‘Robotic politics’ Siasa bila ya hisia; Janga kubwa linalotunyemelea

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
1573816999168.png
1573836004820.png

Siasa za Tanzania kidogo kidogo zinajenga u ‘Yabisi’. Taratibu utu unapotea,kila mtu anahamia kuangalia tu kwamba yeye atapataje anachotaka bila kuangalia kwa kupata atakacho, wengine wata/wanaumia kwa kiasi gani. Hisia ‘feelings’ zinapotea, inabakia mimi napataje, wengine itakuwaje? watajua mwenyewe mbele huko. Politics without feelings!?Katika hatua yake ya juu kabisa nini kitatokea? Mtu yoyote akitulia anaweza kuwa na jibu ya swali hili.

Kitu kinachomtofautisha binadamu na Robot ni hisia (‘Feelings’ sio ‘emotions’). Hisia pia ndio humtofautisha binadamu na wanyama wengine.

Ukiangalia kwa mfano kwa upande wa akili; Robot lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa linaweza kuwa na uwezo wa kufikiri, kuchambua taarifa na kufanya maamuzi kutegemeana na ‘Facts’ kwa Usahihi, haraka na ufanisi mara 1000x…. ya binadamu wa kawaida.

Kwa mfano, Robot linaweza kufanya survey ya foleni Dar es salaam, likachambua na kutoa taarifa ya foleni itakavyokuwa miaka 20 ijayo, likapendekeza hatua za kuchukua, muda na namna ya utekelezaji N.k

Kitu pekee kinachomfanya binadamu awe na ufanisi zaidi ya roboti ni hisia. Binadamu wa kawaida anatarajiwa awe na hekima, busara na huruma kwa binadamu wengine na kila anapofanya uamuzi wowote, pamoja na kuangalia matokeo pia atumie ’feelings’.Hii pia ndio sifa pekee inayomtofautisha binadamu na mnyama kama chui ambaye yeye huangalia tu ni kipi anataka na kukikamilisha hata kama ni kwa kuwala wenzake.

Bila feelings, ubinadamu wa mtu hupotea, bila ubinadamu, robot lina ufanisi kuliko binadamu. Ndio maana hata wengine tunasema Katiba bora ni muhimu sana, ila busara na dhamira njema za mtu mmoja mmoja ni muhimu zaidi kwa sababu binadamu sio na wala hapaswi kuwa robot.

Je! Kama tukiamua kutojisahihisha, mwishowe hisia za ubinadamu zikipotea kwa kiwango cha juu kabisa katika siasa zetu, robots zinaweza kutufaa kufanya siasa badala ya watu?

Yaani kwa mfano unaweka robot kwenye ofisi ya mtaa fulani, halafu kila mtu akifika pale anaandika kero zake, robot linafaya mchanganuo kwa kutumia mifumo ya ki - kompyuta na kutoa solutions, kisha tunaenda kutekeleza?

Ikumbukwe robots haliwezi kuwa na chuki na mtu, haliwezi kudhuru mtu, haliwezi kupendelea, haliwezi kufanya ubaguzi, haliwezi kuwa na roho mbaya,Haliwezi na halina sababu ya kufanya ulaghai au hila, haliwezi kushughulikia maslahi yake lenyewe wala halina cheap propaganda; lenyewe linachukuwa to ‘input’, linafanya ‘process’ linatoa output limemaliza kazi yake ki roho safi kabisa.

Ndugu zangu, tujisahihisheni. Thamani ya binadamu ni utu na hiyo ndio humtofautisha na robot na wanyama wengine. Bila hiyo tumekwisha. Siasa zisitufanye tukapoteza msingi wetu wa asili na tukajikuta tunajidunisha katika kiwango cha kusikitisha.
 
Kwa maana hiyo ukiweza ukaifeed robot kanuni za uendeshaji bunge ukaiweka kuendesha bunge inaweza kufanya maamuzi sahihi na ya haraka kuliko binadamu.
 
Sahihi. ambacho itakosa tu ni hisia, yaani busara ambazo binadamu pekee ndiye anatarajiwa kuwa nayo.

