Robo Tatu ya Tanzania hawaujui Umeme siku ya Tatu Leo - Serikali! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Robo Tatu ya Tanzania hawaujui Umeme siku ya Tatu Leo - Serikali!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Aug 16, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Mgao sasa hauna Mipaka

  Thread hii ni ya Tarehe 22 July 2011 ambayo hapo awali zilianza kuonekana kama hadithi, pamoja na kuamua kuongeza Mega Watt 32 kutokana na Nishati ya Gesi sina hakika kama hili litawezekana.

  Dua zetu hizi mvua zinazonyesha mijini zingenyesha katika vyanzo vya maji ya Mabwawa tunakotegema HYDRO electric walau ukali huu wa maisha upungue.

  Robo tatu ya miji mingi ya Tanzania niliowasiliana nao juzi, jana na leo hawajauona umeme kabisa, hali ni mbaya zaidi kanda ya Ziwa na hasa jijini Mwanza ambapo muda mfupi uliopita imedhihirika kupitia Star TV na ndugu zake walikuwa Off kwa kukosa nishati kutokana na Mitambo yao binafsi ya kuzalisha Umeme kupata hitilafu.

  Sina Shaka tunaelekea Gizani Jumla kabla ya Desemba ya Ngeleja

  Siku 21 za Ngeleja: Taifa linaelekea Gizani Rasmi

  Nashtushwa sana na mbinu za serikali kuendelea kulifanya suala la upatikanaji wa Nishati ya Uhakika ya Umeme kuwa la kisiasa zaidi kuliko kupata ufumbuzi wa kdumu na kuwaeleza watanzania nafasi yake na uwezo tulionao katika kushughulikia tatizo hili.

  Tunaendelea kukwama kwa kasi ya ajabu kwa kuendelea kutegemea kudra ya Mungu kuendesha Nchi, huku kasi ya maovu nayo ikishamiri. Kwa mtaji huu wa maovu mengi kuliko mema kudra za Muunba zinatoka wapi kwa kizazi kilichomuasi? Huu ni mchezo wa kuigiza na ndotoza alinacha kuukwaa utajiri kwa mauzo ya kapu la vioo.

  Serikali inasisitiza kuwa haitasimamisha uzalishaji wa Umeme katika bwawa la Mtera kama ilivyofanya mwaka 2006, haya yanazungumzwa huku kiwango cha chini cha uzalishaji umeme katika bwawa hilo kinapigania roho kwa poniti zaidi ya 90 zilizosalia katika uwezo wake wa juu wa 698.50 mpaka kiwango cha chini cha 690 na ujazo wa hivi karibuni ni mita za ujazo 690.74.

  Vyanzo vyetu vingine ambavyo vinazalisha umeme vyote vipo taaban na vinafanya kazi chini ya kiwango na katika hatua zake za lala salama kabla ya kusitisha shughuli zake kutokana na kutokuwa na maji ya kutosha na hii ni kwa kiwango cha karibu zaidi ya asilimia 100 chini ya kiwango cha kawaida

  Kihansi kwa sasa ni MW 90 badala ya MW 180, Kidatu MW 40 badala ya 204, New Pangani MW 20 badala ya MW168 na Nyumba ya Mungu ni MW3.5 badala ya MW 8.

  Mamlaka ya Hali ya hewa haijatabiri kuwepo na Mvua katika chanzo chochote kati ya vyanzo vinavyokusanya maji kuelekea mabwawa haya si Ruaha Mkubwa wala Ruaha Mdogo na Kisigo wakati ambavyo hukusanya maji mengi kwa ajili ya bwawa la Mtera wakti wa kipindi cha masika.

  Sipati picha kwa kasi hii ya ongezeko la ukame ambao unashamiri tuna miujiza gani ya kupata nishati ya uhakika na ambayo haitakuwa inaelekea kukoma kabisa ndani ya siku 21 za Waziri Ngeleja alizopewa kusahihisha mapungufu yake katika Bajeti ya Nishati na Madini.

  Nashawishika kabisa kuamini kuwa baada ya kipindi si kirefu tunaelekea gizani jumla kama taifa hakuna cha mgawo wala jenereta kutoka vituo vya TANESCO kanda ambayo mengi kati ya hayo yamesimama muda mrefu kutokana na hitilafu za kiufundi na kukosekana kwa vipuri vya kuyakarabati.

  Tunaomba Neema za Muumba Mvua zinyeshe katika vyanzo hivi Taifa lisifike huko, maana kama tutafika huko. Mimi na wewe hatujui nini hasa itakuwa hatima ya Taifa letu.

  ADIOS
   
 2. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mimi umeme upo week nzima sasa
   
 3. n

  nrango Senior Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hakuna mkakati wowote utakaotekelezwa na hao vihiyo ccm,mfumo ni mbovu,hata mvua zikinyesha wataleta porojo nyingine.Ee mwenyenzi mungu wafumbue watanzania ili wafahamu ni nini hasa kinachowatesa...
   
