Robert Kisena wa UDA na wenzake, wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa Mashtaka 19

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group, ambao walikuwa wamiliku wa UDA, Robert Kisena amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

MKURUGENZI UDART NA WENZAKE WASOMEWA MASHTAKA 19 LIKIWEMO LA UTAKATISHAJI FEDHA

Mkurugenzi wa UDART, Robert Kisena(46) na wenzake watatu akiwemo raia wa China, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 19 yakiwemo ya utakatishaji na kusababisha UDART hasara ya zaidi ya BIL. 2.41.

Mbali ya Kisena, washitakiwa wengine ambao wote wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ni Kulwa Kisena(33), Charles Newe(47) na Cheni Shi (32). Raia wa China.

Katika mashtaka hayo, lipo shtaka moja La kuongoza uhalifu, shtaka moja La kujenga kituo cha mafuta bila kibali, shtaka moja La kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa.
20190211_170433.jpeg

Kwa kumbukumbu:
Robert Kisena atangaza kufilisika kwa UDA

Huyu ndiye Simon Kisena mnunuzi wa UDA?

Sakata UDA: Hivi ndivyo madiwani na wabunge wa DSM wanavyotuhumiwa kuhongwa kufunika kombe - JamiiForums

Sakata la Ukwapuzi wa UDA kufufuliwa? - JamiiForums
 
Hapo safi!
KOsa gani mkuu? Ni ile ile kesi ya siku zile baadaye kesi ikafutwa baada ya kampuni kumtembelea waziri mkuu akiwa Dodoma? Kama ni hivyo anzieni hapo! Hiyo ziara ya dodoma!
 
lilikua ni swala la muda tuuu huyu jama kutoshitakiwa.

makandokando yake ni mengi sana,ukianzia alivyo mzibua mitama yule OCD zama zile za uchaguzi wa 2010.
 
Nimeskia Na Michael Wambura nae kapandishwa Kisutu

Magufuli sio wa kumfanyia mchezo Kwenye vita dhidi ya Rushwa

Namuona Mwl Nyerere Kwenye wajihi wa Kiutawala wa Rais Magufuli

JPM Ni ' Nyerere Junior'
Acha kulinganisha simba na mbwa mwitu kwamba wako sawa, simba ni simba na mbwa mwitu ni mbwa mwitu
 
Back
Top Bottom