Robert Kisena Ana jeuli ya Watawala Kiasi cha Kumpiga Ngwala OCD !!!

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225
OCD ADUNDWA NA MGOMBEA UBUNGE CCM POLISI WASEMA NI "JAMBO LA KAWAIDA"

Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa CCM alifika kituo cha polisi na kusababisha sokomoko baada ya kumshambulia kwa mateke na kumuangusha chini mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Maswa (OCD), Peter Ndunguru akimtuhumu kuwa wamemwachia Shibuda.

Akizungumza kwa njia ya simu, OCD Ndunguru alisema mgombea huyo wa CCM aliambatana na viongozi wa chama hicho na kuuliza alipo Shibuda, na walipojibiwa kuwa yupo rumande mgombea huyo alimrukia OCD huyo na kuanza kumshambulia kwa mateke kiasi cha kumuangusha chini.

“Alinirukia na kunipiga,” alieleza OCD.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga amethibitisha tukio hilo, akisema kuwa kulitokea kutokuelewana kati ya afisa wake na mgombea huyo, lakini akadai kuwa hilo ni jambo binafsi ambalo analiacha mikononi mwa OCD mwenyewe.

“Suala la Kisena na OCD ni jambo la kawaida kiutendaji na wala siwezi kulizungumzia... kwa sasa hapa ninashughulika na suala zito la mauaji," alisema kamanda huyo wa Shinyanga.

"Suala hilo lilitokana na kutoelewana kati yao... kama OCD anaweza kumfungulia mashitaka ni yeye lakini sisi hatuna haja naye. Lakini nadhani tutawashauri wayamalize kwa kuwa ni ya kawaida kiutendaji.”

Source;Gazeti la Mwananchi


 

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,243
2,000
waendelee kuwalelea tu kuna siku watawakojolea mdomoni, kisa kulinda maslahi ya wakubwa...
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Mkiamua kufufua basi muwe mnaweka na ukweli kuwa ni habari ya zamani au japo uweke ya zamani uhusianishe na jambo la sasa la sivyo inakuwa haina maana! !!!!!!

Umeshindwa hata japo kutunga swali ili watu wajadili hili kama rejeo la tukio????!!!!
Halafu ikifutwa utasema unaonewa au mods wana uoendeleo!!!!????

Kuna mjadala hapa tena wa muhimu sana ila umebana hoja
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,150
2,000
Mkiamua kufufua basi muwe mnaweka na ukweli kuwa ni habari ya zamani au japo uweke ya zamani uhusianishe na jambo la sasa la sivyo inakuwa haina maana! !!!!!!

Umeshindwa hata japo kutunga swali ili watu wajadili hili kama rejeo la tukio????!!!!
Halafu ikifutwa utasema unaonewa au mods wana uoendeleo!!!!????

Kuna mjadala hapa tena wa muhimu sana ila umebana hoja
kwa mara ya kwanza nakuunga mkono, una hoja kidogo kwenye hii post
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
kwa mara ya kwanza nakuunga mkono, una hoja kidogo kwenye hii post

Bila ya kusema kwa nini huungi siku nyingine na kuweka vigezo vya kukubali leo mi nakuona hujielewi tu mzushi flani hivi na kama vipi usiunge mkono hata hii iki kuonesha msimamo wako!!!!!
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,150
2,000
Bila ya kusema kwa nini huungi siku nyingine na kuweka vigezo vya kukubali leo mi nakuona hujielewi tu mzushi flani hivi na kama vipi usiunge mkono hata hii iki kuonesha msimamo wako!!!!!
dah! sory mkuu,nilichanganya ID yako na ID nyingine ya Lizaboni, hahahaha, pole sana aisee, nimefuta kauli.
 
Last edited by a moderator:

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,404
2,000
Zamani sana hii kitu haha haaah, miaka minne almost jamaa anapiga dili tu na saizi anaingilia kinga na madaraka ya Bunge hakuna wa kumgusa. Mtoto wa mfalme Riziwani Kikwete yuko juu sana.
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
dah! sory mkuu,nilichanganya ID yako na ID nyingine ya Lizaboni, hahahaha, pole sana aisee, nimefuta kauli.

Kaka asante sana nawe nisamehe kwa lugha kali kwanza!!!!!

Ila kunifananisha na huyo kiumbe kweli ulikosea mkuu zumbemkuu!!!!!!
Narudisha shilingi kwenye heshima yetu!!!!!
 
Last edited by a moderator:

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
1,225
Robert Kisena alianza siku nyingi kuiweka serikali mfukoni
Hadi sasa record zake zinaeleweka
Ila sasa hii ya kumpiga ngwala OCD ilivuka kiwango!
 

bategereza

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
3,322
0
Alimuona polisi njaa au fisi. Angegusa musacha kutoka poti mbona tungeongea mengine sasa hii
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,698
2,000
Paw hebu tuondolee huu usumbufu, uzi huu peleka uungane na ule uzi wa mwaka 2010 hapa ni kuwaletea usumbufu wadau tu kwa old news au ikiwezeka ufutilie mbali.
 
Last edited by a moderator:

busha

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,646
2,000
Hawamu za utawala zilizopita zilikua hivi...
Ili uweze kuipiga vizuri serikali ni lazma ugombee ubunge..ili uwende bungeni ambapo ni rahisi kukutana na mawaziri...

Ndo maana wapigaji wengi walikua au waliwai kugombea ubunge...

Kisha unaipiga serikali kwa msaada wa waziri,katibu wa wizara n.k..

Kama umepiga dili la b moja unatoa m kumi kwenye chama kufadhili...

Ukishafikia hapo sasa serikali unaiweka kwenye walet...sio polisi wala mahakama..

Kuna maeneo baba jeska tumuelewe wakuu....Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom