati mwingine unajisikia raha moyoni kwa yale aliyokutenda.Kiubinadamu inatia huruma
 
mie xbf wangu kwa kweli huwa nafurahi akiwa na mafanikio na akipata tatizo huwa roho inaumia sema tu nafurahia akilalamika kuwa girlfriend wake mpya hayuko kama mimi!!
 
mie xbf wangu kwa kweli huwa nafurahi akiwa na mafanikio na akipata tatizo huwa roho inaumia sema tu nafurahia akilalamika kuwa girlfriend wake mpya hayuko kama mimi!!

...haya sasa... :)
 
Inategemea mmeachanaje! Kama mmeachana kwa ugomvi basi yule ambaye amelazimika kumwacha mwenzie huwa na hiyo kitu but kama mmekubaliana kuwa maisha hayaendi so bora kuseparate huwa mnabakia marafiki sana tu!
 
mie xbf wangu kwa kweli huwa nafurahi akiwa na mafanikio na akipata tatizo huwa roho inaumia sema tu nafurahia akilalamika kuwa girlfriend wake mpya hayuko kama mimi!!

Mamii umesema ukweli kabisa hakuna mwanamke/ hata mwanaume nadhani ambaye angependa kusikia mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wake ni bora kuliko alivyokuwa yeye. Mimi huwaga analalamika kwa rafiki zake kuwa alifanya makosa sana kunipoteza na anatamani kunirudisha kwenye himaya yake!! Nikizipata salamu hizi huwa nasikia raha. Hahahahahaaaaaa
 
tena ukiangalia mwingine anafikiria mali ulizonunua anataka azichukuwe hivi kuna wanawake wanapenda kuwa na mali
 
...aha ha....

halafu kuna wale ambao hufanya kila wawezalo kukupa message '(showing off)' eti wamekuwa wabora tangu waachane 'nawe!'

Bado hawajakua kiakili hao ndo maana whats the point of showing off kwa mwingine????
 
Mnapoanza mapenzi mnakualiana, intokea mara chache sana wakati wa kuachana mkakubaliana kuachana. kwa ajili hiyo, alieachwa hakubali yanazuka yote hayo mabaya.Ukimwacha mwenzio mwache kiistarabu...hazusha ugomvi na usimwacheghafla.
 
Watu huwa wanaundergo healing processes in stages. Its not pure sour grapes. Its the same with losing a loved one through death. Haina maana we loved or cared for them less but we heal in different ways. Inaanza na denial, hate and contempt, self-blame na baadaye you reach level of indifference. Then you can even say that you wish them the best.

That is self-actualization...lkn it takes great character to reach that level. Haina maana ni roho mbaya, we are just not all the same to face breakups, loses, failures and even successes we react in different ways.

Once again I'm beaten by your wisdom!

Lakini tukubaliane its not healthy kubakia kwenye grudges mimi nachukulia hiyo ni sign ya immaturity na kwa kiasi kikubwa hii hutokea kwa aliyesababisha hiyo break up; ex gf wangu aliniletea ujumbe kuwa anajiandaa kunywa sumu; nikamjibu kuwa awapo tayari anitaarifu nimpeleke kabisa sumu yenyewe! Ilhali yeye ndiye alinidump !
 
Mimi huwaga analalamika kwa rafiki zake kuwa alifanya makosa sana kunipoteza na anatamani kunirudisha kwenye himaya yake!! Nikizipata salamu hizi huwa nasikia raha. Hahahahahaaaaaa

Nadhani chukua wasaa wa kumwombea ikiwezekana waombe hao watuma salamu wamshauri! Usikae kufurahia matatizo ya binadamu mwenzio!:(
 
Kuna watu wengine huwa wanaachana wakiwa bado wanapendana sana. Lakini Kwahiyo kiroho huwa kinauma wakikutana alafu kila mtu akawa mambo super wivu hapo ndio unapoanzia, yaani mtu anaanza kujiuliza, ... yaani huyu ndio kafikia hapa? N.k Na baada ya kuagana ndio dua mbaya ama kuombeana mabaya kunapoanza! Ni vijiroho vibaya na vya chuki tulivyonavyo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom