Roho inaniuma nimetimiza miaka 35 sina mtoto wala maisha

Binadamu tunataabika sana kwa kujifanyia ulinganifu katika maisha na watu wengine. MUNGU kila mja amempangia mapito yake.Wakati yeye anasikitika hana watoto na maisha yanayoeleweka, kuna mtu anapigania walau apone tu na dalili haipo! Tushukuru kwa kila jambo mkuu
Daa mkuu umemaliza kila kitu yani.
 
Si kila sehemu lazima uwe fundi kujua. Ulichofanya hapa ni ufundi kujua.

Mtu ana shida, anahitaji msaada na wewe unaleta ngonjera zisizokuwa na kichwa wala miguu.

Ndivyo ulivyofundishwa kwenu, mtu akiwa na matatizo suluhu ni kumchamba. Nimeshangaa sana mwanaume unachamba.

Kama ulikuwa huna cha kusema kumsaidia, akheri ungekaa kimya, wala usingepungukiwa chochote.

Inakuaje unaandika barua yote hii kumuharibia mtu siku, kumtonesha kidonda, kuongeza mzigo juu ya mzigo, kuongeza msiba juu ya msiba.

Wewe binadamu gani unaona fasheni kutokuwa na huruma dhidi ya binadamu mwenzio. Unasaidia watu kweli wewe?

Huenda husaidii, sio kwa kuibua huko dhana usiyo na uhakika nayo kama ina uhusiano na mtoa mada basi tu upenyeze mipasho! Halafu unamshauri afanye maamuzi asilie.

Seriously kuna mwanadamu hafanyi maamuzi! Tatizo la mtoa mada sio kutofanya maamuzi bali anafanya maamuzi yasiyo muongezea thamani anayoitaka. Ulipaswa umshauri afanyeje hayo maamuzi baada ya kuacha kulia.

Halafu Baba, Mtoa mada kasema anapambana na maisha na wewe unaibuka na ushauri wa "pambana watu wakupe hongera wanapoona mafanikio". Inaleta tofauti gani? Nicheke .

Mkuu C kama hutojali nicheki PM tushirikishane mawazo. Usimsikilize huyu fundi kujua ambaye kaokota kapoint huko anadhani kanaapply kila mahali. Lipo tumaini kumpata C unayemtaka. Kama hutoboi maana yake kuna mahali unazingua. So you need to take good care of it.

Nisamehewe mimi, nimetuma kama nilivyopokea.
Pole sana Kama post yangu imekuumiza kwa niaba ya muhusika!

Hata hivyo ukweli unatakiwa usemwe bila kupepesa macho. Sikufikiri Kama nimeandika "michambo" (hata sijui michambo ni vitu gani)

Mimi naamini ndani ya maelezo yangu endapo muhusika atayosoma kwa kutuliza akili hatakosa cha kujifunza

Usitegemee kila siku kupewa ushauri 'soft' huenda usikusaidie sana. Wakati mwingine unatakiwa uambiwe vitu katika uhalisia wake ili ujitafakari

Na mwisho kabisa, inabidi uelewa kwamba anayekusaidia kimawazo si lazima kupamba pamba maneno ili kukufurahisha ndo ujue anakutia moyo!

Wakati mwingine maneno magumu yanaweza kukusaidia zaidi kuliko maneno mepesi mepesi.
 
Roho inaniuma jamani leo nimetimiza miaka 35 kamili sina mtoto wala sina maisha licha ya kutumia miaka 10 katika kupambana na maisha.

Uzee sasa umepiga hodi taratibu hapa nilipo nahisi naanza kuchanganyikiwa kwa umri huu mpaka leo hii naishi maisha ya kubangaiza nipate hela ya kula miaka 35 yote hii.
Gender...?
 
Roho inaniuma jamani leo nimetimiza miaka 35 kamili sina mtoto wala sina maisha licha ya kutumia miaka 10 katika kupambana na maisha.

Uzee sasa umepiga hodi taratibu hapa nilipo nahisi naanza kuchanganyikiwa kwa umri huu mpaka leo hii naishi maisha ya kubangaiza nipate hela ya kula miaka 35 yote hii.
Brather usikate tamaa wanaume hatuzeeki piga kazi IPO siku mwanga utauona
Screenshot_2021-04-19-19-12-01-94.jpg
 
Kuna Jamaa alipata kazi akiwa na miaka 25 yaan mwaka mmoja baada ya kumaliza chuo kikuu..ila alikuja kufa miaka miwili baadaye yaan akiwa na miaka 27


Kuna mwengine yeye baada ya masomo, aliajiriwa akiwa namiaka 43 akaisha miaka 90


Hilo nisuala la Ajira tu..je wanaojiajili??


