Robert Mugabe a liberator or tyrant?

mleta mada nadhani utakuwa umekurupuka humjui na kufaham historia ya huyo jemedari ambaye wazungu waligonga na kufyta mkia
mfano mzuri ni rais wa pekee aliyekubali ushoga zimbabwe kwa sharti ya kumuoa Obama,wakati marais wenzake wa Afrika wakiwa wanakwepa kama wanakubali au kukataa ushoga kwa uoga wa kutengwa na USA,na ndio maana ni rais pekee ambaye inasemekana aliendesha nchi kidikteta but hao hao walio mtoa hawakutana kumpindua bali kwa mazungumzo na kumuomba na kumuahidi mambo kibao ambayo hata baada ya kuachia ngazi alikuwa akipatiwa kwa 100%
R.I.P MUGABE SIMBA WA AFRICA
 
Mungu ndie anaye jua wapi ataenda ila Mimi namtakia pepo maana alinifurahisha kuchukua mashamba ya wazungu kuwapa wazawa
Kweli??? Siyo alijipatia mwenyewe na wenzake, familia za komredi zake wa juu? Siyo Grace Mugabe amakamata mashamba ngapi?? Na je masikini wangapi walipata?
Kwa hiyo tutofautishe waporaji na wezi kufuatana na rangi?
 
Asilimia kubwa ya ubaya ulionekana kwa Mugabe ni wa 'kuchonga' Wazungu sio watu wazuri!!
je umewauliza watoto na wajukuu wa Wandebele 20,000 waliochinjwa na Brigedi ya Tano ya Mugabe mnamo 1982/84?
Katika mauaji ya Gukurahundi ?
Soma hapa: Zimbabwe begins exhuming victims of Gukurahundi massacre
 
Zungumzeni mambo yote lakini kumbukeni hadi sasa hivi " Zimbabwe sio Koloni na haitakuwa koloni tena " Pumzika kwa Amani Jongwe Robert Gabriel Mugabe, sote njia yetu ni moja, tangulia wengine tupo njiani twaja
 
TELEMMGLPICT000208530488_trans_NvBQzQNjv4BqVq7v3XiGTWaNhf-5XDoWgJJ_JKHlDCgS6YVllv4j1sA.jpeg

Robert Mugabe, George Silundika na Joshua Nkomo jijini Dar-es-Salaam, 1963

TYRANNIES ALWAYS COLLAPSE -Agnes Heller, Hungarian Philosopher

himaya za kinduli siku zote huanguka, dikteta limekufa, liliua watu 20,000 wa kabila la Ndebele kwa kumuunga mkono mpinzani na mwanamapinduzi mwenzie Joshua Nkomo.

February 1982 dikteta Mugabe alitangaza "...Nkomo ni chatu ndani ya nyumba, na namna pekee ya kukabiliana na nyoka ni kumshambulia na kumponda kichwa." Baada ya hapo akatuma vikosi vya makomandoo kwenda kufyeka kabila la Ndebele.

Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 mpinzani Morgan Tsvangirai alikuwa amejificha kwenye ubalozi wa Uholanzi ndani ya Harare kunusuru roho yake. Sasa y
amefika mwisho.


EDxvgBKWsAU_zvu.jpg

taswira ya mwisho ya dikteta Mugabe nchini Singapore

halafu haya madikteta yanatawala miaka 40 na bado hayajajenga hospitali au kusomesha waganga wa kuwatibu wanapoelekea kufa, hawana aibu.

Kwa nini tumelazimishwa kuomboleza siku tatu?
 
Hivi Mugabe hajawahi kuuwa wapinzani wake? Ukiuwa unaenda MOTONI KWA IMANI YA DINI YAKE .
 
Lkn madikteta mapepo hayawezi kuwaacha siku zote hawana cha kujifunza. Dictators die hard.
 
Habari wana JF. Africa tungekuwa na viongozi aina hii wengi kwa umoja wetu mabeberu wasingetusumbua. This was Mugabe. Kweli chini kunakula watu bwana
 

Attachments

  • EEE8BCCD-7239-47CE-AB42-62DE12B17013.MP4
    1.3 MB
Habari wana JF. Africa tungekuwa na viongozi aina hii wengi kwa umoja wetu mabeberu wasingetusumbua. This was Mugabe. Kweli chini kunakula watu bwana
Wengi wamebaki waganga njaa na kutembeza bakuri, waroho, wezi wala rushwa ndiyo wamebaki Africa. Kizazi kile kilikuwa strong, freedom fighter, patriotic, kweli kweli.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom