ROHO inanisuta lakini utamu unanivuta

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Nilikutana na Binti mmoja pale Mlimani City na kuanzisha naye mahusiano ya kawaida lakini baadaye akawa mpenzi wangu. Lakini baadaye yule binti akanieleza kuwa ameolewa na anaishi na Mume wake pale River Side na wote ni walokole wa kwa mzee wa upako.

Siku mmoja alinialika kwake kwenye sherehe ya Graduation ya Wifi yake anayemaliza Form Four Mwaka huu. Tangu hapo mume wake amekuwa Rafiki yangu wa karibu mno na tunataraji kufanya biashara ya pamoja kuagiza bidhaa za vyakula kutoka mikoani.

Tatizo langu ni kwamba Binti kwa kweli ana mvuto lakini kwa upande mwingine najiona siwezi kumsaliti mumewe ambaye ni rafiki yangu mpya.

Sijielewi nifanyeje!?
 
Hichi huku mtaani tunikiita 'kiherehere' unitafunie mke halafu uje kuanzisha urafiki wa kinafiki na kutaka kufanya biashara na mimi ? nikigundua ni kisu cha tumbo tu.Vunja mawasiliano na hiyo familia kabisaa,badilisha namba ya simu,hama kwa kifupi kaa mbali nao.
 
Jivue gamba kwa mke wa mtu wewe lasivyo utakiona kilichomkuta DC wa Igunga achilia mbali yule magamba alokutwa na mke wa mtu!!
 
Siku zako zinahesabika. Mnaanza biashara pamoja, ukiweka tu mtaji wako mume anakufuta katika ramani ya walio hai. Kama mimi ningehama hata mji. Pole sana marehemu mtarajiwa..
 
labda alimtambulisha kama muumini mwenza walokole wanatabia ya kuaminiana haraka mtoa mada hajasema kama yy sio muumini wa hilo kanisa pia. aiseeeee mekuuu,mtwa,mangi,nk futa mawasiliano mapema mwambie mtaji wako umeibwa au umeghairi la sivo unajitafutia kifo,
 
mkuu jamaa amekuweka sokoni, kwenye hiyo biashara we ndio bidhaa.........
kimbia fasta mkuu, mke wa m2 sumu!!
 
unabalaa wewe, put urself into the shoes of that husband halafu uone ungefanyaje?
 
Back
Top Bottom