Roberty Mugabe kufanyiwa 85th Birthday ya USD 250,000

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Rais Robert Mugabe alitimiza miaka 85 Jumamosi iliyopita na jitihada zimekamilika za kumwandalia hafla nzito Jumamosi hii ambayo itahudhuriwa pia na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai. Takriban dola za Marekani elfu 250 zimekusanywa na wafuasi wa Rais Mugabe kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Maadhimisho yatafanyiwa katika mji wa Chinhoyi, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Huku maankuli yakiandaliwa uchumi wa Zimbabwe umeporomoka na njia pekee yakuunusuru ni kuomba dola za Marekani bilioni mbili kutoka kwa nchi jirani.

Hadi sasa hakuna nchi yoyote ya kusini mwa Afrika ambayo imeitikia ombi hilo kwa kutoa ahadi ya kihakika.

Wakati huo huo visa vya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu inaongezeka. Zaidi ya watu elfu tatu unusu wakufa kutokana na kipindupindu.

Wenye shibe

Ili kupamba sherehe za 'Birthday' ya Rais Mugabe, mfanyibiashara mmoja ambaye pia ni afisa wa chama cha ZanuPF, Philip Chiyangwa alitoa mchango wa zaidi ya dola laki moja.

Serikali ya muungano inakumbwa na hali ya kutoaminiana

Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai ambaye amekuwa mpinzani mkali wa Rais Mugabe, naye pia hajawachwa nyuma. Atakuwepo.

Ni mwaka jana tu ambapo Bwana Tsvangirai alikejeli sherehe hizo na kuzitaja kuwa mkusanyiko wa wachache wenye shibe.

Muungano wa Rais Mugabe na Tsvangirai ungali unayumbayumba kutokana na hali ya kutoaminiana na kutokuwepo usawa katika ugawaji wa nyadhifa za uongozi.

Source: BBC
 
Rais Robert Mugabe alitimiza miaka 85 Jumamosi iliyopita na jitihada zimekamilika za kumwandalia hafla nzito Jumamosi hii ambayo itahudhuriwa pia na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai. Takriban dola za Marekani elfu 250 zimekusanywa na wafuasi wa Rais Mugabe kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Maadhimisho yatafanyiwa katika mji wa Chinhoyi, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Huku maankuli yakiandaliwa uchumi wa Zimbabwe umeporomoka na njia pekee yakuunusuru ni kuomba dola za Marekani bilioni mbili kutoka kwa nchi jirani.


TUME HURU YA UCHAGUZI ni kitu muhimu sana, manake KURA ya mwananchi itaheshimiwa. Ukiona mtu nchi yake ina njaa, kipindupindu nk, bado na wafuasi wake wanafanya sherehe kubwa hivyo, hiyo ni dhihaka kwa wananchi. Yani wanaonesha lolote watakalofanya hata wananchi wakasirike watakuwepo tu madarakani.

Kwa nini wasiitishe mchango angalau fedha zitakazopatikana zinunulie dawa za kipindupindu. Hawa wafanyabiashara wanachanga hela kibao, yote ni kulindwa na Serikali. Kweli Afrika tuna hatua nyingi tunakoelekea kwa demokrasia.
 
Kweli kabisa mambo haya ya kushinda kwa vyovyote yanaondoa umakini wa serikali za Afrika, wanafanya yale wanayotaka wao na kuona wananchi wote ni sisimi.

Hospital inataka $30,000 ianze operations na hawajui wazipate wapi wakati jamaa wanachinja ng'ombe na kunywa bia kwa $250,000. Ila siku moja waafrika watapata bahati ya kuwa na viongozi makini.

Soma zaidi kuhusu Mugabe's party kwenye link hizi.

Mugabe's B-Part on abcnews
Mugabe's B-Party on bbc
Mugabe's B-Party on CNN

One can say, these are western media who print Mugabe as a brutal dictator but the question here is why $250,000 for Birth day party?. This shows Zimbabwe is not as worse as we thought, though its wealthy may be concentrated within very few cronies of Mugabe.
 
Miaka 85 Mugabe kweli anajipongeza nini?

hana miaka mingi sasa ya kuishi mguu mmoja unaelekea kaburini kwani ni mtu mzee tayari

Hivi at 85 nini anatafuta cha zaidi?
 
Hapa Mugabe anatimiliza ule usemi kwamba 'The Poor Are Always With Us'.
 
Back
Top Bottom