Ripoti ya mauaji nyumbani kwa waziri

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,850
155,804
Nyumbani kwa Waziri Celina kombani yalitokea mauaji ya kutatanisha mwaka huu.
Polisi waliunda tume ya kuchunguza mauaji hayo.
Hadi leo kimya kikuu kimetawala.
Je ni kwamba kombe limefunikwa ili mwanaharamu apite?
 
Kwani ripoti ya mabomu ya Mbagala ilishatoka?
Mtangoja milele na mtakufa bila kelele kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetere.
Msifanye mchezo na wanasiasa.
 
Nani atakayekuwa wa kwanza kuukiri ukweli huo.
Ccm inatumia kivuli cha amani na utulivu kuvunia kura huko vijijini.
 
Huyu Waziri Kombani mbona anahusishwa na mambo machafu machafu mengi? Kuna yule mtumishi wa halmashauri ya Bagamoyo aliyekwiba fedha za mradi mpaka ikabidi waziri mkuu amsimamishe kazi inasemekana alikuwa anamkatia kidogo huyu mama; halafu wale wafanyabiashara wa madini waliouawa na kumuhusisha Zombe pia huyu mama alikuwa na uhusiano nao; pia kuna mauaji ya kutatanisha yalitokea nyumbani kwake na mpaka hivi sasa bado polisi wanapeleleza. Je mtu wa namna hii anafaa kuwa kiongozi wa serikali?
 
This is TZ. Hakuna cha ripoti wala nini. Ukisikia tume imeundwa unadhani mwishoni itaandaa ripoti??? ni full usanii, watu wanakula posho za tume na kisha mambo yanaendea kama yalivyozooleka - business as usual.

- ripoti ya Richmond imeishia wapi?
-tume iliyoundwa kufuatilia mabomu?
-tume ya kufuatilia vinasa sauti kwenye hotel ya silaha

-kila kitu kinaundiwa tume
 
Huyu Waziri Kombani mbona anahusishwa na mambo machafu machafu mengi? Kuna yule mtumishi wa halmashauri ya Bagamoyo aliyekwiba fedha za mradi mpaka ikabidi waziri mkuu amsimamishe kazi inasemekana alikuwa anamkatia kidogo huyu mama; halafu wale wafanyabiashara wa madini waliouawa na kumuhusisha Zombe pia huyu mama alikuwa na uhusiano nao; pia kuna mauaji ya kutatanisha yalitokea nyumbani kwake na mpaka hivi sasa bado polisi wanapeleleza. Je mtu wa namna hii anafaa kuwa kiongozi wa serikali?

Hawa wafanyabiashara walikuwa wanatoka kwenye jimbo la uchaguzi la huyu mama kwa hiyo kwa namna yeyote alipaswa kuhusika na vifo vya hao wafanyabiashara!
 
Nani anajari uhai wa wengine..hakuna..tutakufa tu ..tutaendelea kulalamika tu lakini hatuna serikari inayajari uhai na maisha ya raia wake.hakuna.:A S-eek:
 
Wana Jamii ripoti za uchunguzi zinakuwa siri mpaka pale zinapotangwaza hadharani ndio inakuwa public document. Tusubiri labda iko katika kutfanyia uchunguzi ili wale jamaa wapelekwe mahakamani, ingawa sio vibaya kuuulizia kwa DCI kama tume bado inaendelea na kazi.
 
Tume za kiafrka zina majungu wanakuja wakina ocampo wanachunguza wanaondoka,sisi tunang'aa sharubu ! We have to raise our voices.enough is enough.
 
Back
Top Bottom