Rocket ni ndege ya aina gani? Je upo uwanja wake hapa Tanzania?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,911
Swali langu ni kujuzwa kuhusu rocket ni aina gani? Ya ndege Maana naiona sana juu mawinguni inapita inatoa sijui ni moshi ule unakuwa mrefu hivi harafu baadaye unafutika,

Je? Uwanja wake upo wapi? Kwa hapa Tanzania Au inatua maeneo gani
 
Mkuu, ndege kubwa hasa za biashara zinatumia injini za jet. Zinapokuwa hewani huacha mistari meupe (moshi?)

Mvuke wenye unyevu nyevu wa gesi (una mchanganyiko wa carbon dioxide/hewa mkaa, sulphur, nitrojen, mafuta ambayo hayajaunguzwa, metal n.k) unaotolewa toka injini za jeti zikiwa angani kuanzia angalau mwinuko wa futi 20, 000 toka ardhini ambapo kuna joto dogo/mgandamizo mdogo wa hewa/ubaridi ambao hugandisha kwa muda hiyo gesi na kutengeneza kitu kinachoonekana kama moshi/mawingu. Ni kama ule mvuke/moshi anaopumua mtu kipindi cha baridi.

Viwanja vyote vikubwa ndege hizo huweza tua mfano Dar, Kilimanjaro na Mwanza. Hata Boeing 787 (dreamliner) yetu inatoa huo moshi ikiwa angani.
Kipindi cha utoto tulikuwa tunaita ndege za Urusi!
Screenshot_20200530-083913~2.png
Screenshot_20200530-083913~2.png
 
Hiyo unayoiona inaacha moshi nyuma sio rocket.

Ni ndege ya kawaida kabisa ya jet engine kama airbus au dreamliner za magufuli na hayo mawingu/moshi unaoachwa nyuma uanaitwa condensation trails kwa kifupi 'contrails' yanatokea pale hewa ya moto iliyotokea kwenye engine inapokutana na hewa ya baridi na kupoa haraka kutengeneza wingu
 
Rocket sio ndege kama unavyo fikilia, rocket ni chombo kinachotumiwa kupeleka vifaa au wanaanga kwenye anga za juu zaid na zile unazoziona pembeni yake zi atoa moshi ni injini zinazo fungwa ili kusaid kui-push kutoka nje ya dunia, ndio maana inapofika nje ya dunia zile injini zinajitoa maana zinakuwa hazina kaz tena.

Ndivyo mm ninavyo elewa
 
Mkuu, ndege kubwa hasa za biashara zinatumia injini za jet. Zinapokuwa hewani huacha mistari meupe (moshi?)

Mvuke wenye unyevu nyevu wa gesi (una mchanganyiko wa carbon dioxide/hewa mkaa, sulphur, nitrojen, mafuta ambayo hayajaunguzwa, metal n.k) unaotolewa toka injini za jeti zikiwa angani kuanzia angalau mwinuko wa futi 20, 000 toka ardhini ambapo kuna joto dogo/mgandamizo mdogo wa hewa/ubaridi ambao hugandisha kwa muda hiyo gesi na kutengeneza kitu kinachoonekana kama moshi/mawingu. Ni kama ule mvuke/moshi anaopumua mtu kipindi cha baridi.

Viwanja vyote vikubwa ndege hizo huweza tua mfano Dar, Kilimanjaro na Mwanza. Hata Boeing 787 (dreamliner) yetu inatoa huo moshi ikiwa angani.
Kipindi cha utoto tulikuwa tunaita ndege za Urusi!View attachment 1463237View attachment 1463237
Kwann ndege sizizotumia hizo jet engine hazito iyo kitu?
 
Hizo sio rocket,Ni jumbo jet,,rocket haina kiwanja,Ina launching pad,,pia rocket husafiri vertically sio holizontal Kama unavyoziona hizo jet zinazoacha mvuke,
Sawa zamani tukiona hivyo,tukidanganyana eti Ni rocket,siyo
Tofauti ya vertically na holizontal ni nini?
 
Kuna ndege zinatumia propeller engine na zile za jet engine,,za jet ndo hutoa huo mvuke,

Rocket zenyewe hutumia rocket engine na zinakuwa na propellent either solid ama liguid,ambazo ndo huungua kuform thrust,
Okay nimekuelewa mkuu
 
Kwenye porojo za mtaani unaambiwa Pakistan walirusha rocket kwenda mwezini baada ya siku moja wakatangaza wamegundua kuna maji kwenye mwezi. Jana yake India walikuwa wameshatangaza rocket ya Pakistan yaanguka bahari ya hindi.
 
Hahaha kwahyo bahari walihisi ni mwezi
 
Rocket toyote ya iran,iraq,Pakistan ikitua mwezini utasikia wamegundua kuwa mwezi ulishawahi kukatwa vipande viwili baadaye ukaunganushwa na mtume
 
Back
Top Bottom