 4. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  huku Mwanza mgao ni wa nguvu sana, umeme unarudi saa tano usiku halafu saa kumi na mbili asubuhi unakatika tena, basi hasira huwa zinaongezeka juu ya serikali ya magamba!
   
 5. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mtakuwa mnakamilisha Robo inayobaki katika Robo tatu kukamilisha kitu kizima
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mtakuwa mnakamilisha Robo inayobaki katika Robo tatu kukamilisha kitu kizima
   
 7. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nimeambiwa maeneo ya Ileemela, Pansiansi, Bugarika, Nyakato na Mkuyuni (Samahani kama nimekosea majina hayo) na Maeneo mengi ya mjini kati siku ya pili mfululizo leo hakuna umeme wala mjomba wake na umeme ni Jenerator kwa sana huku Bei ya Mfuta ikiwa imeongezeka ghafla hapo jana kutoka 2154 hadi 2264 kwa vituo vingi vinavyotoa huduma hiyo huko Jijini Mwanza
   
 8. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  ni kweli kwa sasa hapa Mwanza Petrol ni Tsh 2264, mchana maeneo hayo mengi uliyoyataja hakuna kitu kinachoitwa umeme mpaka saa tano usiku halafu saa kumi na mbili asubuhi wanauchukua umeme wao, sasa hapo sijui mtu utapiga shughuli zako saa ngapi!? Shughuli nyingi utakuta simesimama, naona wanatuletea umeme wa kuchajia simu tu! Kweli hii serikali ni hopeless!
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hilo janga kwa taifa hakuna jinsi bali ndio tuliowapa dhamana ya serikali kutuongoza
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nimependa sana katuni ya Kipanya ya Leo katika Gazeti la Mwananchi. Natafuta maarifa ya kuiscan niiweke hapa
   
 11. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ma majibu mepesi ndio utamaduni wao...Leo wanadudanganya kuwa wanafanya mpango kupata MW 32 kutoka Nishati ya Gesi. Damn
   
 12. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  nenda kwenye website inawezekana kaiweka au kwenye website yao mwananchi sehemu ya katuni..
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  na sehemu zilizomo kwenye hiyo robo ni zile za maeneo ya hospital za mikoa kama mwananyala maeneo ya muhimbili..
   
 14. REBEL

  REBEL Senior Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  poleni watu wa bara.visiwani huku wanakata umeme saa limoja tu kwa siku.
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Umeme wa dharura ya usiku na hospital. Ni kama nchi imetangaza hali ya hatari ya umeme hivi hutuhusiwi kuwa na umeme maana ni haramu! magamba! jamaa wame-prove failure! Nahisi kichefuchefu na tambo za ahari lukuki za last year election. Kama taahira vile!
   
 16. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Takwimu za TANESCO zinaonyesha kuwa Miji Mingi mikubwa ya Tanzania sasa inapata mgao wa Mega Watt 4 kwa siku ratio ambayo ni kama tone katika kujaza Pipa
   
 17. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Na mmefanikiwa Hili kutokana na wananchi visiwani kuvua Gamba huku bara bado tumevaa Gamba la umbumbu na Ujuha wa kuinamisha vichwa chini
   
 18. w

  wikolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hali ya umeme iliyopo kwa saa inakatisha tamaa kwa kiasi kikubwa sana. Kwa maoni yangu, wale waliopewa dhamana ya kushughulikia hili wameshindwa kwa zaidi ya 100%.Nipo Geita na umeme una karibu siku tatu sasa. Ulipatikana usiku wa kuamkia jana majira ya saa mbili usiku na ulidumu kwa muda wa masaa yasiyozidi mawili. Tangu wakati huo haujapatikana tena (labda kama utakuwa umerudi asubuhi ya leo) na hali kwa kweli ni hovyo kabisa na inasababisha watu wengi wanashindwa kufanya shughuli zao za kujipatia kipato. Hivi tutaendelea hivi mpaka lini? Kinachoudhi zaidi ni kwamba mwisho wa mwezi watanikata PAYE yao bila kusamehe hata shilingi moja wakati mimi umeme hawanipi kwa siku tatu mfululizo na bila maelezo yoyote!!! Anyway wengi wameshasema kwamba mambo kama haya yanapatikana Tanzania tu.
   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Na bajeti ya Ngeleja isha pita mbona patamu hapo!
   
 20. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Angalieni kusije kukawa na mgao maeneo ya Chadema pake yake. Niliongea na mtu wa Arusha mjini akasema ni kama wanakomolewa kwa kuchagua chadema maana mgao ni mbaya kupita kiasi.

  Chadema fatilieni hili kwenye majimbo yenu mjilIdhishe kama kweli huo mgao ni fair.
   
Loading...