Au hata ukachukua vipengele vya sheria Fulani ukavi codify kwenye robot, litasimamia kwa viwango vya juu sana, tatizo litakosa hisia. Sasa sisi tuliopewa tunu hiyo bure tunaipiga teke kwa sababu zisizo na msingi wowote
 
View attachment 1263710View attachment 1263717
Siasa za Tanzania kidogo kidogo zinajenga u ‘Yabisi’. Taratibu utu unapotea,kila mtu anahamia kuangalia tu kwamba yeye atapataje anachotaka bila kuangalia kwa kupata atakacho, wengine wata/wanaumia kwa kiasi gani. Hisia ‘feelings’ zinapotea, inabakia mimi napataje, wengine itakuwaje? watajua mwenyewe mbele huko. Politics without feelings!?Katika hatua yake ya juu kabisa nini kitatokea? Mtu yoyote akitulia anaweza kuwa na jibu ya swali hili.

Kitu kinachomtofautisha binadamu na Robot ni hisia (‘Feelings’ sio ‘emotions’). Hisia pia ndio humtofautisha binadamu na wanyama wengine.

Ukiangalia kwa mfano kwa upande wa akili; Robot lililotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa linaweza kuwa na uwezo wa kufikiri, kuchambua taarifa na kufanya maamuzi kutegemeana na ‘Facts’ kwa Usahihi, haraka na ufanisi mara 1000x…. ya binadamu wa kawaida.

Kwa mfano, Robot linaweza kufanya survey ya foleni Dar es salaam, likachambua na kutoa taarifa ya foleni itakavyokuwa miaka 20 ijayo, likapendekeza hatua za kuchukua, muda na namna ya utekelezaji N.k

Kitu pekee kinachomfanya binadamu awe na ufanisi zaidi ya roboti ni hisia. Binadamu wa kawaida anatarajiwa awe na hekima, busara na huruma kwa binadamu wengine na kila anapofanya uamuzi wowote, pamoja na kuangalia matokeo pia atumie ’feelings’.Hii pia ndio sifa pekee inayomtofautisha binadamu na mnyama kama chui ambaye yeye huangalia tu ni kipi anataka na kukikamilisha hata kama ni kwa kuwala wenzake.

Bila feelings, ubinadamu wa mtu hupotea, bila ubinadamu, robot lina ufanisi kuliko binadamu. Ndio maana hata wengine tunasema Katiba bora ni muhimu sana, ila busara na dhamira njema za mtu mmoja mmoja ni muhimu zaidi kwa sababu binadamu sio na wala hapaswi kuwa robot.

Je! Kama tukiamua kutojisahihisha, mwishowe hisia za ubinadamu zikipotea kwa kiwango cha juu kabisa katika siasa zetu, robots zinaweza kutufaa kufanya siasa badala ya watu?

Yaani kwa mfano unaweka robot kwenye ofisi ya mtaa fulani, halafu kila mtu akifika pale anaandika kero zake, robot linafaya mchanganuo kwa kutumia mifumo ya ki - kompyuta na kutoa solutions, kisha tunaenda kutekeleza?

Ikumbukwe robots haliwezi kuwa na chuki na mtu, haliwezi kudhuru mtu, haliwezi kupendelea, haliwezi kufanya ubaguzi, haliwezi kuwa na roho mbaya,Haliwezi na halina sababu ya kufanya ulaghai au hila, haliwezi kushughulikia maslahi yake lenyewe wala halina cheap propaganda; lenyewe linachukuwa to ‘input’, linafanya ‘process’ linatoa output limemaliza kazi yake ki roho safi kabisa.

Ndugu zangu, tujisahihisheni. Thamani ya binadamu ni utu na hiyo ndio humtofautisha na robot na wanyama wengine. Bila hiyo tumekwisha. Siasa zisitufanye tukapoteza msingi wetu wa asili na tukajikuta tunajidunisha katika kiwango cha kusikitisha.
Umenena vema mkuu.
 
Maendeleo hayana Chama wakati unstaka wenyeviti wote wa Mitaa na vitongoji wawe wanaCcm Inaingia akilini? Wasio na Vyama jee
 
Siasa zisitufanye tukapoteza msingi wetu wa asili na tukajikuta tunajidunisha katika kiwango cha kusikitisha
 
Back
Top Bottom