Dodou
JF-Expert Member
- May 4, 2017
- 494
- 390
Nyota aliejipatia umaarufu katika kiwanda cha filamu baada ya kuigiza kama Vampire-Edward Cullen katika filamu za Twilight saga, amefunguka wiki hii alipokuwa akihojiwa na The Newyork times na kusema kuwa ilisalia kidogo tu atimuliwe kutokuigiza filamu hizo wakati alipokuwa akiigiza filamu ya kwanza Twilight ya mwaka 2008 kutokana na ugomvi na kutoelewana na viongozi wa filamu hiyo mpaka pale agent wake alipoamua kuingilia kati na kuweka sawa kila kitu
"Sikuhitaji kumnyenyekea mtu. Na sidhani kama nilifanya hivyo" alisema Pattinson na kueleza kuwa "Nauchukulia uigizaji wangu na mbinu zangu za uigizaji serious kiasi kwamba muda wote nilikuwa nikigombana na mtu yeyote aliekuwa akiniendesha.... mpaka kufikia hatua hiyo ya kutaka kufukuzwa"
Kwa upande mwingine alisema kuwa "Kuigiza Twilight filamu ya tano ilikuwa ni starehe ya ajabu kwani ilikuwa ni bahati kuwa katika kundi la watu ambao tayari nilifanya nao kazi katika filamu hizo, na moja ya kitu kizuri ni kuwa unapoigiza filamu za muendelezo basi unatakiwa kukubali jukumu la kuigiza uhusika ule ule"
Robert Pattinson mwigizaji ambae amezaliwa May 13 mwaka 1986 huko London Uingereza ameigiza baadhi ya filamu kama Harrypotter, The lost City of Z, Cosmopolis na Good Time ambayo itaachiwa rasmi Marekani August mwaka huu. Pia aliisifia filamu ya Cosmopolis ambayo aliigiza baada ya kuigiza filamu za Twilight mwaka 2012 kwa kusema kuwa "Nafikiri ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufanya kitu kilichokuwa na ugumu kiasi flani na hasa naupenda ukweli kuwa ni filamu ambayo ilitoka tayari nikiwa na umaarufu wangu, ilikuwa ni mabadiliko makubwa kwangu nilitambua kuwa hicho ndicho kilikuwa kitu ambacho nilitaka kufanya"
Robert Pattinson ataigiza yeye lakini usimwambie kuangalia movie zake kwani zinamfanya ajihisi na kujipatia wakati mgumu na kuwa huwa anakuwa na hali ya aina flani pale ambapo watu hukosoa kazi aliyoifanya au watu kumwambia kuwa amewakilisha kitu flani, huku akisema kwa utani kuwa "karibia huwa naogopa mtu akisema kuwa kitu nilichofanya ni kizuri"
Mwaka 2010 Robert Pattinson alitajwa na jarida la Forbes kama miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi Zaidi dunuiani na mwaka huo huo pia Forbes ilimtaja kama mmoja kati ya watu maarufu wenye nguvu Zaidi duniani.