Roho inaniuma: Nimetimiza miaka 35 sina maendeleo yoyote ya kujivunia niliyoweza kuyafanya

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Ndugu zangu hatimaye nimetimiza miaka 35.

Kila nikijiangalia sioni kitu cha kimaendeleo au jambo la kimaendeleo nililolifanya ambalo ninaweza kujivunia mbele ya watu

Historia pekee iliyobakia ninayoweza kuisema ni enzi hizo shuleni nilikuwa nafanya vizuri na chuoni kufanya vyema lakini mpaka sasa sina maendeleo yeyote yale, nimekwama sijui naelekea wapi.

Ila ndo hivyo wadau.
 
Kutokana na uzoefu wa maisha uliyopitia wewe binafsi,ni dhahir sasa MUDA WA KUJIRIPUA( TAKE RISK AMBAYO HUJAWAH KUICHUKUA ILA USIUE WALA KUIBA)....


#2get sthng u Neva had,u av 2do sthng u Neva do#
Asante sana broo umenipa ushauri mzuri kiukweli ulichokizungumza uko sahihi kabisaa sina jinsi kabisa kufanya hivoo
 
Epukana na fikra za Chuo na Degree zitakupoteza.

Nadhani kwa umri huo sasa ushajua ni jambo gani hasa una uwezo wa kulifanya vizuri kwa uwezo wako.

Bila kumtegemea yoyote ( Kama ni kilimo ingia mwenyewe FRONT - Inapunguza Risks ) fanya jambo hilo hata kama lina faida kidogo ( compounding effect itafanyika ) lifanye kwa muda mrefu.

Acha kuruka ruka na jambo moja kesho jingine kesho kutwa jingine.

Maduka ya Reja reja hayana faida kubwa ila kinachowasaidia wachagga ni kuomaa nayo kwa muda mrefu ( plus janja janja effect ambazo huwezi kuzijua kama unarukia ruka kila siku na jambo jipya.

Kama ni Machingajaribu kuifanaya kwa muda huku ukiwa umetulia, utaona matokeo.

Hakuna kazi mbaya kwa kuanzia hata kama ina faida kidogo au mshahara kidogo.

You need to start somewhere.
 
Nadhani kwa umri huo sasa ushajua ni jambo gani hasa una uwezo wa kulifanya vizuri kwa uwezo wako.

Bila kumtegemea yoyote ( Kama ni kilimoingia mwenyewe FRONT - Inapunguza Risks )ingia FRONT mwenyewe fanya jambo hilo hata kama lina faida kidogo ( compounding effect itafanyika ) lianye kwa muda mrefu.

Acha kuruka ruka najambo moja kesho jingine kesho kutwa jingine.

Maduka ya Reja reja hayana faida kubwa ila kinachowasaidia wachagga ni kuomaa nayo kwa muda mrefu ( plus janja janja effect ambazo huwezi kuzijua kama unarukia ruka kila siku na jambo jipya.
Yeah,
Consistency, persistence, perseverance, continuity ...
 
Hupaswi kuwa na Career wala academic goals. Inapaswa kuandaa malengo ambayo yatafanya maisha yawe na mlinganyo sahili, mathalan afya yako ya mwili, mahusiano, na kuhakikisha afya yako ya kiakili ipo sawa. Hakuna siku utapata kombe kwa kuwa na mahusiano yaliyo na utapiamlo simply kwa kuwa malengo yako yalikuwa kwenye kumiliki material things. Don't take life too seriously,as we are really temporary here.

Duniani tumekuja kutalii tu na kuondoka , sana sana tukiwa na bahati we may last another 50 years kutoka sasa na kama ujuavyo mwezi mmoja una weekend 4 hivyo kuufanya mwaka mzima kuwa na weekend 48. Hivyo basi kwa muktadha huo ikiwa utajaaliwa miaka mingine 50 ni sawa na weekends 2400. Do we really need toget so worked up?....Ni sawa!

Unapaswa kuwa na elimu ya maarifa, kujipa likizo kwenye jambo lolote unalofanya, kupenda,kuwa na mitafaruku kidogo kwenye mahusiano, ...it's ok!

Usiwe serious sana kwenye maisha, kama maisha yanakuletea mapozi achana nayo fanya mambo mengine yaliyo ndani ya uwezo wako ili ufurahie kila moment as it comes.
 
Hilo nitatizo kwa watu wengi sana sana hasa awamu ya tano ,fikiria kijana aliyemaliza chuo 2015 hata kwa kozi zilizokua na ajira kama elimu hakuna tena ajira yan kama kijana alijua na 30yeas sasa ana 35+ yeara na bado hakuna ajira ndio maana unaona wamekimbilia ajira za ccm hali imekua ngumu kilichobaki ni kutangaza nia majimboni na kutukana upinzani ili mamlaka za uteuzi ziwaone wapate ajira hali so shwari kabisa ndugu
 
Hata hivyo smartphone unayomiliki ni hatua ya maendeleo, endelea kuwekeza na kuongeza bidii utafika unapopataka haijalishi utafika ukiwa na umri gani
 

Similar Discussions

19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom