Roho imeniuma nimeachwa na mwanamke nimpendaye sababu ameniona sina mwelekeo mzuri wa maisha

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Imekuwa kama ni ndoto kwangu hatimaye Yule mwanamke niliempenda na nikiamini atakuja kuwa wife material hatimaye leo asubuhi ameniacha.

Amenipigia simu akiniambia nina maongezi na wewe kama uko sehemu tulivu Hebu kaa unisikilize akaniambia mambo mengi kuhusu haya mahusiano yetu mimi na yeye ila finally aliniambia mipango yake kuhusu maisha na akaenda mbali zaidi akaniambia mimi ndo kikwazo kikubwa kwake hivyo anachokiona nampotezea muda wake tuu hivyo tulipofikia hapa panatosha amenivumilia sana lakini sasa amechoka na ameona sina mwelekeo wowote kuhusu maisha.

Kwa sasa hapa nilipo sijui cha kufanya nina maumivu makali mnoo ninayoyasikia mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi mnoo roho inaniuma kumpoteza huyu binti sababu sina maisha.
 
Pole sana mkuu cha msingi we songa mbeoe tafuta maisha pambana na life kutafuta pesa wanarudigi wenyewe

usikate tamaa maisha ndivyo yalivyo kua mvumilivu na kupiga moyo konde yote ni mambo ya kawaida ila tafuta pesa mkuu

narudia tena tafuta pesa mkuu watarudi wenyewe hao
 
Kipi Bora kuacha sababu anaona huna muelekeo au kusalitiwa sababu anaona huna muelekeo???

Binafsi ningechagua kuachwa...wanawake km hao ni wazuri sana shukuru hajakupiga matukio sasa tafuta hela Kwanza....
 
Imekuwa kama ni ndoto kwangu hatimaye Yule mwanamke niliempenda na nikiamini atakuja kuwa wife material hatimaye leo asubuhi ameniacha.

Amenipigia simu akiniambia nina maongezi na wewe kama uko sehemu tulivu Hebu kaa unisikilize akaniambia mambo mengi kuhusu haya mahusiano yetu mimi na yeye ila finally aliniambia mipango yake kuhusu maisha na akaenda mbali zaidi akaniambia mimi ndo kikwazo kikubwa kwake hivyo anachokiona nampotezea muda wake tuu hivyo tulipofikia hapa panatosha amenivumilia sana lakini sasa amechoka na ameona sina mwelekeo wowote kuhusu maisha.

Kwa sasa hapa nilipo sijui cha kufanya nina maumivu makali mnoo ninayoyasikia mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi mnoo roho inaniuma kumpoteza huyu binti sababu sina maisha.
Pole sana kaka! Cha msingi piga moyo konde naamini haya maumivu ipo siku utabaki kuyasimulia tu na kua history wakati huo una maisha yako uliyoridhika nayo na furaha ya moyo wako itakua zaidi ya ilivyokua wakati uko na huyo mwanamke....!

Kuna wakati inabidi upitie maumivu makali sana katika mapenzi ili ujifunze kitu, na siku zote mwanamke unaekuja kuishi nae ni yule ambae hukua na plan naye kabisa wala yeye hakua na plan ya kuja kuishi naww ila ndo atakuja kuvumilia madhaifu yako na kukubari yote na atakupenda sana tu zaidi ya huyo ambae naweza kusema hakua na upendo wa dhati na sio mvumilivu, Yaani huyo mwanamke hata ungefanikiwa kumuoa maishani mwako ungepata shida sana....

Ungeyumba kidogo tu kiuchumi kwenye maisha yako KUGONGEWA au KUKUACHA ingekua easy mno... Ni bora hata umepata signal ya tabia yake bado hamjaingia ndani ya pingu ya maisha....

Kwa asaiv saka pesa kwa machungu yote uwe na maisha mazuri na uelekeo....
 
Mkuu salama

Mjumbe sijaona kitu cha kukufanya uumie hapo, iwapo tu una afya salama huo tu ni mtaji tosha
sasa ya nini kulia. Kaa chini jifanyie personal assessment wapi unabugi na nimanzi wa ngapi anakuleta michongo hiyo, Yafanyie kazi hayo mapungufu yako.

Tafuta michongo hapo mjini upige utamsahau kabisa na utapata mwingine mkali!

"Mapenzi ni mzunguko"

Shukrani!
 
Mkuu shukuru Mungu, amekueleza ukweli, umejua alihokuwa anakuwazia kwa kipindi kirefu bila wewe kujua. Katika hali kama hizo, Mara nyingi mwanamke huwa anakuwa alianzisha mahusiano na mwanaume fulani akiwa na matazamio makubwa juu yake kimaisha, hivyo inapotokea expected imekuwa tofauti na observed plus umri wake unaenda mbio lbd, pressure kutoka kwa marafiki zake wenye wanaume wenye uelekeo mzuri wa maisha,Shida huanzia hapo.
POLE SANA MKUU.
 
tunajaribu kuwa wema,maisha yanatafunya kuwa sisi.daah pole mkuu tuliza kichwa akili then upambane kuijenga great future
 
mkuu nipe namba yake ili asipotee kwa washenzi.......nitamtunza ukishakuwa na muelekeo nakusharudishia
 
Muda muafaka wa kumroga sasa..
Kama utaweza mtafute mchezaji wa mpira wa Manchester City anaitwa Gabriel Jesus aliwahi kupata shida kama yako ili akuambie yeye tatizo hilo alilimalizaje. Yeye kwa sasa anafurahia maisha kuliko mwanzo.
 
Acha kulia ila brother tafuta pesa aisee!! Hawa viumbe dawa ni men kuwa na kibunda chakuzidi!! Ayo maneno aliyokupa iyo hasira uliyonayo iwekeze kwenye utafutaji ukiwa na kibunda hata ukiachwa hauumii mzee.... Maana unakuwa na list yakueleweka!!! Me huwa naamini sana mwanaume ukiwa na pesa maumivu ya mapenzi hutokaa uyasikie
 
Pambana ndugu yangu...!!wenzio yamtukuta hayo hayo...!!tukafight asaiv anataka kurudi...!!ndivyo walivyo...!!tumia hasira na maumivu hayo kutafuta pesa mkuu....!!utazikamata hela mpk ushangae....!!Karma Is Bitch
 
Back
Top Bottom