KATAA KATAKATA KUJIWEKEA DEADLINE KWENYE MAISHA....wengi wamejiwekea Deadline lkn matokeo yake, tarehe namwaka husika umefika na hawana kitu, wamejikuta ni watu wa msongo wa mawazo sanaaaaa...


Yaaan achana na mambo yakusema nikifika miaka 30 , nitakua na nyunba, gari kazi n.k

WEWE HUJUI KESHO YAKO .. AJUAYE NI MUNGU.


utapanga hili, lkn kumbe Mungu anataka akucheleweshe ili ujifunze jinsi gan maisha yalivyo,nasiku ukiyapata basi uyachezeee.


Muache Mungu aite Mungu ...Komaaa komaaa pambana pambanaa


KUSHINDA LAZIMA USHINDE SIO KWA HARAKA ILA UTASHINDA KWA UHAKIKA.


MUNGU HAPENDI WATU WAVIVU, WANAOKATA TAMAA
Asante Mkuu, nimejifunza kitu.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Dah! nina 27 tu lakin naona nipo nyuma sana mpaka inafika mahali nawaonea wivu walifeli sekondari, Ila nashukuru Mungu amenijalia mtoto mmoja japo napata taabu sana kutunza lakin kwakweli ndo anayenifanya nione raha ya maisha

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Daah miaka 35 huna mtoto ebu tupige hesabu ndogo hapa labda tuseme mwaka ujao unapata mtoto unakuwa upo na miaka 36 , mwanao anakuwa hadi anafika miaka 6 anaanza darasa la kwanza wewe unakuwa upo 42, anasoma hadi darasa la 7 wewe unakuwa upo na 49 mwanao anakuwa yupo na miaka 13....haya amefaulu kwenda shule ya sekondary ya kata anasoma hadi kidato cha nne, wewe unakuwa upo na miaka 53 wakat mwanao yupo na miaka 17 ...............daah itaendelea
 
Wakati wewe unalalamika hivyo, kuna mwenzako ana 35 na ana watoto kadhaa ila hana uwezo wa kuwahudumia na kuwapa mahitaji ya msingi.

Anawatazama wakiangamia na kuwa na dalili ya future mbaya. Hakuna kitu kina fedhehesha kama uwe na watoto ushindwe wapa malezi bora......

Anyways nikutoe hofu, mwanamke ndie anatakiwa kuvurugwa umri huo ukifika hana Ramani wala familia , kwa mwanaume umri huo ni saa moja asubuhi, bado mapema sana. Ila kwa mwanamke ni saa kumi na mbili jioni jua limezama kiza kimeingia.

Wewe hapo ndani ya huo umri wa miaka 35 unaweza chapa mimba wanawake hata 20 na wakakufanya baba wa watoto 20 ukiwa umri wa miaka 36 ila mwanamke hiyo haiwezekani hata kwa muujiza.

Mwanamke akifika 35 kwanza ana nafasi ndogo sana ya kupata zaidi ya watoto wawili. Ila ni impossible kuwa na watoto zaidi ya hao sababu ya complications mbali mbali za kiuzazi.

Imagine abebe ujauzito miezi 9, alee hadi miaka miwili tu hapo, tayari miaka mitatu hiyo. Miaka 3 jumlisha kwenye miaka 35 ana 38 akijiacha akae sawa baadae miaka 39 au 40 ndio mtoto wa pili..... So unaona namna inavyokuwa tofauti kwa mwanaume.

So nadhani unajitisha tu. Na mwanaume akishafika 35 mapenzi ya kisekondari huo muda hatakiwi kuwa nao.... Yeye ni kutafuta tu pesa.....
 
Roho inaniuma jamani leo nimetimiza miaka 35 kamili sina mtoto wala sina maisha licha ya kutumia miaka 10 katika kupambana na maisha.

Uzee sasa umepiga hodi taratibu hapa nilipo nahisi naanza kuchanganyikiwa kwa umri huu mpaka leo hii naishi maisha ya kubangaiza nipate hela ya kula miaka 35 yote hii.
Usikate tamaa bado hujachelewa! Life starts at 40.. Usijilinganishe na waliowahi.. Kila mmojawetu ana fungu lake na saa yake ya kupata
 
Back
Top Bottom