Roho inaniuma sana, mabati niliyoezekea nyumba yangu yamepauka sana

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Yaani nimefanikiwa kujenga nyumba tena kubwa ila sijahamia bado vitu vichache nihamie, lakini kinachoniuma kipindi napaua (kupiga bati)niliaminishwa kuwa bati za kampuni fulani (hapa siitaji jina) ni nzuri na nikaonyeshwa nyumba ya jirani yenye hizo bati kuwa hazipauki.

Nilikubali baada ya kukagua na nikajiridhisha kila kitu, nikaenda nunua hizo bati pale Tazara nikapaua nyumba vizuri tu, sasa ni miaka 4 tangu nipaue sijahamia lakini zile bati kwa kweli zinatia kinyaa zimepauka hadi sina hamu ya kuhamia tena huko.

Hapa kinachoniuma zaidi nyumba ya jirani zake rangi iko vile vile na ni yeye aliniagizia alikonunua hadi bei ni hiyo hiyo, na hata jirani na ofisini kuna bati kama hizo hizo zimezungushiwa kama fensi sehemu wanakojenga hazijapauka kila siku naona ni mpya na nashindwa elewa hapa kuna siri gani kwenye hiyo kampuni nyingine zipauke nyingine zisipauke!

Hapa nawaza je! Ninunue bati zingine au ninunue rangi ya bati nikapake upya kwa mkono?

Ushauri wenu naombeni.
 
Mkuu bati ambazo hazipauki hazijawahi kuwepo relax usiishii kwa mashindano na kujifananisha kila kitu, iliyopauka ni rangi siyo bati ..

Rangi za bati zako kupauka kusipoteze Furaha ya Nyumba yako. Tusiumie kwa tulivyopoteza na kusahau tulivyobaki navyoo.
 
Piga rangi maisha yaendelee.

Bidhaa huwa zinazalishwa kwa batch. So unaweza kukuta batch moja iko vizuri ila nyingine ikazingua.

So za jirani ni za kampuni Sawa na yako ila ni batch tofauti. Kwa hiyo inawezekana yake iko vizuri ila wewe ulibahatika kununua batch zisizo nzuri.

Hujawahi kuona nyumba moja na bati alinunua za kampuni moja lakini unakuta baadhi zimeshaanza kupauka na zingine bado rangi iko vizuri?

Au unakuta kofia bado zinang'aa lakini bati imepoteza mng'ao wake. Au bati iko poa ila kofia zimepauka!
 
Yaani nimefanikiwa kujenga nyumba tena kubwa ila sijahamia bado vitu vichache nihamie,l akini kinachoniuma kipindi napaua (kupiga bati)niliaminishwa kuwa bati za kampuni fulani (hapa siitaji jina) ni nzuri na nikaonyeshwa nyumba ya jirani yenye hizo bati kuwa hazipauki...
Kuna siku nilinunua Bati- baada yakufika site Fundi alipokuja alinipigia Simu kuwa zile bati sio za ALAF ni fake. Bahati nna Jamaa angu anafanya kazi ALAF nilipompigia akanielekeza namna ya kutambuwa ALAF original na Fake!

Niliporudi Dukani Mmoja ya alieniuzia (walikuwa wawili) akaanza maneno ya shombo. Mimi nikawaambia wanibadilishie zile Bati wanipe Original au wanipe pesa yangu! Vinginevyo Kesi nawausisha ALAF Ili wawasaidie kuwaonyesha Walipozipata hizo fake ALAF mwenzake aliposikia hivyo akanipa tena Bati 50 zingine.

Akalipia usafiri wa kupeleka original Bati site na kusomba zile fake kurudisha dukani. Ni Zaidi ya Mwaka Bati zote zipo na same color.Pole sana ila kama una risiti ya Hizo Bati washirikishe ALAF mwende Dukani mkakomae nao
 
Mkuu kwa faida ya wengi ungeelezea jinsi ya kutambua which ni fake na which ni original
 
Back
Top Bottom